Maisha yananikatisha tamaa sana

Miaka 26 huna ndugu unajilaumu my nigga uza smartphone nenda town kawe chinga ludi hapa baada ya miezi 6 utuambie Kama bado una iso stress
 


Kama hupo na pumzi na mzima wa Afya mshukuru Sana Mungu .
 
Usichoke omba Mungu mkuuu sisi pia tunapitia changamoto izo izo ulizo nazo ila Mungu ni tumaini letu
 
Jitahidi utafute mwenza. Na tambua nguvu pia ni mtaji tosha kama uko timamu kiafya na akili. Hivyo ukiishi ndani ya kipato chako na kupunguza kama si kuachana na matumizi yasiyokuwa ya lazima, kidogo kitakuwa kikubwa na kukuwezesha kutekeleza unachokihitaji. Hatima ya maisha yako ni namna unavyofikiri na kutenda. Katika kutamatisha, Ibada, zaka na sadaka toa.
 
Kukata tamaa dhambi ktk maisha. Anza na kufanya hata kibarua utafanikiwa uwe na mtazamo chanya
 
😂😂😂😂😂kwny adverts zenu mnasemaga awe anapumua ila kwny real life mnaanza kuingizia issue za hela
Sa utapumuaje kama una njaa? Bila kushiba tutazagamuana vipi? Pesa ya kubadilisha mboga na mambo mengine ya msingi lazima iwepo
 
Mwili na akili yangu imezoea sana mchakamchaka wa kazi, yaani nikikaa bila kujishughisha najisikia unyonge sana
Kuna shughuli nyingi tu zenye mchakamchaka na zenye kukuingizia kipato, tafuta site za Ujenzi, omba kuwa saidia fundi, Nenda masokoni jichannganye kubeba mizigo ama kusaidia wanunuzi kuwabebea vifurushi vyao, Nenda shamba kalime.. Au jisogeze mabondeni anzisha bustani ya mboga mboga kisha jitangaze kwa majirani mtaani utapata wateja wa kutosha sana..

Kila la heri
 
Kama we ni mwanaume
Mtafute fundi ujenzi ambae hapoi hapo mtaani jiunge nae puyanga nae we uwe saidia fundi wako utanufaika yafuatayo.
1.Utapata skills za ki mason na kuna siku utakuwa fundi
2.Utakuwa unakula site wakati wa kazi
3.Utarudi magetoni umechoka hata mawazo ya kulialia na kudeka hutakuwa nayo maana utakuwa umechoka utalala kama kiroba au mzimu.
4.Kwa vile huna msaada jiambie wewe ndie msaada wa maisha yako uliebaki so aminia kutumia akili na nguvu kwenye jambo lolote lilopo mbele yako ili mawazo yakutamani waliokufa yakutoke.
MAISHA ni magumu sio kwako tu sema tunapishana mapokezi na reactions.
DOGO KAZA BORA UFE UKIWA MAPAMBANONI
 
Tatizo vijana wanatumikishwa na ndoto za maisha bora bila kujali mchakato wake.
Mfano mimi nilimaliza chuo nikaomba pagale jirani nikaanza kufundisha watoto hadi chekechea baadae nikanunua machine ya kufyatulia tofali humo kwenye kufyatua matofali dream job yangu nikakutana nayo leo hii nipo familia ambayo hata wengine wanaitamani pia kwenye top 3 ya madon wa ukoo na mimi nimo.
 
Huyu ana mchezo sana. Kwanza anafaa afurahie kwa kuwa hana mzazi anayemtegemea. Anajipambania yeye binafsi.

Wanaume wanalala nje kutafuta rizki halafu huyu anachoka? Pumbqv sana
 
Manisha haya mkuu, kuna kipindi unajiona umechelewa halafu unakutana na mtu kakuzidi miaka 20 ana hali mbaya kukuzidi na bado anapambana
Ndio hivyo mkuu kila mtu na fungu lake kwa wakati wake kikubwa ni kutokukata tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…