Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mkuu,Hatuwezi kujadili jambo ambalo halipo, yaani halijawahi kutokea na haliwezi kuja kutokea.
Kwa nini tujipotezee muda kwa kuwaza na kujadili mambo ya namna hiyo?
Hili ni jaribio la kufanya fikra dhahania. Abstract thinking.
Tunaweza kujadili fikra dhahania. Na tumejadili.
Ukifanya hesabu tu umefanya fikra dhahania. Bila fikra dhahania hakuna hesabu wala sayansi.
Hii internet yenyewe imeanza kama fikra dhahania.
Labda unataka kusema hutaki kujadili fikra dhahania, haina faida.
Kutotaka unaruhusiwa, ni uamuzi wako, lakini, kuna faida za kufanya fikra dhahania.
Kwanza kabisa, fikra hizi zinatupa nafasi watu weusi kujifikiria tulipo, sehemu yetu katika dunia, mchango wetu, zinajenga empathy, kuweza kuifikiria dunia kutoka position ya mwenzako.
Kwa mfano, sasa hivi kuna mazungumzo mengi sana ya "white privilege" na ubaya wake. Watu weusi wengi wana wepesi sana wa kuwasema wazungu kwa "white privilege". Kwa mtu anayefikiri kwa kina, maongezi haya yanaweza kuzalisha swali. Hivi sisi weusi tungekuwa dominant culture, mimi nikawa na "black privilege", ningeijua hiyo black privilege? Ningesemwa kwa hiyo "black privilege" ambayo nimeipata kwa bahati nasibu ya kuzaliwa tu bila kuitaka wala kuipanga, kusemwa huko kungekuwa sawa? Kulifikiria seali hiki kunaweza kumpa mtu msimamo mzuri zaidi kuhusu kuwasema wazungu kwa "white privilege".
Kufanya fikra za kidhahania kunatusaidia kuongeza creativity, kuchambua mambo vizuri na kwa kina, kuweza kubadilika vizuri zaidi, kuongeza critical thinking, kuongeza uwezo wa kuona dot zinazoungana, kuongeza uwezo wa kujielewa mwenyewe, kuongeza uwezo wa kushirikiana na kuwasiliana vizuri, kuongeza emotional intelligence, kuongeza uwezo wa kuelewa mambo kifalsafa zaidi, kuobgeza maendeleo ya kisayansi na teknolojia, kuongeza uwezo wa kujieleza kisanaa na kuweza jufanya maamuzi mazuri zaidi.