Nilikuwa nataka kuanza kuielezea concept ya Trinity yaani utatu mtakatifu lakini umeniambia huko nyuma ya kwamba unaifahamu kuhusiana na uungu, na uanielewa vizuri Biblia inatufundisha hivi
Matendo 17:29 Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.
Halafu bwana Yesu akatufundisha hivi
Mathayo 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Katika hilo fungu la Mathayo hali hizo tatu ndio utimilifu au ukamilifu wa Mungu mmoja,
Zaburi 89:26 Yeye ataniita, Wewe baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.
Warumi 9:5 ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Mungu mwana ndiye ambaye kwake yeye ulimwengu uliumbwa
Waebrania 1:2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
kwa hiyo kwa maana nyingine Yesu ni neno la Mungu, hili ni kati ya somo gumu kwasababu najua nizalisha maswali mengi kwa mfano watu wataanza kuuliza Kwanini basi Yesu anaongea mwenyewe kuhusu yeye mwenyewe kwenda kwa baba yake na Mungu wake (Yohana 20:17)? kwanini anamwomba Baba kama Mungu wake(Yohana 17:1, Mathayo 27:46)? Kwanini anasema kwamba Baba ni Mkuu kuliko alivyo yeye(Yohana 14:28) kama Yesu mwenyewe ni Mungu(Yohana 1:1)?
Hayo maswali nimeyajibu huko kwenye concept ya Incarnation nikajaribu kukupa na vifungu vichache, japokuwa najua hadi kwasasa hivi unakataa, lakini aina mbaya kwasababu umeniambia Trinity unaielewa vizuri ngojea nijibu swali lako, lililobaki hapa chini
Hapo nilipoweka red alichukuliwa na Mungu Baba
1 Wathesalonike 1:10 na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.
Hapo nilipoweka blue nimekwisha lielezea, ila angalia hii Timotheo
1 Timotheo 3:16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Hapo nilipoweka purple nimekwisha elezea, labda na mimi nikuulize swali, naweka hapa chini aya ya Qurani halafu nakuuliza swali
Qurani 19:17
Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.
Sasa
Mashaxizo kulingana na hiyo aya Jibril aliweza kuwa na sura ya mwanaadamu kamili na wewe unapinga concept ya God Incarnate
Swali: Ikiwa Malaika aliweza kujifananisha na kuwa mtu je Mungu hawezi? Malaika na Mungu nani ana uwezo zaidi!?