Yah! Nimeyaona mkuu. Nilikua hai hai kidogo.
Ok tuendelee...
Kutokana na majibu yako:
Inshort. Yesu hajalaaniwa wala hajafanyika laana.
Si ndio?
Umetumia 1 wakorinto 1: 18 na umepinga Wagalatia 3: 13 iloyosema:
...kwakua alifanywa laana kwa ajili yetu...
Jee tukopamoja hapo?
Kama sio fafanua.
Kama ndio. Huoni unaamini baadhi na kuacha baadhi?
Kwani kumbukumbu la Torati 21: 22-23 sidhani kama inamuongelea Yesu. Wakati wagalatia imempoint Yesu.
...
Hapo kwenye nilipoweka red, nafikiri umeshindwa kulielewa neno, Paulo alikuwa ananukuu maneno ya Torati, kwamba amelaaniwa na Mungu aliyetundikwa mimi nilichokifanya nimekupeleka kwenye Torati aliyoinukuu, kwasababu agano jipya limekuja baada ya Yesu, ila vitabu vya agano la kale vilikuwepo kabla ya Yesu, Torati ni ya Musa, na ndio iliyoandikwa hivyo, sasa mimi nilichokifanya nikakupeleka kwenye hilo fungu la Torati ambalo limeandikwa hivyo nikakupa na vigezo ili kwamba mtu alaaniwe ni lazima awe na dhambi, na pili anatundikwa akiwa amekwisha kufa, ndio maana nikakuuliza yale maswali, je Yesu alitenda dhambi, ambapo umekataa, nikakuuliza tena je alitundikwa akiwa amekufa... ikaonekana ametundikwa hai
Hebu sasa tuliangalie hilo fungu la Wagalatia
Wagalatia 3:13 Kristo alitukomboa katika laana ya
torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu;
maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
Hapo kwenye hilo andiko hapo juu zingatia hizo bold, kwa hiyo kumbe torati ndiyo iliyosema hivyo, Mtume Paulo anasema maana imeandikwa, imeandikwa wapi sasa!? mimi nilichokifanya nimekupeleka sehemu ilipoandikwa na mtume Paulo aliponukuu ambapo ndio kwenye torati...
Hapo nilikuwa nakuonyesha msingi wa kulielewa neno, na mtume Paulo alichokuwa anakisema hapo ni kweli, kwamba alifanywa laana pasipo kuwa na laana, kutokana na vile vigezo nilivyokupa, tena Paulo anasema kwa ajili yetu...
Sasa unapopinga, tena kwenye hilo andiko ulilolichukua, Mtume Paulo anaeleza kabisa maana imeandikwa, na ni kweli imeandikwa na nimekupeleka sehemu iliyo andikwa ambapo ni kwenye Torati
Sasa hapo nilipoweka red unachokataa ni kipi!? wakati Wagalatia imenukuu Torati, kwa hiyo tatizo jingine nililoliona kwako ni ile hali ya kushindwa kulielewa neno, ndio maana unakuja na hitimisho Biblia imechakachuliwa... kumbe ni mtu kutolielewa neno
Jibu la maswali yako:
Mimi naamini Yesu hakulaniwa. Na naamini wagalatia imesema uongo.
Mimi naamini bible pale inaposema kweli na pia ikisema uongo, naamini hapa bible inatudanganya.
Msimamo wangu huo ni tofauti na wewe unaeiamini yote wakati bible imechakachuliwa sana.
...
Naomba uondoe shaka yoyote ktk hayo maelezo yangu na naomba ucomfirm whether unaiamini yote or baadhi. Ili, nichukue nafasi ya kukuthibitishia bible imechakachukuliwa. Nitatumia aya chache kutoka Qur-an na aya nyingi nitatoa ktk Bible.
...
Naomba mwongozo.
Hapo nilipoweka red pia maelezo niliyoyatoa hapo juu nadhani yanaeleweka, nimekwisha lijibu hapo juu, Naiamini Biblia yote
Hapo nilipoweka Blue unaweza ukaendelea, kwasababu nimekwisha ielewa shida yako na Tatizo kwanini unasema hivyo, okay sawa leta hayo maelezo...