Maiti ya kichanga yafikisha siku 40 mochwari kusubiri DNA

Maiti ya kichanga yafikisha siku 40 mochwari kusubiri DNA

Buza Kwa Mpalange

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
268
Reaction score
156
Mgogoro kati ya uongozi wa kituo cha afya Nguvu Kazi kilichopo Nyeburu, Chanika mkoani Dar es Salaam na wazazi umesababisha maiti ya mtoto mchanga kukaa mochwari kwa siku 40.

Mgogoro huo ulianza baada ya mama wa mtoto huyo Maisha Ally kujifungua Septemba 7 kituoni hapo na kupewa taarifa kuwa mtoto wake alipelekwa hospitali ya Amana na kisha kufariki dunia wakati akipata matibabu.

Kufuatia kauli hiyo Maisha na mumewe Stephano Alphonce walikilalamikia kituo hicho kuwa kimeuza mtoto wao na kuamua kuisusa maiti hiyo inayodaiwa kuwapo hospitali ya Amana hadi kufanyike uchunguzi wa vinasaba (DNA).

Kufuatia malalamiko hayo Septemba 15 Serikali iliunda kamati ya kuchunguza utata huo ambayo ilianza kwa kuwahoji wazazi wa mtoto huyo na watumishi wa kituo.

Baada ya kamati kufanya uchunguzi, Oktoba Mosi mwaka huu ilijiridhisha kuwa kuna ulazima wa kupima vinasaba vya mtoto huyo na wazazi wake yaani ili kujiridhisha zaidi.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri alisema bado uchunguzi unaendelea na watatoa majibu pindi utakapokamilika.

“Tume iliyoundwa inaendelea na uchunguzi na bado taratibu za uchukuaji na upimaji wa vinasaba unaendelea, hivi karibuni tutatatua suala hilo,” alisema Shauri.

Akizungumza nyumbani kwake Septemba 14, Maisha alisema waliisusa maiti hiyo kwa kuwa utaratibu wa mtoto kuhamishwa hospitali haukufuatwa na kulikuwa na udanganyifu wakati wa mchakato wake wa kujifungua.

Tofauti na utaratibu ulivyo, Maisha alidai alipojifungua hakuonyeshwa mtoto, wala kuambiwa amejifungua jinsia gani, lakini ndugu zake walipokea taarifa kutoka kwa wauguzi kuwa alipojifungua alipoteza fahamu ilhali yeye akidai kuwa alichomwa sindano ya ganzi pekee na alikuwa na fahamu.

“Nilijifungua Septemba 7 saa saba mchana kwa njia ya upasuaji kwa kuchomwa sindano ya ganzi mgongoni. Wakati wa upasuaji ilikuwa kimyakimya sikuambiwa chochote wala kuonyeshwa mtoto. Baadaye saa 10 ndugu walikuja na shangazi aliingia nikaongea naye, ila niliona anashtuka,” alisimulia Maisha.

©Mwananchi
 
Subira yavuta kheri ! Si walisusa ? Wasubiri vipimo ukweli udhihirike
 
Niliiona kwenye interview ya Zamaradi, very sad, iwe mtoto ni wa kwao ama hapana, the pain is unbearable.
 
Uswahili mtupu yani. Jumanne shauri mzee wa watu anatoka mvi bila kupenda ana majukumu mazito ya kitaifa bado kuna waswahili kama hawa wanazingua bangi.
 
Mbona wanamtesa kiumbe wa MUNGU.
lile baridi la mule sio mchezo.
Marehemu wanageuka kuwa weusi.
Wamzike tu.
 
Kesi ya nyani anapelekewa ngedere mtuhumiwa daktari na vijana wake na mpima DNA daktari na vijana wake unategemea majibu yatokaje hata kama sio.
 
Kesi ya nyani anapelekewa ngedere mtuhumiwa daktari na vijana wake na mpima DNA daktari na vijana wake unategemea majibu yatokaje hata kama sio.
Kwenye kesi kama hizi, upimaj wa DNA unafanyika katika utaratibu wa "blinding". Watakaofanya huo upimaji hata hawatajua sampuli za wazazi ni zipi, na kutakua na pair mbili za sampuli zingine. Wapimaji hawatajua sampuli za wazazi halisi ni zipi. Ndio maana hiyo process inachukua muda, lazima maandalizi yafanyike kuhakikisha kuwa upimaji unafanyika bila bias.
Mdomowabata
 
Kwenye kesi kama hizi, upimaj wa DNA unafanyika katika utaratibu wa "blinding". Watakaofanya huo upimaji hata hawatajua sampuli za wazazi ni zipi, na kutakua na pair mbili za sampuli zingine. Wapimaji hawatajua sampuli za wazazi halisi ni zipi. Ndio maana hiyo process inachukua muda, lazima maandalizi yafanyike kuhakikisha kuwa upimaji unafanyika bila bias.
Mdomowabata
Hapa umetoa mwangaza mkuu...shukran kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom