Maiti za vichanga zakutwa mtoni

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Miili ya vichanga wawili wanaosadikiwa kuwa mapacha imekutwa kwenye Mto Nairobi Jijini Nairobi nchini Kenya katika zoezi la usafi

Watoto hao walikutwa wakiwa kwenye mifuko ya plastiki mmoja akiwa bado akipumua lakini alipoteza maisha muda mfupi baadaye. Walizikwa karibu na walipokutwa

Mamlaka zinaamini miili hiyo inatupwa kwenye mto huo na mahospitali baada ya utoaji mimba ambao ni kinyume cha sheria nchini Kenya

Gavana wa Nairobi, Mike Sonko ametoa wiki moja uchunguzi ufanyike maana hii ni mara ya nane tukio kama hili la kukutwa miili linatokea ndani ya miezi michache

Licha ya miili ya watoto nane, maiti za watu wazima wanne pia zimepatikana tangu zoezi la kusafisha mto lianze
 
.Yaani mtu anatupa mapacha .Kweli watu hawajui baraka ni nini.Very sad 😫 😫😫 😫
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…