Majaji 10 wameteuliwa na mahakimu 91 wameajiriwa

Majaji 10 wameteuliwa na mahakimu 91 wameajiriwa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
MAJAJI 10 WAMETEULIWA NA MAHAKIMU 91 WAMEAJIRIWA

Katika kuongeza kasi ya utendaji kazi, Mahakama imeendelea kuongeza idadi ya Maafisa Mahakama.

Katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 jumla ya Majaji 10 wameteuliwa (Mahakama Kuu – 5 na Mahakama ya Rufani – 5) na hivyo kufanya idadi ya Majaji waliopo kufikia 146 (Mahakama Kuu – 107 na Mahakama ya Rufani - 39).

Vilevile, Mahakimu 91 wameajiriwa na hivyo kufanya idadi ya Mahakimu kufikia 1,426 (Mahakama za Mwanzo - 195 na Mahakama za Hakimu Mkazi - 1,231)

Huu ni utekekelezaji wa Bajeti ya serikali ya mwaka 2024/25 kwa Wizara ya Katiba na Sheria eneo la Kuimarisha Usikilizaji wa Mashauri.

Kumbe Majaji sio Mahakimu??😂😂😂😂😂
 
Kumbe Majaji sio Mahakimu??😂😂😂😂😂
Jaji anahudumu kuanzia ngazi ya mahakama kuu hadi mahakama ya rufani.

Hakimu anahudumu kuanzia ngazi ya mahakama ya mwanzo, mahakama ya wilaya na mahakama ya hakimu mkazi/ mahakama ya mkoa kama ilivyo Kisutu.
 
Screenshot_20250507_003140.png
 
Back
Top Bottom