Katika kuongeza kasi ya utendaji kazi, Mahakama imeendelea kuongeza idadi ya Maafisa Mahakama.
Katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 jumla ya Majaji 10 wameteuliwa (Mahakama Kuu – 5 na Mahakama ya Rufani – 5) na hivyo kufanya idadi ya Majaji waliopo kufikia 146 (Mahakama Kuu – 107 na Mahakama ya Rufani - 39).
Vilevile, Mahakimu 91 wameajiriwa na hivyo kufanya idadi ya Mahakimu kufikia 1,426 (Mahakama za Mwanzo - 195 na Mahakama za Hakimu Mkazi - 1,231)
Huu ni utekekelezaji wa Bajeti ya serikali ya mwaka 2024/25 kwa Wizara ya Katiba na Sheria eneo la Kuimarisha Usikilizaji wa Mashauri.