MAJAJI WACHAGULIWE, katiba mpya itamke hili.

MAJAJI WACHAGULIWE, katiba mpya itamke hili.

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,537
Reaction score
6,472
JAMANI, MAJAJI watajwe kwenye katiba mpya kwamba wachaguliwe, ili kuwa na independence of judicially nzuri na pia kuwe na discouragement ya rushwa kuliko ilivyo sasa. pia tutapata majaji wenye uelewa mzuri na sifa za kutosha, sio hakimu fulani tu anateuliwa, chukua mfano yule mama Lema pale kisutu ateuliwe kuwa Jaji na anavyokula rushwa, what do you expect?

tunataka majaji wachaguliwe kama ilivyo Kenya na marekani. hapo ndio wataacha nyodo zote za rushwa, na pia hawatakuwa na deni lolote kwa serikali, yaani hawatafanya kazi kwa kuiogopa serikali au hawatakuwa biased. kwasababu kwenye kuteuliwa na rais, kuna majaji wengine wamepandikizwa tu na serikali.

Tundu Lisu alichosema ni cha kweli, ukiangalia judgement za majaji wengine, utachefuka kwa kingereza, poor English kuliko hata form six leaver wa Katelero. ukienda kwa mahakimu, wana kimombo kibovu ajabu, sasa hao hao mahakimu ndio wakifanya kazi muda mrefu wanateuliwa kuwa majaji, what do you expect? tunataka wachaguliwe na bunge, waitwe pale mbele ya bunge wajieleze na kuulizwa maswali, wapimwe uelewa wao na wapigiwe kura. kama kuna mwanasheria yeyote ambaye amekutana na kuwafahamu majaji atakubaliana na mimi jambo hili. ndugu zangu ili kuwa na upatikanaji wa haki hapa tz, lazima tupiganie hilo lipite kwenye katiba mpya.
 
Samahani mkuu mimi umeniacha njia panda!Kuchaguliwa unamaanisha nini hasa? Hebu mfafanua kiundani kidogo pendekezo lako la mchakato wa kuwachagua hao majaji. Wanachaguliwa na majaji, wananchi,bunge au vipi?
 
Afadhali ndugu yangu MWILI NYUMBA umeuliza maana nami Hute kaniacha njia panda, jaji wa mahakama kuchaguliwa? Je ni kupitia sanduku la kura? Sijawahi kulisikia hili popote.

Karibu tena mkuu Hute utufafanulie zaidi huu mchakato wa kuchagua majaji wa mahakama.
 
Last edited by a moderator:

wanatakiwa kuchaguliwa na wabunge, ambao ni wawakilishi wa wananchi. ndivyo inavyofanyika hata kenya kwa katiba mpya hii. hata kama angeteuliwa na rais, lakini in order to be approved, lazima apitie bungeni, akajieleze, apigwe maswali, wabunge waone anafaa ndio wampitishe, rais kupewa rungu lote peke yake ni power kubwa mno, ndio maana anaweza kuweka watu wake wa channel zake. that's what i mean. angalia hata marekeni ilivyo.
 
Ok Mkuu Hute, hapa tupo pamoja sasa. Naona ulimaanisha zaidi kuimarisha vetting mechanism, ni kweli ni bora bunge likawa linawafanyia usaili kupitia a designated committee ambapo huko queries zote juu ya conducts na utendaji wao zitaibuliwa na kupatiwa majibu. Lakini kumbuka hili halitaondoa appointing authority bali kuimarisha uwazi na ufanisi.
 
yap, kama ulishawahi kusoma baadhi ya judgement za hao majaji wetu wa High court, wengi wana kiingereza cha form four au six, huwezi amini unachosoma. kumbuka, pamoja na kwamba baadhi ya majaji hawa huwa wanachaguliwa toka kwenye list ya mawakili wa serikali na mawaikili wa kujitegemea kama kina jaji fauz, almost 70% ya majaji wote huwa wanakuwa ni wale walioanzia uhakimu. hivyo mwingine alikuwa hakumu wa wilaya, akawa hakimu mkazi, halafu anapata ujaji. namna ya kupigania vyeo hapa bongo nafikiri unaijua, wengi wamefanya manjonjo na shortcuts kibao na jaji mkuu na jaji kiongozi ili wateuliwe,....ukiwa na mke hakimu, tema mate chini, hao niliowataja na majaji wengine wote ni waume wenzio. na wana amri na mamlaka kam apolisi na jeshini...hivyo wanapata ujaji toka uhakimu kwa shortcuts tu. na wakifika pale wengi ni mambumbumbu kabisa, wengi ni wala rushwa mno, wanaishiwa kupewa v8 la kutembelea, kunyonya mafuta everyday na dereva wa kumuendesha, wengine pamoja na mlinzi. hawana lolote kichwani na hao ndio wanaoharibu kesi ajabu. uliza mtu yeyote ambaye yupo kwenye hii field ya sheria, utalia mchozi.

ukiwa mahakamani, kwamfano kama wewe ni wakili wa serikali/prosecutor, kazi kubwa unayoifanya ni kupambana na jaji/hakimu namna gani utamzibia mianya ya rushwa, kwasababu from day one kesi imefunguliwa kwake, yeye anaangalia tu namna gani atapiga, si namna gani atafanya haki. tunahitaji uadilifu, na watu wakichujwa na kuwekwa kitimoto, bila shaka watajiona wako accountable kwa kiasi fulani, kuliko kuwaachia tu uhuru wa manyani.
 
Kweli kabisa Hute
Mahakama ya Tanzania kwa sasa imeingia doa, mbaya zaidi inaharibiwa na insiders wenyewe zaidi.

Kuhusu quality ya majaji tatizo ni mfumo wenyewe. Unajua Tanzania inategemea sana individual capacities kuliko uimara wa mfumo wake kuweza kudhibiti/kuendesha mambo. Wananchi wengi wameliona hili ndiyo maana hata maoni yao mengi juu ya katiba mpya ni udhibiti wa mambo, natumai tume ya Mzee Warioba hawatafumbia hili. Ndio maana chini ya mfumo mmoja wa serikali waziri mmoja anatimiza vema wajibu wake na mwingine ni business as usual. Speaker yule alikuwa bora huyu anafumbia macho kanuni, Rais yule hakuwahi kulaumiwa juu ya uteuzi wa majaji na huyu analaumiwa. Hakuna kabisa consinstency ya uwajibikaji.

Tukirudi katika mapendekezo yako pia hakutakuwa na ufanisi kama hakutafanyika over-hauling ya mfumo mzima wa utendaji maana hata Bunge pia lina matatizo as Mahakama na Executive. Ukilipa bunge kazi ya vetting ya hao wateule kwa hali ilivyo sasa ni
bure, it'll be only rubber stamping. Katiba mpya inahitaji kujenga taasisi imara, very independent na ufanisi katika check and balance za mihimili mikuu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom