Nimefuatilia kikao cha waziri mkuu leo na wafanyabishara kuhusu mgogoro wa kariakoo nimesikitika sana.
Licha ya kwenda na Mawaziri na Timu ya wataalamu wa Wizara mbalimbali ameshindwa kutatua matatizo ya wafanyabiashara wa Kariakoo.
Amepata fursa ya kuwasikiliza wafanyabiashara siku nzima ya leo halafu anaishia kuunda tume ambayo hata haifahamiki inaenda kufanya kazi gani kama matatizo yote ya wafanyabiashara yameelezwa hiyo tume inaenda kufanya kazi gani.
Tume imeundwa bila hadidu za rejea bila ukomo wa kuhitimisha kazi yake na mbaya zaidi hata mambo ambayo yalihitaji kufanyiwa maamuzi hata wale wafanyabishara waliokamatiwa mizigo yao inaachiwa tume hiyo ambayo haina mamlaka kisheria.
Matatizo mengi yaliyosemwa na wafanyabiashara yamesababishwa na mawaziri wa fedha na viwanda na biasharana TRA lakini waziri mkuu ameshindwa kutoa tamko lolote dhidi ya viongozi hao na kukimbilia kuunda tume kama njia ya kupoteza hoja za wafanyabiashara hao.
Unawaingiza wafanyabiashara kwenye tume ambao wanayo majukumu yao ya kibiasharana kifamilia bila hata ridhaa yao kwa muda usiojulika na hizo shughuli zao zinabaki kusimamiwa na nani?
Wafanyabiashara wamekueleza waziri mkuu kuwa matatizo yao wamekuwa wakiyaeleza kwenye vikao mbalimbali vya Task Force ya kikodi na vya wizara ya fedha bila mafanikio leo hayo mapendekezo ya tume uliyounda yanapelekwa wapi ya katekelezwe na nani.
Hii inathibitisha kwamba nchi yetu haina Waziri Mkuu Mama Samia yuko peke yake ni aheri angeenda yeye mwenyewe kutatua matatizo ya wananchi wake badala ya waziri mkuu ambaye ameenda kupiga porojo na kuyaacha matatizo kama alivyoyakuta.
Bado tunakumbuka matume mbalimbali ambayo waziri mkuu amekuwa akiyaunda na hayana matokeo na hayana mrejesho wowote hadi leo na amesahau kwamba alishawahi kuunda tume ya kuungua soko la kariakoo ambayo hadi leo hajapeleka majibu ya tume kwa wafanyabiashara wa kariakoo.