Angalia uongo wa polisiccm kuhusu kukamatwa kwa Mbowe. Hivi yule dhalimu mwendazake kama Mbowe angekutwa na hatia ya kupanga njama ya kuua Viongozi wa juu Serikalini angemwacha huru tangu September mwaka jana?
Ni jambo la kheri kuwa sera rasmi kuhusiana na Covid-19 hatimaye imebadilika uelekeo kwa nyuzi 180. Kwamba kama uelekeo ulikuwa mashariki, tumegeuka nyuma kuelekea magharibi.
Mwanga mpya wa matumaini unaanza kujitokeza. Chanjo toka kwa wahisani tuliowaanzishia mabeberu zimeanza kutufikia bila malipo.
Utaratibu wa haraka na ufanywe sasa ili chanjo zilizopo zianze kutolewa kwa wanaozihitaji pasipo na muda kupotea tena.
Ikumbukwe tulikuwa tumetanga mbali huku tukijidanganya kuwa tuko vizuri: View attachment 1866962
Wakati hali kamili mahospitalini ikiendelea kuwa mbaya zaidi:
Tungali na tatizo kubwa la uelewa lilosababishwa na porojo za awamu ile kuhusiana na huu ugonjwa.
Wasiokubali bado kuwa ugonjwa huu upo na wala si vita vya kiuchumi wangalipo na ni wengi. Wasiokubali chanjo kuwa ni salama, upigwaji na zenye kushutumiwa kuteketeza afya zetu kama njama tu za mabeberu nao wangalipo na si wachache.
Kuwafumbia macho waliotufikisha hapo bila kuwawajibisha, hakuwezi kuwa na manufaa. Ni muhimu sana waliokuwa vinara wa upotoshaji huu wakaachia ngazi wenyewe kwa manufaa ya taifa kwa kujiuzulu au kwa kufurushwa.
Kwamba mawaziri Majaliwa, Jaffo na vigogo wote wizara ya afya wangalipo ofisini kuendelea na mapambano na ugonjwa huu? Bado wana dhima ipi hawa dhidi ya ugonjwa huu?
Kuwa na timu mpya kutaleta msukumo na mwanzo mwingine utakaotuletea kuwa na tija zaidi. Kutambua na kukiri wazi wazi kuwa tulipotoka kutapunguza ukakasi kwenye kuwataka waumuni wa awamu ile nao kubadilisha uelekeo.
Hii pia ingekuwa funzo kwa wote kwenye kusisitiza uwajibikaji katika dhidi ya maslahi yoyote binafsi.
Mabibi na mabwana awamu ya tano imepita na sasa kazi inaendelea katika awamu ya sita chini ya Rais Samia. Kwamba tupo awamu ya sita itakuwa kutojitendea haki mno kutoyaangazia kabisa madhara ya awamu ya tano kwa awamu ya sita yote chanya na hasi. Kwa uzi huu itoshe kuyaangazia madhara hasi ya...
Itakuwa kujidanganya kama taifa kudhani kuwa tuko vizuri. Matumaini mapya yaliyoibuka baada ya SSH kuchukua nchi yamekwisha baada ya siku 100 ofisini. Kama taifa tunayumba tokea kwenye corona hadi kwenye mustakabala kama taifa. Taifa limegawanyika hisia kali na munkari juu: 1. Kuhusiana na...
Mimi si mwanasiasa bali najali sana yote yanayojiri nchini ikiwemo dhuluma na udhalimu wa kutisha kama vile kutekwa, kupotezwa, kubambikiwa kesi FEKI etc ili tu wahuni waendelee kutenda dhuluma na udhalimu wao nchini wa miaka nenda miaka rudi. Ndiyo maana nasema siku ukitia akili kichwani utaelewa tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.