Majaliwa kastaafu siasa au kastaafishwa?

Angeendelea kugombea mngesema king'ng'anizi, amestaafu mnakuja kuanzisha uzi kuhoji maamuzi yake, watanzania vp mbn hamna jema? Nchi hii fanya mambo yako funga masikio
 
Angeendelea kugombea mngesema king'ng'anizi, amestaafu mnakuja kuanzisha uzi kuhoji maamuzi yake, watanzania vp mbn hamna jema? Nchi hii fanya mambo yako funga masikio
Tabia zao.....ukiona kaondoka ujue basi kuna fimbo.
 
Mke wa kikwete anapata mafao yoteeeee lakini Kwa ulafi Leo anagombea tena aiseee
 
Chawa mwandamizi, Samia analindwa na Watanganyika na ndio wanaong'ang'ania aendelee kukaa hapo ili waibe vizuri.

Siyo sahihi kuwasema Wazanzibar kwa dhambi isiyowahusu wakati ukweli mnaujuwa mama yupo hapo kwa maslahi ya genge la Msoga.

Awamu ya 4 imerudi madarakani kwa kutumia exit door.

Mpaka uwe na akili ndio utalijuwa hili.
 
Nani siyo Mzee? Acheni kubeza Wazee Uongozi siyo kubeba Zege. Ni Utulivu, Busara na Hekima. Ahaaaa Ujana ndiyo uongozi au Majigambo?? Trump , Museven, hwaongozi tena kwa ufanisi mkubwa? Njaa tuu na uchawa unawasumbua nyie mnaojiita Vijana.
Kwahiyo role model wa uongozi wetu hapa Tanzania ni akina Museveni? 2015 tu hapa JK alitumia kigezo cha umri kuwakata akina mzee Lowasa na wenzake, kwamadai kuwa kundi kubwa la wapiga kura ni vijana, leo hii unaturudisha nyuma kuwang'ang'ania wazee. Hawa vijana akina Mavunde na wenzao mnaowalea ni lini watashika hatamu za uongozi wa nchi? Utumishi wa umma ni mbio za kupeana vijiti, wamefanya kazi nzuri, tunawapongeza na kuwashukuru, lakini umri wakustaafu ukifika, ni vizuri wastaafu. Hutusemi hivi kwakuwa tunawachukia, la hasha! Tunasema hivi kujenga utamaduni wa watu kutokung'ang'a kufia madarakani.
 
Ameombwa asichukue fomu ili akachukue nafasi nyeti ambayo itakuwa wazi soon ndani ya chama kwakuwa anayeishikiria sasa alipewa nafasi nyingine pale jk convention kuelekea October 26. mwenye D mbili kaelewa
 
TUNGEKUWA NA BUNGE IMARA WABUNGE WANGEKATAA NCHIMBI KUJIUZULU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…