Majaliwa Stadium uwe reference kwa viwanja vingine Ligi Kuu

MwananchiOG

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
1,970
Reaction score
4,037
Ukiacha viwanja vikubwa vinavyojulikana kama Mkapa Stadium na Azam Complex, Kwakweli huu uwanja wa Majaliwa licha ya kuwa mkoani lakini una muonekano mzuri sana na standard hususan kwa vilabu vidogo vya mikoani zinazoshiriki ligi kuu.Ni aibu kwa baadhi ya timu tena kongwe kama JKT kutumia uwanja ambao unasikitisha na kudhoofisha sana ubora wa ligi yetu. Nadiriki kusema uwanja wa Majaliwa una pitch nzuri sana kuliko hata CCM Kirumba.

Hongera sana Namungo fc

 
Pale Songea kuna ule wa Majimaji nao mzuri sema ndio hivyo Team yenyewe sijui imepigwa na laana gani
 
Nice

Natanga na njiaa ee natanga na njia nahangaika comments ndefu zinanitesaaa
 
Haujakidhi vigezo maana kuna upande watu wanasimama, na upande mwingine wanakaa kwenye zege kwa hiyo haufai kutumika kama reference. Hivi kuweka viti vya plastiki kwa dunia ya leo ya Mchina ni kwa nini inashindikana? Kiti kimoja cha plastic baada ya mechi mbili tatu kinakuwa gharama zake zimesharudi.
 
Nani mmilliki wa uwanja huu, sio CCM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…