Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 236
Na wakishawakamata wakiwa hai, kwa sheria za nchi yetu watapewa dhamana, na wakishakuwa nje watawahonga polisi na mahakimu na baadae wanarudi kuishi nasi kuendeleza ujambazi wao!hivi kwa nini wanashindwa kuwakamata? Maana kwa kuwkamata wakiwa hai itawasaidia polisi kupata information kutoka kwao na kuendeleza zaidi mapambano dhidi yao
Sheria za Tanzania zinakataza kabisa watu hata polisi kujichukulia sheria mkononi.
hakika polisi hawakupaswa kuwauwa walitakiwa wawakamate wakiwa wazima au hata majeruhi lakini sio kuuwa. Kwani hao walikuwa WATUHUMIA WA UJAMBAZI na wala SIO MAJAMBAZI.
Aliyekuwa na uwezo wa kusema hao ni majambazi ni uamuzi wa mahakama.
Polisi wanavunja sheria.
najiuliza hivi kwanini hata watu binafsi wakimkamata kibaka na kumuuwa polisi hao hao wanafanya uchunguzi na wakigundulika walioshiriki wanawafikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.
Au hata mwizi akija kuvamia nyumba yako na wewe ukamkamata na kumpiga hadi kumuuwa, unashitakiwa kwa kosa la mauaji. Kwanini polisi wasishitakiwe
lazima sheria iangaliwe ili wote wawe na haki sawa mbele ya sheria.
Bihalamuro na si Biharamuro! Kazi nzuri polisi, lakini na wale wezi wakubwa kama akina Jitu Patel na RA fanyeni hivyo hivyo
Wote mmekosa ni Biharamulo
Kama ni habari ya kweli well done Polisi. Hawa sasa hivi ni kuwaua tu
Bihalamuro na si Biharamuro! Kazi nzuri polisi, lakini na wale wezi wakubwa kama akina Jitu Patel na RA fanyeni hivyo hivyo
wawe majambazi kweli basi#
Habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuna majambazi 6 wameuwawa katika mapambano na askari huko buharamuro , majambazi hao walikutwa na silaha kadhaa za kivita inasemekana walikuwa wanajiandaa kuvamia mgodi mmoja wa madini katika eneo hilo .
Bado haijajulikana kama majambazi hao ni wan chi jirani au ni raia wa Tanzania , mpambano huo ulichukuwa dakika chini ya 40 kwa sababu askari hao walikataa amri ya kuwataka kujisalimisha kwa askari
Tutawafahamisha zaidi jinsi tutakavyokuwa tunapata habari zaidi
http://groups.google.com/group/wanabidii/t/2c9d8cd361d55f57?hl=sw