Majambazi Wakenya Walivyotikisa na Kuweka Historia Kanda ya Kaskazini Nchini Tanzania

Majambazi Wakenya Walivyotikisa na Kuweka Historia Kanda ya Kaskazini Nchini Tanzania

INAENDELEA SEHEMU YA MWISHO

Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea Benki ya NMB tawi la Mwanga, mkoani Kilimanjaro, ambalo lilivamiwa na majambazi na kupora zaidi ya Sh. milioni 234, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi kitengo cha Operesheni maalumu, Bw. Venance Tossi, alisema watumishi wa benki kuishi katika ofisi za benki imekuwa ikiwapa ugumu polisi wanaolinda katika benki hizo.

Alisema kutokana na tukio hilo askari waliokuwa wanalinda benki hiyo walishindwa kuwatilia shaka watu waliofika katika benki hiyo wakiwa ndani ya gari na Meneja wa benki hiyo yenye namba za usajili T 524 AED kwa kudhani ni ndugu wa meneja huyo.

Kweli ipo haja ya kuzungumza na wenye mabenki, watumishi wao wasiishi katika benki hizo, alisema.

Tukio hilo liliwapa ugumu askari wetu kutambua watu waliofika na meneja katika benki hiyo kwani ni mara kwa mara ndugu wa watumishi wamekuwa wakifika kwa ajili ya kuwasalimu ndugu zao wanaoishi ghorofa ya pili ya benki hiyo.

'Hatuwezi kukubali hali hii ikaendelea huku lawama kubwa zikiwa kwa Polisi wetu," alisema.

Aidha, kutokana na tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai nchini, Bw. Robert Manumba kwa kushirikiana na makachero wa Polisi wapo wilayani humo wamekuwa wakifanya upelelezi wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo, makachero hao wamefika kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kuwasaka majambazi hayo yaliyokuwa na silaha na kufanikiwa kutoweka na fedha hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Bw. Lucas Ng`hoboko alisema Polisi kwa kushirikiana na raia wema wamefanikiwa kupata gari aina ya Toyota Land Cruiser lililodaiwa kutumika katika tukio?hilo, likiwa limetelekezwa katika kijiji cha Orkoriri kata ya King?ori wilayani Arumeru Mkoani Arusha usiku wa kuamkia Julai 14, mwaka huu.

Alisema gari hilo lilitambuliwa kuwa ni mali ya ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) ambalo liliibwa kwenye ofisi hizo Mkoani Arusha Julai 5, mwaka huu.

Kamanda Ng?hoboko alisema wananchi wa kijiji hicho waliwaarifu polisi kuwa walisikia mlio wa gari majira ya saa 8:00 usiku na mara baada ya kusogea jirani na gari hilo hawakuona mtu aliyekuwepo ndani.

Alisema gari lenye namba za usajili T979 AMY aina ya Toyota Corola 100 ambalo lilikuwa likitumiwa na majambazi wengine wanne, mmoja aliuwawa baada ya kutokea mashambulizi kati ya?polisi waliokuwa doria katika eneo la YMCA na kuharibiwa vibaya na risasi bado halijatambuliwa kuwa ni mali ya nani.

Alisema Polisi wanaendelea na msako mkali wa usiku na mchana ili kuhakikisha wanawakamata watu waliohusika na tukio hilo, huku huduma za kibenki zikiendelea kama kawaida katika benki hiyo, ambapo hadi sasa Meneja wa benki hiyo na Meneja Operesheni wanashikiliwa na polisi kwa upelelezi zaidi.

Tukio la uporaji katika benki hiyo lilijiri Julai 11, mwaka huu, saa 1:15 usiku baada ya kundi la watu sita wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kumteka Meneja wa Benki hiyo, Bw. Robert Marando (56) na familia yake na Meneja Operesheni, Bi. Salome Matemu (54) na familia yake na kuwaamuru kuchukua funguo za chumba maalumu cha kuhifadhia fedha Strong Room na kisha kuchukua fedha na kuwafungia ndani ya chumba hicho.

Aidha, watu hao walimuua kwa risasi askari polisi mwenye namba E6829, PC Michael na kumjeruhi askari mwenye namba F6973 PC Naftali ambao walionesha umahiri katika kupambana na majambazi hayo na kupora silaha zao aina ya SMG zilizokuwa na risasi 60. Hata hivyo, polisi walifanikiwa kuua jambazi mojawapo aliyetambuliwa kwa jina la Peter Ndung?u (37), raia wa Kenya ambaye katika hati yake ya kusafiria ilionyesha aliingia nchini kupitia mpaka wa Namanga Mkoani Arusha mwenzi mmoja kabla ya tukio.

Aidha, katika upekuzi wa gari hilo Polisi walifanikiwa kukamata silaha mbalimbali zikiwemo bastola mbili aina ya Bareta ikiwa na risasi saba na nyingine ya UK ikiwa na risasi nane, zikiwa zimefutwa namba za usajili, risasi 18 zikiwa zimefichwa kwenye soksi, magazini ya SMG yenye risasi 30 na nyingine iliokotwa eneo la tukio ikiwa na risasi 30 na simu ya kiganjani, ambapo kila namba aliyopiga ilionyesha mawasiliano yanaonyesha ni namba za nchini Kenya.

Kutokea kwa tukio hilo kumezua hisia tofauti kwa wananchi wa ndani na nje ya Mkoa wa Kilimanjaro kwani ni miaka mitatu imepita tangu kutokea kwa tukio jingine katika Benki ya NBC tawi la Moshi mnamo Mei 21, 2004, ambapo majambazi walifanikiwa kupora zaidi ya Sh. bilioni 5.3, kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kuporwa katika taasisi za fedha nchini.


Posted Date::7/20/2007
ARUSHA YATIKISIKA😛OLISI100 WAPAMBANA NA MAJAMBAZI

*Risasi zapigwa kwa zaidi ya saa sita
*Wasichana wafichua maficho yao
*Bomu latumika kulipua maficho
Na Mussa Juma, Arusha.


MJI wa Arusha, jana uligeuka uwanja wa mapambano baada ya polisi, wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na vikosi vingine vya ulinzi na usalama, kupambana vikali na watuhumiwa wa ujambazi baada ya kugundua maficho yao. Mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha, walikusanyika katika eneo la Njiro Kontena, kushuhudia tukio hilo, ambalo wengi wanalifananisha na sinema kutokana na kurushiana risasi kwa saa zaidi ya sita kati ya polisi na watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi. Hadi jana jioni, saa kadhaa baada ya watuhumiwa hao wa ujambazi kuzidiwa nguvu na kuamua kujisalimisha, mazungumzo ya tukio hilo yalikuwa yametawala mazungumzo ya watu karibu pembe zote za mji wa Arusha.
Watuhumiwa hao, wanadaiwa kuhusika na wizi wa Sh 234 milioni mali ya Benki ya National Microfinance (NMB) tawi la Mwanga, Kilimanjaro. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Basilio Matei, watuhumiwa hao ni Samweli Gitau Saitoti (33) anayedaiwa kuwa ni Mkikuyu mkazi wa eneo la Ngong Nairobi, ambaye ni dereva wa matatu na Peter Michael Kimenya (40) Mkikuyu mkazi wa Thika Nairobi, ambaye ni dereva wa magari makubwa.

Inadaiwa pia kuwa mmoja wa watuhumiwa hao, Samson Chonjo (26), aliyekamatwa katika tukio tofauti jana, ni miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kuhusika na wizi huo. Watuhumiwa hao waliwapa wakati mgumu polisi tangu saa 8.00 usiku wa kuamkia jana, walipozingira nyumba hiyo hadi saa 5.53 asubuhi, walipoamua kujisalimisha baada ya kurushiana risasi na polisi waliozingira nyumba walimokuwa wamejificha.
Katika tukio hilo, polisi walikamata bunduki mbili aina ya SMG zikiwa na risasi 85, bastola tano zikiwa na magazini nne zenye risasi 30 na majaketi ya kuzuia risasi pamoja na mabomu mbalimbali yaliyokuwa hajalipuliwa. Bado askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wanaendelea na kazi ya kutegua mabomu yaliyokuwa katika nyumba hiyo.
Kamanda Matei alisema majambazi hao walikamatwa na fedha taslimu dola 8,145 za Kimarekani na Sh 978,000 na alimtaja mwingine aliyekamatwa kuwa ni Samson Chonjo (26) mkazi wa eneo la Ngulelo mjini hapa. Alisema Chonjo alikamatwa jana asubuhi katika eneo la Ngulelo baada ya polisi kupata taarifa za wasamaria wema. Kamanda Basilio, alisema maafisa wa Jeshi la Polisi kutoka jijini Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha bado wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao.
"Kama unavyojua leo ndio tumewakamata bado tunawahoji kuhusiana na matukio ya ujambazi na sio la Mwanga pekee," alisema Kamanda Basilio.

Alisema licha ya kuhojiwa kwa watuhumiwa hao, bado Kikosi Maalum ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kinaendelea kutegua mabomu kadhaa yaliyokuwa yametegwa na majambazi hao kutoka Kenya kabla hawajajisalimisha. Ilielezwa kuwa watuhumiwa hao walitega mabomu kuzunguka nyumba hiyo na walikuwa wakirusha risasi mfululizo kwa kutumia bunduki aina ya SMG na bastola, na wakati mwingine wakirusha mabomu ya kutupa kwa mikono. Hata hivyo, jitihada za polisi, viongozi wa serikali, maafisa wa Jeshi la Wananchi na maafisa wa Usalama wa Taifa ambao baadhi yao kwa mara ya kwanza jana walikuwa wamebeba silaha nzito, ilisababisha watuhumiwa hao kujisalimisha majira ya saa 5.53 asubuhi.

Mamia ya watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo, walishangazwa na ujasiri watuhumiwa hao kwa kurushiana risasi na polisi zaidi ya 100 kwa muda mrefu, licha ya kuwapo Kikosi Maalum cha Polisi kutoka Dar es Salaam ambao baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo, watuhumiwa hao walipanda juu ya dari. Maficho ya watuhumiwa hao, waliovalia majaketi ya kuzuia risasi, huku wakiwa wametega mabomu ndani ya nyumba hiyo na nje, yalijgundulika kutokana na makachero wa polisi kunasa namba za simu za wasichana ambao walikuwa wana uhusiano nao kimapenzi.
Akizungumza katika eneo la tukio, akiwa amevaa kifaa cha kuzuia risasi, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kapteni Evance Balama alisema, mara baada ya polisi kuwasiliana na wasichana hao, walitaja eneo walipo na polisi kuamua kuwafuata.

Kapteni Balama alisema baada ya wasichana hao kutambua kuwa wanasakwa na polisi waligoma kutoka katika nyumba hiyo, hadi mama mzazi wa mmoja wa wasichana hao alipotafutwa na kuzungumza na mtoto wake. Alisema baada ya majadiliano kadhaa baina ya mama huyo na mtoto, baadaye watuhumiwa hao waliruhusu wasichana hao kutoka nje ya nyumba hiyo ya kisasa yenye ghorofa moja.
Kwa kiasi kikubwa, kutoka nje kwa wasichana hao, kuliwasaidia polisi kuwajua maadui, hasa walipoelezwa kuwa tayari wametega mabomu nyumba nzima, hivyo wasipotumia busara wanaweza kuangamia.
"Hawa wametupa msaada mkubwa na bado tunawashikilia, tunaamini watatueleza mengi," alisema afisa mmoja wa polisi akiwa na maafisa usalama katika eneo la tukio.

Jitihada za Polisi wa Kikosi Maalum kutoka Dar es Salaam, wakiongozwa na maafisa mbalimbali akiwamo Kamanda Duani Nyanda, zilifanikisha polisi kuingia ndani ya nyumba hiyo, huku wakiwa na wamevalia majaketi ya kuzuia risasi. Hata hivyo, polisi hao walishindwa kukabiliana uso kwa uso na watu hao, kutokana na kupewa taarifa kutoka ngazi za juu za jeshi hilo kuwa watuhumiwa wanatakiwa kukamatwa wakiwa hai ili watoe taarifa zitakazosaidia kuvunja mtandao wao wa ujambazi nchini.
"Hapa tulipo kama tukiamua kumimina risasi lazima tutawaua, ila nasi lazima kutakuwa na vifo, lakini kuna maelekezo kuwa tusiwaue," alisema afisa mmoja wa polisi aliyekuwapo eneo la tukio, saa chache kabla ya watuhumiwa kuamua kujisalimisha.

Baada ya jeuri ya watuhumiwa hao kupiga hovyo zaidi ya risasi 15, polisi waliamua kujibu kwa kupiga makombora ya RPG ambayo yalifanikiwa kubomoa sehemu kubwa ya kuta za nyumba hiyo na wakatupa zaidi ya mabomu 20 ya machozi ndani ya nyumba.
Mapambano yalishika kasi zaidi majira ya saa 3.00 na 4.00 asubuhi, lakini watuhumiwa hao waliendelea kukaidi amri ya kujisalimisha huku wakijibu kwa risasi za rashasha. Hata hivyo, ilipofika majira ya saa 5.00 asubuhi, watuhumiwa hao waliokuwa wakiwasiliana na wasichana wao, waliweza kupiga simu polisi namba 112 na kuomba kujisalimisha kwa masharti kuwa wasiuawe.

Baada ya simu hiyo, maafisa wa polisi wakiongozwa pia na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Arusha (RCO), Chilogile, walikubali na kutoa muda wa kujisalimisha. Kutokana na makubaliano hayo, kwa kutumia kipaza sauti walihesabiwa hadi 10, lakini walikaidi ndipo polisi walipowaonya kuwa, wataishusha nyumba yote kwa mabomu na risasi, hali iliyowafanya kujisalimisha mmoja mmoja, wakiwa wameweka mikono kichwani.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia watu hao wawili, wakiwa chini ya ulinzi wa polisi wakionekana wenye afya nzuri, huku mmoja akiwa mweupe mwenye kipara ambaye polisi kutoka Dar es Salaam walimtambua kuwa alitajwa kuhusika katika uporaji wa Ubungo. Watuhumiwa hao, waliondolewa kwenye jumba hilo majira ya saa 6.00 mchana wakiwa kwenye gari la polisi namba T118 AEN, huku wakisindikizwa kwa ulinzi mkali.
Awali, mamia ya wananchi wa Arusha walitaka kuzuia kuondolewa kwa watu hao wakitaka kuwaua, lakini polisi walifanikiwa kuwatawanya kwa kupiga mabomu ya machozi na kuwasambaza kwa kutumia mbwa. Nyumba hiyo ni mali ya Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Makoye Ngerere, ambaye hivi karibuni alihamishiwa Makao Makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Habari za uchunguzi zimebainisha kuwa watuhumiwa hao, walipanga nyumba hiyo kuanzia Jumapili Julai 17 kwa makubaliano ya kulipa kodi ya Sh 450,000 kwa mwezi, kwa muda wa miezi sita. Hata hivyo, ilielezwa kuwa watuhumiwa hao kuwa, walipata nyumba hiyo kupitia dalali mmoja wa kike (jina linahifadhiwa).
Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Korongoni ambacho ndipo tukio hilo lilitokea, Zulfa Mhina alisema kabla ya kuishi katika nyumba hiyo majambazi hao, alipokea watu kadhaa waliokuwa wanatafuta nyumba. Mhina ambaye nyumba yake inapakana na nyumba walimokuwa majambazi hao, alisema mtu mmoja alifika kwake kutafuta nyumba akidai ana vijana wake wanatoka nje ya nchi.
Hata hivyo, baada ya kuoneshwa nyumba hiyo hakurudi hadi mapema wiki hii alipopata taarifa tayari nyumba hiyo inawapangaji. Alisema taarifa hizo alipewa na aliyekuwa mlinzi wa nyumba hiyo, Hamisi Kironga ambaye aliondolewa mara baada ya majambazi hao kupanga nyumba hiyo.
Hadi jana mchana kikosi cha askari toka jeshi la wananchi(JW) cha kutegua mabomu na maafisa kadhaa wa serikali akiwepo mbunge wa jimbo la Arusha, Felix Mrema walikuwa katika eneo la tukio wakiendelea na ukaguzi wa mabomu. Kamanda wa polisi mkoani hapa, Basilio Matei ambaye alifika kwenye eneo la tukio mchana, alisema kuwa angetoa taarifa majira ya jioni mara baada ya kukusanya taarifa zote muhimu.




MASHAHIDI WADAI MAHAKAMANI WANAMTAMBUA MSHITAKIWA WA 11
13 Apr 2007
By Hellen Mwango
Mashahidi katika kesi ya wizi wa Sh. milioni 168.5 za Benki NBC tawi la Ubungo, Dar es Salaam wameiambia mahakama kuwa wanamtambua mshtakiwa wa 11, Hussein Masoud, kuwa alihusika na wizi, baada ya kumuona siku ya tukio.

Mashahidi hao, Maulid Mpangala (34) na Hezron Aloyce (29), walidai kuwa kwa nyakati tofauti walimuona mshtakiwa huyo ndani ya benki na wenzake wanne wakiwa na bunduki.

Walikuwa wakitoa ushaidi mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bi. Pellagia Khaday.

Wakiongozwa na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bw. Charles Kenyella.

Shahidi Mpangala, alidai kuwa ni mfanyabiashara wa kuku wa nyama na siku ya tukio alikwenda NBC Ubungo kuweka fedha.

Ushahidi wake ulikuwa hivi:Mwendesha Mashtaka: Februari 2, mwaka jana saa 3: 00 asubuhi ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa benki ya NBC tawi la Ubungo.
Mwendesha Mashtaka:Ulikwenda kufanya nini hapo benki?

Shahidi:Nilikwenda kwa lengo la kutuma fedha kwa Kasimu Makia aliyenitumia kuku wa biashara kutoka Singida.

Mwendesha Mashtaka:Ulikuwa na shilingi ngapi?
Shahidi:Nilikuwa na Sh. 850,000.

Mwendesha Mashtaka: Nini kiliendelea baada ya kufika hapo benki, ulifanikiwa kuzituma hizo fedha?

Shahidi: Hapana, kwani wakati nafanya maandalizi ya kuzipanga fedha na kujaza fomu majambazi walivamia na kuniibia.

Wakati niko katika moja ya meza ndani ya benki hiyo, mara niliona watu wanne wakiingia na wakatoa amri kwa sauti laleni chini wote huku wakiwa wameshika bunduki mkononi alidai Mpangala.

Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa baada ya amri hiyo aligeuka kuangalia nyuma na kutaka kujua kuna nini kinaendelea.

Mara mtu mmoja alinifuata na kuninyooshea mtutu wa bunduki akaniuliza, wewe unakaidi kulala chini? Ndipo nikainama juu ya meza na yule jambazi akachukua zile fedha aliendelea kudai.

Aliongeza kuwa alishindwa kufanya chochote kwa vile huyo jambazi alikuwa na bunduki na walitumia kama dakika 10 kukusanya fedha za wateja mbalimbali.

Mwendesha Mashtaka:Unaweza kumtambua huyo aliyekuamuru ulale chini?

Shahidi: Ndio Mheshimiwa.

Shahidi alishuka katika kizimba na kwenda kumgusa mshtakiwa Masoud ambaye ni mshtakiwa wa 11.

Mpangala alidai kuwa anamkumbuka kwa sababu alimfanyia ukatili pale alipomuamuru kwa kumuonyesha mtutu wa bunduki na kumchukulia fedha zake.


WANAOTUHUMIWA KUIIBIA NBC 123m/- WAACHIWA HURU
26 Jan 2007
By Rosemary Mirondo
Washtakiwa wawili kati ya 16 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh. milioni 123 kwa kutumia silaha mali ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jana wameachiwa huru.

Washtakiwa hao walioachiwa huru mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi, Bw. Sivangilwa Mwangesi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ni Mohamed Abbas na Mbaruku Ally. Watuhumiwa hao waliachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kuomba kuwafutia mashtaka chini kifungu 98 (a) cha Mwenendo wa Mashtaka ya Jinai (CPA) kwa kuwa hawana nia ya kuwashtaki.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Charles Kenyella akisaidina na Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Bi. Naima Mwanga na Inspekta wa Polisi, Bw. Raphael Rutaihwa uliomba kubadilisha hati ya mashtaka baada ya washtakiwa hao kuachiwa huru.

ACP Kenyella aliwasomea upya mashtaka washtakiwa waliobakia ambao ni Ramadhan Abraham maarufu kama Dodo, Jackson Mloleni (35), Rahma Gallos (31), Mohamed Abbas (36), Ally Mbaruk (25), Philipo Mushi, Rashid Lembis, Martin Mndasha na John Mndasha. Wengine ni Jackson Salalani, Lucas Nyamaila, Mashaka Pastory na Hussein Masoud.

ACP Kenyella alidai kuwa siku na mahali pasipofahamika washtakiwa hao wanadaiwa kula njama ya unyang'anyi wa kutumia silaha. Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa mnamo Februari 2 mwaka jana, katika benki ya NBC, Tawi la Ubungo, washtakiwa hao kwa pamoja, waliiba Sh. 168,577,275.84, dola 16,128 za Kimarekani na Euro 50 zote zikiwa mali ya benki hiyo, na kabla na baada ya wizi huo waliwatishia watumishi wa benki hiyo kwa kupiga risasi hewani.

Katika shtaka la tatu, ilidaiwa kuwa siku ya tukio la pili eneo la benki hiyo, washtakiwa waliiba Sh. 8,651,250/= kutoka kwa Bw Andrew Athanas. Katika shtaka la nne na tano, ilidaiwa kuwa, washtakiwa hao waliiba Sh. 300,000/= kutoka kwa Bw Hezron Aloyce na Sh. 850,000/= kutoka kwa Bw Maulid Mpangala. Vilevile katika shtaka la sita, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa siku hiyohiyo waliiba Sh. 100,000/= kutoka kwa………


17.11.2006 0132 EAT
MFANYABIASHARA DAR AHUSISHWA MAUAJI, WIZI NBC

Na Grace Michael

MFANYABIASHARA Bw. Hussein Masudi (31) mkazi wa Dar es Salaam amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka matano yakiwemo ya mauaji na wizi wa kutumia silaha katika benki za NBC, NMB, Standard Chartered na duka la kubadilisha fedha la Mc Sons.

Mtuhumiwa alifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashitaka na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Bw. Charles Kenyella mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi, Bw. Sivangilwa Mwangesi.

Mbali na kesi hizo mshitakiwa pia alikabiliwa na kesi nyingine ya dawa za kulevya ambazo anadaiwa kukutwa nazo wakati alipokuwa akipekuliwa nyumbani zenye thamani ya sh. 4,050,000.

Mshitakiwa alisomewa mashitaka ya kesi ya mauaji yaliyotokea Aprili 20, mwaka huu Ubungo Dar es Salaam ambapo mfanyakazi wa NMB, Bw. Ernest Manyoni pamoja na askari namba D.6866, PC Abdallah waliuawa.

Katika kesi hiyo jumla ya washitakiwa 20 wameshafikishwa mahakamani hapo na Bw. Masudi anakuwa mtu wa 21.

Aidha alisomewa kesi nyingine ya mauaji yaliyofanyika Januari 14, mwaka huu katika maeneo ya Kipunguni, Dar es Salaam ambapo anatuhumiwa kumuua Bw. Rajab Jadi. Kesi hiyo ina jumla ya washitakiwa 17 na wengi kati yao, wanakabiliwa na kesi zote tano.

Kesi ya tatu iliyomkabili ni ya wizi wa kutumia silaha katika Benki ya Standard Chartered uliofanyika Machi 6, mwaka huu ambapo jumla ya sh. milioni 300 ziliibiwa. Inadaiwa kuwa kabla ya kufanya tukio hilo, walimtishia kwa silaha Bi. Fortunata Lucas ili kufanikisha wizi huo wa fedha mali ya Kampuni ya Shivacom.

Mshitakiwa aliunganishwa katika kesi ya wizi wa kutumia silaha katika duka la kubadilishia fedha la Mc Sons na kufanya idadi ya washitakiwa katika kesi hiyo kuwa nane ambao wanadaiwa kutenda makosa hayo Septemba 20, mwaka jana ambapo wanadaiwa kuiba jumla ya sh. milioni 150.

Bw. Masudi pia alisomewa mashitaka ya kula njama na kuiba mamilioni ya fedha katika Benki ya NBC Tawi la Ubungo kwa kutumia silaha Februari 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ina jumla ya washitakiwa 13 ambapo upande wa mashitaka uliwasilisha ombi la kukabidhiwa kwa mshitakiwa Bw. Ramadhan Dodo mikononi kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala kwa hatua nyingine ya upelelezi.

Upelelezi wa kesi hizo bado haujakamili na washitakiwa wote wako rumande kutokana na mashitaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana.


UHALIFU: KAMA POLISI WANASHIRIKI WANANCHI WAKIMBILIE WAPI?

Na Lucas Kisasa

Katika gazeti la MZALENDO toleo namba 1810 la Jumapili iliyopita ya Februari 5, mwaka huu ipo barua ya msomaji ambaye hakujitambulisha na ambayo ina ujumbe mzito kwa Jeshi la Polisi kuhusiana na wimbi la ujambazi uliotanda karibu nchi nzima kwa sasa.
Barua hio yenye kichwa cha habari


WAKUU WA POLISI WANAPATA WAPI UTAJIRI WA KUTISHA? HAO NDIO WANASHIRIKIANA NA MAJAMBAZI WAKUBWA kwa muhtasari tu inaainisha yafuatayo:
• Kwamba polisi wanaonekana wameshindwa kudhibiti matukio ya ujambazi.
• Majambazi haya yanayofanya uporaji kwa kutumia silaha yamelelewa na polisi wenyewe wakiongozwa na baadhi ya viongozi wao kwa kuwa na ukaribu kiuhusiano na majambazi hayo.
Utajiri mkubwa wa baadhi ya wakuu wa polisi unatokana na kuwepo kwa matukio ya ujambazi.
Haiwezekani kamwe kwa baadhi ya wakuu wa polisi kuwa na utajiri mkubwa ambao hauwezi hata kuelezeka huku mishahara yao na marupurupu mengine wanayopata yanajulikana.
Itawezekana vipi baadhi ya viongozi hao wa polisi waliopo na hata waliostaafu kuwa na majumba mengi ya kifahari wanayopangisha; kuwa na magari lukuki ya kifahari; kusomesha watoto wao nje kwa mapato yao halali?
Wizi wa magari na uvamizi wa benki unaofanywa na majambazi baadhi ya viongozi wa polisi huwa na habari nao na wanachofanya ni kuweka mazingira mazuri kwa majambazi kutekeleza vitendo vyao viovu bila bughudha.
Kwa ujumla tuhuma hizi dhidi ya Jeshi la Polisi zilizoainishwa na mwananchi huyo katika barua yake hiyo kwenye MZALENDO ni nzito na ambazo haziwezi kupuuzwa hivi hivi.
Kimsingi mwananchi huyo aliyetoa maoni yake kwenye MZALENDO hayuko peke yake. Mazungumzo yaliyotanda katika maeneo mbalimbali nchi nzima kwa sasa iwe kwenye mabaa, vijiwe, maofisini na maeneo mengine, licha ya kuzungumzia ujambazi wenyewe, wananchi wanaonyesha wasiwasi na shaka kubwa kuhusu uwezo na umakini wa Jeshi letu la Polisi katika kupambana na majambazi na kulinda usalama wa raia.
Bila kuumauma maneno, kilichopo sasa ni kwamba kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, wananchi wanaonekana kukosa imani na Jeshi la Polisi, chombo cha dola kilichoundwa makusudi kulinda usalama wa raia.
Kwamba sasa wananchi wanaonekana kutokuwa na imani tena na Jeshi lao la Polisi na kwamba polisi wetu wanawekwa katika kundi moja na majambazi siyo tu ni jambo la hatari bali ni la hatari kweli kweli.
Jambo la kujiuliza ni, kwanini hali hii imetokea? Kifanyike kitu gani kurudisha imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi? Katika kujibu maswali haya mambo kadhaa hayana budi kuainishwa wazi.
Awali ya yote ni muhimu kuweka wazi kuwa baadhi ya vitendo vya polisi ndivyo vinavyowafanya wananchi waanze kukosa imani na Jeshi hilo. Chukulia kwa mfano kilichotokea Machi 26 mwaka 2002 wakati kiasi cha sh. milioni 50 kilipotoweka katika kituo cha polisi cha Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo wizi ulifanyika katika kituo hicho cha polisi na bila shaka wahusika wakuu ni polisi wenyewe na kama aliyefanya uharamia huo ni mtu wa nje, aliweza kufanya hivyo kwa kusaidiwa na polisi.
Sasa basi kama wizi au ujambazi unafanyika katika kituo cha polisi hali itakuwaje katika maeneo mengine ya raia?
Wizi wa zaidi ya dola za kimarekani milioni mbili uliofanyika katika Benki ya Stanbic mwaka 2001 tunaelezwa kuwa baadhi ya polisi nao wanatuhumiwa kuhusika katika kuwalinda wezi kwa kuwapa ulinzi ili wasiweze kukamatwa.
Hii ni mifano miwili tu inayohusisha polisi na matukio ya wizi na ujambazi lakini yapo matukio mengine mengi yanayotokea nchini mwetu kwa sasa na ambayo yanalitia doa kubwa Jeshi letu la Polisi.
Matukio ya rushwa kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani yamekuwa ni jambo la kawaida sasa. Karibu katika nchi nzima, ambapo wakati mwingine wako baadhi ya askari hao huchukua rushwa waziwazi kutoka kwa madereva wa magari mbalimbali yakiwemo ya abiria na hasa daladala.
Ni kweli rushwa haiwagusi polisi peke yao. Rushwa imetanda katika taaluma zote nchini mwetu. Wako waandishi wa habari; wakusanya kodi; madaktari; mabwana afya; mahakimu; na kadhalika ambao baadhi yao ni wala rushwa.
Lakini kinachotisha kuhusu rushwa kwa chombo cha dola kama Jeshi la Polisi ni kuwa wao ambao ni walinzi wa amani, wanapojihusisha na rushwa na ujambazi raia wa kawaida anakuwa hana pa kukimbilia.
Hili ndilo linalowatisha wananchi. Kwamba ikiwa wako baadhi ya polisi wanajihusisha na ujambazi sasa wananchi wakimbilie wapi? Ni kweli Jeshi letu la kulinda usalama wa raia lina matatizo mengi ya msingi kama yale ya mishahara na maslahi duni; uhaba wa nyenzo za kufanyia kazi; na kadhalika, lakini matatizo hayo hayahalalishi baadhi yao kufanya vitendo vya kiharamia. Ukakamavu kwa askari wa Jeshi la Polisi ni jambo la lazima. Uadilifu kwa askari pia ni jambo ambalo halikwepeki.
Je, askari wetu wengi wa Jeshi la Polisi ni wakakamavu? Ni swali ambalo hapana budi polisi wenyewe wajiulize kwanza. Ni dhahiri kuwa askari aliyevimbiana mwili na mwenye kitambi ni nadra kuwa mkakamavu.
Wapo baadhi ya polisi ambao kwa hakika hawana sura ya upolisi bali wanaonekana kama wafanyabiashara au hata mameneja wa "kampuni ya manyoya". Sijui askari ambaye tumbo lake ni kubwa na hata mkanda wake wa suruali hauonekani atawezaje kumdhibiti jambazi kwa kukimbizana naye.
Kama ilivyoainisha barua ya msomaji kwenye MZALENDO mapato ya wafanyakazi wengi wa Serikali wakiwemo polisi yanajulikana. Sasa mtu anaweza kujiuliza polisi huyu mwenye mashamba makubwa makubwa; mwenye daladala lukuki; na mwenye majumba ya fahari mtaji huo ameupata wapi kama siyo rushwa?
Ni kweli kabisa siyo polisi wote wabaya. Wapo polisi wengi tu wazuri na waadilifu katika Jeshi letu, lakini sifa yao nzuri inaharibiwa na polisi wachache na hasa wale wanaoendekeza rushwa na kusaidiana na majambazi.
Moja ya matatizo ya polisi yanaweza kuwa yanatokana na namna ajira inavyofanyika ndani ya Jeshi hilo. Tatizo hili kwa sasa inaelekea halipo lakini ulikuwepo wakati katika miaka michache iliyopita ajira katika Jeshi la Polisi ilikuwa katika misingi ya kujuana tu na siyo kufuata historia ya vijana wanaoajiriwa.
Ndiyo maana wako baadhi ya wananchi walikuwa wakishangaa wanapoona baadhi ya vijana waliovaa sare za polisi ( na ambao tabia zao zinafahamika katika jamii) kwa kuuliza hata huyu naye ni askari polisi?
Hata hivyo hiyo sasa pengine ni historia kwani utaratibu wa ajira sasa kwa Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi umekuwa mgumu zaidi ambapo waajiriwa inabidi wafuatiliwe kwanza katika vijiji wanavyotoka ambavyo ndivyo vinavyowapitisha au kuwaidhinisha.
Kimsingi Jeshi la Polisi katika hali ya sasa hapana budi libadilike. Lifanye hivyo kwanza kwa kubadilika kinadharia na pili kimkakati. Polisi wanapaswa wajipange upya, wajitazame na wajisafishe. Wakishindwa kufanya hivyo basi wapangwe upya na kusafishwa.
Kwamba majambazi yanadiriki kupora kwenye mabenki kwa kutumia karibu robo saa katika uporaji (kama ilivyofanyika katika tukio la ujambazi kwenye Benki ya NBC tawi la Ubungo, jijini Dar es Salaam) na kupiga risasi hewani bila kuingiliwa na polisi ni jambo linaloleta maswali mengi vichwani mwa wananchi.
Ni vigumu kuweza kusema kuwa ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa katika kuirekebisha hali hii. Hata hivyo, jambo moja ni wazi nalo ni kwamba, wananchi hawako tayari kuona hali hii ya utendaji mbovu wa Jeshi la Polisi ikiendelea. Mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi ni ya lazima.

Simu: 0744-309858
E.mail: kisasa2000@yahoo.com

TUZO KWA MASHUJAA WA UJAMBAZI UBUNGO SAWA,LAKINI?

2006-04-29 10:19:19
Na Badru Kimwaga
Tukio la ujambazi la aina yake lililotokea hivi karibuni katika makutano ya barabara za Mandela,Sam Nujoma na Morogoro pale Ubungo jijini Dar es Salaam ni dalili za wazi kuwa, vita dhidi ya ujambazi bado ni ngumu.

Kwa namna yoyote ile, zinahitajika juhudi, maarifa na mikakati ya hali ya juu, tena basi ya muda mrefu katika kuhakikisha kuwa matukio ya aina hiyo yanapunguzwa na kudhibitiwa kabisa hata kuwafanya raia kuishi kwa amani na utulivu ikiwa pamoja na kushiriki bila uoga kwenye shughuli za kujiletea maendeleo yao.

Katika tukio hilo, lililotokea mchana kweupee wakati magari mawili ya Benki ya NMB yalikuwa yakisafirisha zaidi ya sh bilioni moja kuzipeleka mkoani Morogoro yalimiminiwa risasi na majambazi ambayo yalikuwa yamejiandaa vilivyo kukabili aina yoyote ya upinzani ambao ungefanikisha kuzuia azma yao.

Hata hivyo, yalifanikiwa kupora sh milioni 150 na kubakisha sh milioni 850 katika makasha kadhaa yaliyohifadhi fedha hizo.

Yasemekana kuwa, kwa juhudi binafsi au mapenzi kwa maisha ya watu na jeshi lake, trafiki polisi mmoja alijitolea mhanga kutafuta bunduki kutoka kule alikoipata na kisha kujibanza katika eneo aliloamini kuwa anaweza kupata shabaha na kuanza kuwafyatulia risasi majambazi hayo, ambayo yaliingiwa na kiwewe hata kushindwa kubeba zigo lote la fedha, baada ya kubaini kuwa maisha yao yapo hatarini. Wakati wa purukushani hiyo, iliyosababisha kizaazaa kikubwa na mkanganyiko wa hali ya juu kwa raia na makamanda wa majeshi mbalimbali waliokuwa katika pilikapilika zao za maisha muda huo, walishuhudia risasi za moto zikirindima bila ya huruma au udhibiti wa aina yoyote ile.

Kwa hakika, ziliponyamaza ilishuhudiwa maiti mbili za askari aliyekuwa akisindikiza fedha hizo, kwenda Morogoro na mfanyakazi wa benki hiyo wakiwa maiti huku wamelowa damu.

Halikadhalika watu kadhaa walijeruhiwa kwa risasi wakiwa wanapita njia au katika mhamaniko huo mkubwa na wa aina yake kutokea.

Maarifa na juhudi zaidi zinatakiwa ili kujipanga upya kuyakabili majambazi, kutokana na namna mbinu za kivita zilivyotumika kufanikisha wizi huo toka Ubungo hadi Tabata Relini,Tazara na kurudi hadi jalalani na kisha barabara ya Pugu na hatimaye Kurasini, ni ishara tosha kuwa watu hawa walikuwa wameiva katika medani za kivita hasa katika namna ya kuwakwepa adui huku wakiwa na fedha zao na majeruhi wao.

Jeshi la polisi linastahili pongezi kwa namna lilivyojitokeza haraka na kutumia juhudi na maarifa kujaribu kwenda sambamba na majambazi hayo, hata kuyatia kiwewe ambacho hakijawahi kuonekana wakati wowote kabla ya hapo.

Kwa kutumia helkopta iliyokuwa ikirandaranda angani kusaidia kufanikisha udhibiti na kuwachungulia kwa chini majambazi au watu wote waliokuwa katika nyendo zisizoeleweka.

Lilikuwa ni tukio jipya na la aina yake katika masuala ya ulinzi na usalama hapa nchini lililofanyika kwa dakika kadhaa kwenye anga la Dar es Salaam. Kabla ya hapo, ilizoeleka polisi wanapopewa taarifa kukawia kufika katika maeneo ya matukio kwa kutoa visingizo hivi na vile. Kwa namna yoyote ile, hatua hiyo ya kufika mapema na kuonyesha namna gani wanajituma ni kwamba inatia moyo na inafaa kuendelezwa.

Mhe Rais Jakaya Kikwete alipopata fursa, alienda katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kuwajulia hali majeruhi waliotokana na tukio hilo. Baada ya kutafakari kwa kina, Rais Kikwete aliahidi kuwa serikali itawasomesha watoto watatu wa askari polisi aliyekufa katika tukio hilo Koplo Abdallah Marwa,hadi kufikia kiwango ambacho wao wenyewe wataona kuwa inatosha.

Halikadhalika alilitaka jeshi la polisi kuwapandisha vyeo polisi waliojeruhiwa katika tukio hilo, kama njia ya kutambua na kuthamini michango yao ya kujitolea mhanga kukabili rabsha za majambazi, ambayo yalionyesha kwamba hayakuwa na chembe ya huruma kwa watu.
Wengine waliojeruhiwa katika tukio hilo ni stafu sajenti Wallace Mmuni na Koplo Adimu Kilowoko.

Rais alisema kuwa tukio hilo limemsikitisha sana kwa sababu mbili muhimu, kwanza ni ya wizi wenyewe na pili ni aina ya ukatili uliotumika katika kufanikisha kiu yao ya kutaka fedha nyingi kwa kutumia njia za mkato, yaani kulimiminia gari risasi nyingi mfululizo. Akimuelezea askari aliyekufa katika tukio hilo alisema kuwa?amekufa kishujaa na kumuombea kwa Mungu ili apokelewe pema peponi na kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya majambazi yataendelea na hayataachwa yatambe yapendavyo.

'Yule trafiki namwagiza IGP ampandishe cheo na askari wengine wote walioshiriki katika mapambano yale pia wapandishwe vyeo?' alisema.

Rais ambaye alizungumza huku akionesha kuguswa na tukio hilo kwa namna ya uchungu mkubwa, alionyesha namna gani anavyothamini maisha ya watu yaliyopotea bila ya hatia yoyote ile, huku baadhi ya watu wakijeruhiwa kwa sababu ya uroho wa mali. Siku chache baada ya rais kutoa tamko hilo, la kuwataka majeruhi waliojitoa mhanga kukabili wimbi lile la ujambazi ikiwa pamoja na trafiki yule wapandishwe vyeo, IGP Said Mwema aliitikia amri hiyo ya amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kuwapandisha vyeo.

Vyeo walivyopandishwa askari hao ni vya ngazi moja moja tu, yaani kwa aliyekuwa praiveti anakuwa koplo na kuendelea. Kwa hakika tuzo ni tuzo.

Lakini katika mazingira ya tukio lile, ambalo watu walijitoa mhanga na kuonyesha uzalendo wa hali ya juu, ni kwamba walitakiwa kuthaminiwa hasa kwa kupewa vyeo angalu vya ngazi tatu au hata nne na kisha kupewa fursa ya upendeleao kwa kupelekewa vyuoni haraka msimu ujao ili kwamba vyeo vyao vilingane na elimu yao.

Haifahamiki mara moja kwa nini sisi watanzania kweli tunakuwa wanyimi wa kutoa vyeo, hata kwa watu waliofanya matukio yaliyotukuka kama hayo kwa namna ya kipekee.

Hebu fikiria kama majambazi yale yasingesikia bunduki zikikohoa na kutishia usalama wao, unadhani wasingefanikiwa kubeba zigo lote la fedha la sh bilioni moja??

Kwa namna yoyote ile, dhamira ya majambazi hayo kuteka magari hayo ni kupora fedha zote na ikibidi kuua watu wote ambao wangeonyesha nia hasa ya kuwazuia kutimiza azma yao hiyo.

Na isitoshe yawezekana majambazi yale, ambayo kwa mujibu wa ripoti ya kamanda wa polisi wa kanda maalum Alfred Tibaigana ni kwamba yaliacha risasi zipatazo 75 hivi na bunduki ikiwemo revolver na nyinginezo, ni kwamba yangeweza kuua watu wengi zaidi na taifa kuingia katika msiba mkubwa wa kusaga meno.

Sasa basi, mtu anapojitolea maisha yake na kunusuru maisha ya watu wengi na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kama hicho halafu anaambulia ngazi moja tu ya cheo chake. Swali dogo la kujiuliza jamani kweli tunathamini hasa alichokifanya??

Kutunikiwa cheo ni hatua nzuri.Lakini inawezekana cheo hicho angekipata wakati wowote, pindi mkuu wa majeshi angeyapitia mafaili ya askari wote, mara baada ya kuingia madarakani na kwamba kilikuwa kimekawia tu njiani kumfikia.

Lakini kama angeongezewa vyeo kwa ngazi mbili au tatu hivi ,ni ishara tosha kuwa kweli ametunukiwa na maisha yake yakabadilika kabisa, hata kuwa mfano kwa watu wengine na askari wenzake kwamba, kama utafanya jambo zuri la kujitoa mhanga ni kwamba taifa litathamini unachokifanya.

Lakini kwa askari au watu wengine unadhani kwa kuona tuzo kama hiyo, kweli itawahamasisha kujitolea mhanga katika mazingira ya hatari kama yale??

Ni vyema sana suala la kupandishwa vyeo, hasa kwa yule trafiki likaangaliwa upya kama tunataka kuona watu wananufaika hasa na kujitoa kwao mhanga.

Mungu ibariki nchi yetu na watu wanajitolea mhanga kama trafiki yule wa Ubungo.


VINARA WA UPORAJI UBUNGO WATAJWA

2006-05-01 16:50:16
Na Adam Fungamwango, Jijini
Watu kadhaa ambao wanashukiwa kuwa vinara waliohusika kuchonga dili nzima iliyosababishwa kuporwa kwa mamilioni ya pesa za benki ya NMB wametajwa kwa majina.

Hatua hiyo ambayo ni muhimu katika upelelezi wa sakata hilo la aina yake, imefikiwa baada ya jambazi mmoja kudakwa na kisha kubanwa hadi 'kufanya usaliti'.

Taarifa za kipolisi zinasema jambazi huyo aliyewataja wenzake ameuawa katika majibishano ya risasi na polisi mkoani Arusha.

Jambazi huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Frank Lyatuu 31, ambaye inasemekana alikiri kabisa kuhusika na wizi huo.

Alitwangwa risasi wakati alipochomoa bunduki yake aliyokuwa ameficha sehemu za siri na kuanza kuwamiminia risasi polisi.

Wakati hayo yakitendeka, jambazi huyo alikuwa akiwapeleka polisi mafichoni kwao ambako huwa wanaficha silaha.

Polisi mkoani Arusha wamesema walimkamata jambazi huyo Ijumaa iliyopita eneo la kwa Idd kwenye gereji moja na baada ya kumhoji akakiri kuhusika kabisa na matukio mbalimbali ya ujambazi likiwemo lile la kwenye mataa ya Ubungo.

Katika sakata hilo, polisi wanasema kuwa wakati anasindikizwa na askari ili akawaonyeshe 'ghala' lao la silaha, ghafla kama vile makomandoo na 'mastelingi' wa sinema za kibabe wanavyochomoka maadui zao baada ya kutekwa, alichomoka na kuanza kutimua mbio, huku akimimina risasi.

Polisi wanasema alianza kufyatua risasi kwa nia ya kuwatisha askari ili kujinusuru, lakini maaskari shujaa walifanikiwa kumlamba shaba iliyomdondosha chini na alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali na mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa wa Arusha Mount Meru.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha Matei Busilo, amesema majambazi yaliyotajwa mengi yalichomewa utambi na marehemu Lyatuu ambapo baada ya kumbana kisawasawa aliwataja wenzake ambao alishirikiana nao kwenye ujambazi huo.

Waliotajwa ni pamoja na Allen Charles Urio, a.k.a Katengo ambapo huyu ametajwa kuwa ni jambazi hatari, kwani ndiyo kiongozi wa majambazi katika Nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Katengo ambaye yeye alikamatwa hivi karibuni, inadaiwa kuwa yeye ndiye kiongozi wa majambazi wote katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

Jambazi mwingine aliyetajwa ni Richard Paul, ambaye imedaiwa kuwa ni rafiki wa karibu na Bw Justine Nyari ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka thelathini jela.

Mwingine aliyetajwa kushiriki katika uporaji huo ni Phillipo Charles ambaye ni maarufu kwa jina la Mpolee, Ramadhani Abraham a.k.a Dodo na Frank Mromboo.

Mwingine aliyetajwa ni Wycliff Lumumba na Allen Urio ambao inadaiwa wameshatoroka gerezani nchini Kenya walikokuwa wamekamatwa.

Katika tukio la Ubungo, jumla ya shilingi milioni 150 ziliporwa. Watu wawili akiwemo askari walipoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa

WATATU WAKAMATWA WIZI NMB UBUNGO

Written by Maxence M. Melo
Wednesday, 26 April 2006
Na: Esther Mvungi

Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkaoni Dar es Salaam wakituhumiwa kuhusika na uporaji wa mamilioni ya shilingi, mali ya benki ya NMB, uliotokea Alhamisi iliyopita, eneo la Ubungo, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, alisema kutokana na ukubwa wa suala hilo, si vyema kwa sasa kuwataja majina watuhumiwa hao.
"Suala ni kubwa na lina mtandao mkubwa… uchunguzi bado unahitajika, si busara kusema wapi wamekamatwa na ni kwa vipi wanahusika na tukio hilo," alisema Tibaigana.
Alisema sh. 800,000 zimepatikana kati ya sh. milioni 150 zilizoporwa na majambazi hayo yaliyokuwa yakitumia silaha na kusababisha mauaji ya watu wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa. Jitihada za polisi ziliwezesha kusalimisha sh. milioni 850.
Waliouawa kwa kupigwa risasi katika uporaji huo ni Konstebo wa Polisi Abdallah Marwa na mfanyakazi wa NMB, tawi la Wami, Morogoro, Everest Manyonyi.
Polisi wengine watatu, Sajini Taji Wales Mmuni, askari Venance Mligo na Koplo Adimu Kilowoko waliokuwa wakisindikiza fedha hizo wakiwa katika magari yenye namba za usajili SU 34390 na SU 36177, walijeruhiwa kwa risasi na wamelazwa Muhimbili. Raia wanne pia walijeruhiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi iliyopita, Tibaigana alisema bunduki tatu aina ya SMG, zikiwa na magazini tano na risasi 75, bastola mbili na risasi 13 zilikutwa kwenye gari lenye namba za usajili T 761 AHG, Toyota Corolla Limited, lililotelekezwa barabara ya Kilwa, karibu na kambi ya Jeshi ya Twalipo. Alisema bostola nyingine mbili zilipatikana eneo la tukio Ubungo.
Katika hatua nyingine, Kamanda Tibaigana amevitaka vyombo vya habari kuwa na subira na kuandika taarifa ambazo zinatolewa na Jeshi la Polisi.
Alisema taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na vyombo vya habari kuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanahusika katika tukio hilo la uporaji si za kweli.


STELINGI' WA WIZI UBUNGO ANASWA
NI MKENYA, ASIMAMISHWA KISUTU
ANAUNGANISHWA NA WENZAKE 17

na Asha Bani
RAIA wa Kenya, anayedaiwa kuwa jambazi sugu, ametiwa mbaroni, akituhumiwa kuhusika na tukio la mauaji na uporaji wa fedha katika Benki ya NMB, katika tukio lililotokea Ubungo, Dar es Salaam. Alikamatwa nchini Kenya wiki mbili zilizopita. Jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mtuhumiwa huyo, Wilcliff Imbova (26), maarufu kwa jina la ‘Wikii' ameunganishwa na watuhumiwa wengine 17, kujibu tuhuma za mauaji na uporaji. Imbova anadaiwa kuwa ndiye kinara aliyeongoza mauaji na uporaji huo uliotikisa nchi. Polisi waliomkagua walidai kwamba ana majeraha ya risasi mgongoni.

Inadaiwa kwamba mtuhumiwa alijeruhiwa Ubungo wakati akirushiana risasi na polisi. Mbele ya Hakimu Mkazi, Michael Lugulu, Mwendesha Mashitaka, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Charles Kenyela, alidai kwamba Imbova na wenzake, walimuua; mfanyakazi wa NMB, Ernest Manyonyi; na polisi, D. 6866, Konstebo Abdallah.

Katika shitaka la pili, mtuhumiwa huyo na wenzake wanadaiwa kupora sh milioni 150, mali ya Benki ya NMB, ambazo zilikuwa zikipelekwa Morogoro. Wanadaiwa kutenda uhalifu huo Aprili, 20, mwaka huu saa 6:30 mchana katika makutano ya barabara ya Morogoro, Sam Nujoma na Mandela; eneo la Ubungo, Dar es Salaam.

Watuhumiwa wengine ni pamoja na askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), MT. 76162 Emmanuel Lamel na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT. 77754 Nazareti Amurike.

Wengine ni Mashaka Pastori Paulo Mahengi au Uhuru (28), Rashid Embres au Ramaa (26), John Mndasha (32), Martin Mndasha au Kijazi (24) na Philipo Mushi au Mpolee (27), Jackson Issawangu au Mangea (37), Lucas Aloyce au Nyamaila (37), Haji Hamis Kweru (47), Juma Athumani Nyundo (44); dereva wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Ally Omary Lumi Lumbi (46); na Dereva wa NMB Kanda ya Wami, Yassin Juma (27).

Wengine ni Hamis Mjaka (41); Peter Mjata (44); mfanyakazi wa NMB Tawi la Bank House, Musa Zuberi Mustafa (33); na mhudumu wa ofisi za NMB Tawi la Morogoro, Simon Ephata Kaaya (43). Kesi hiyo itatajwa tena Julai 28, mwaka huu.



ILIKUWA PIGA UA UBUNGO

2006-04-21 15:58:33
Na Job Ndomba, Ubungo
Eneo la mataa ya Ubungo jana mchana liligeuka kama uwanja wa vita wakati majambazi yenye silaha kali yalipokuwa yakifanya uporaji ilikuwa ni piga ua risasi zilimiminwa, watu wakauawa na damu kumwagika barabarani kama maji ya bomba.

Tukio hilo lililoonekana kama moja ya sinema za wakali wa Hollywood wa kule Marekani, lilitokea saa 6:30 mchana.

Wakati tukio hilo linatokea, eneo hilo la Ubungo, kama kawaida lilikuwa na watu kibao waliokuwa kwenye pilika pilika zao za kusaka maisha, wengine wakiwa vituo vya daladala wakisubiri mabasi yaendayo maeneo ya Mwenge, Chuo Kikuu, Manzese, Kimara na Buguruni.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo pale Ubungo, wamesema wakiwa hawana hili wala lile, waliona gari moja aina ya Toyota Corolla likiwa na mijibaba iliyoshiba ikiwa imetulia jirani na yanapopaki magari makubwa pale Ubungo jirani na kituo cha mafuta cha Toico.

'Hatukuweza kulitilia mashaka gari hilo tukiamini ni askari wanaovaa kiraia wameamua kutega mingo yao hapo...kwani hata askari siku hizi wanatumia gari lolote,' akasema shuhuda mmoja.

Ghafla baada ya dakika 15 hivi, ndipo mchezo ulipoanza kuonekana kwani tuliona gari hilo likitoka kwa kasi sehemu lilipokuwa limepaki huku gari jingine aina ya Pick up Hard Top, likiwa na watu kama saba hivi wakiwa wamevaa silaha nzito shingoni wakichomoza.

'Kufumba na kufumbua tuliona magari mawili Toyota Land Cruiser mali ya benki ya NMB yakianza kushambuliwa kwa risasi mfululizo,' akasema shuhuda mwingine.

Mashuhuda hao wanasema, gari la kwanza lenye namba za usajili SU 36177 lilivamiwa wakati linajiandaa kukunja kona ya kutoka barabara ya Sam Nujoma kuingia barabara ya Morogoro kuelekea Kimara.

Ghafla watu hao waliokuwa katika gari la wazi walilirushia mvua ya risasi na kumfanya dereva apoteze mwelekeo na kulivaa gari aina ya Benzi lenye namba T 760 AAW.

Hata hivyo, gari jingine mali ya benki hiyo lenye namba SU 34390 ambalo ndilo lilikuwa limebeba 'mzigo' wa fedha likiwa na FFU wanne na afisa wa benki hiyo kutoka Wami Morogoro, walishuhudia wenzao wakichakazwa kwa risasi, hali iliyowafanya watake kupitiliza kwenda njia ya Buguruni.

Bahati haikuwa yao, kwani majambazi yale yalilenga risasi kwenye tairi na kufanya lipoteze mwelekeo na kugonga nguzo za kuongozea magari, na hapo ndipo roho za ukatili za yale majambazi zilipoonekana.

'Heri wale waliokuwa katika gari la kwanza, lakini hawa wa humu walichakazwa kwa risasi mfululizo na kuliharibu gari lote hadi likaonekana kama la zamani, kisha majambazi hayo yakavuta makasha mawili ya pesa huku jambazi mmoja aliyeonekana na usongo akichakaza risasi bila huruma,'akasema shuhuda huyo.

Wakati 'mchezo huo mchafu' uliodumu kwa takribani dakika 15 hivi unafanyika, askari mmoja wa kikosi cha usalama barabarani, Solomon Adam, aliyekuwa akiongoza magari hapo, alishuhudia unyama huo na kuamua kutimua mbio kuelekea kituo kidogo cha polisi kilichopo Ubungo Terminal.

'Wengi walidhani anajisalimisha kuogopa kuuawa, lakini kumbe alikuwa shujaa wa tukio hilo...yaani baada ya kufika kituoni hapo alitoa taarifa kwa polisi wenzake na kisha kuchukua silaha na kurejea eneo la mapambano,'akasema mtu mwingine aliyeshuhudia tukio hilo.

Akizungumza na Alasiri huku akionekana kutooamini kile kilichotokea, Koplo Solomon, akasema aliwahi kuchukua silaha kituoni ili aweze kupambana na majambazi hayo yaliyokuwa na silaha nzito huku yakichakaza ovyo risasi.

'Nilijificha huku nikirusha risasi za mapigo, lakini mijambazi ile ikaniona na kunirushia risasi, nikafanikiwa kuiona na kujitupa katika mtaro, ile risasi ikampata mpita njia mguuni,' akasema Koplo Solo.

Huku akiwa amechafuka na mavazi yake meupe yakiwa hayatamaniki, Koplo Solomon, akasema juhudi zake hata hivyo inawezekana ndizo zilizosaidia majambazi hao kushindwa kuondoka na maboksi mengine mawili ya chuma yaliyokuwa na pesa nyingi zaidi.

Katika tukio hilo, mijambazi hiyo ilifanikiwa kukomba makasha mawili yaliyokuwa na jumla ya Sh.milioni 150 huku kiasi cha Sh.milioni 850 zote zikiwa zinasafirishwa kule tawi la NMB Wami Morogoro, zikiokolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutokea tukio hilo, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, alisema akiwa safarini kuelekea mkoani Morogoro, ghafla alipigiwa simu ya kufahamishwa kutokea kwa tukio la ujambazi katika kanda yake.

'Nilimwamuru dereva ageuze gari na kurejea Dar...nilipofika Ubungo nilishuhudia jinsi hali ilivyokuwa mbaya, lakini vijana wangu wamefanya kazi nzuri na kuyapata magari matano waliyotumia majambazi hayo na silaha sita,' akasema Tibaigana.

Akasema, majambazi hao wanaonekana wazoefu, kwa kuwa waliwazuga polisi kwa kutumia magari matano tofauti kuanzia eneo la tukio ambapo walikuwa na Corolla T 533 AAB.
Gari hilo katika karatasi za bima likionyesha namba T 440 AJL.

Kamanda Tibaigana akasema magari mengine ni T 848 AHF (Toyota Surf) lililokuwa barabara ya Nyerere, T561 AHG (Corolla likiachwa Banda la Ngozi) na T761 AHG Toyota Limited likiwa karibu na kambi ya Twalipo Mgulani.

Katika gari hilo la mwisho, Kamanda Tibaigana amesema polisi walikuta SMG tatu zikiwa na risasi 75 na magazine 5, bastola moja (chinese) na risasi 15 na magazine moja. Katika eneo la tukio alisema zilipatikana silaha mbili bastola na rivolva moja. Leo asubuhi, Kamanda Tibaigana ameliambia gazeti hili kuwa ni mapema kueleza hatua walizofikia hadi sasa kusaka majambazi hayo



03.05.2006 09:56
HATIMAYE POLISI YAANIKA 'MAJAMBAZI' WA UBUNGO

*Wamo askari watatu wa JWTZ, raia saba
*Yathibitika bunduki zilizotumiwa ni za kivita
*Bunduki aina ya LMG bado haijapatikana
*Ziliibwa kutoka kambi moja ya Jeshi Dar

Na Mwandishi Wetu

JESHI la Polisi 'limewaanika' watuhumiwa 10 wakiwamo askari watatu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa tuhuma za kuhusika na tukio la uporaji wa fedha za NMB lililotokea Ubungo, Dar es Salaam, mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Polisi Makao Makuu, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishina wa Polisi Robert Manumba, alisema miongoni mwa watuhumiwa hao ni wafanyakazi wanne wa NMB wakiwamo madereva wawili wa magari yaliyovamiwa katika tukio hilo. DCI Manumba aliwataja watuhumiwa askari kuwa ni MT.77754 Praiveti Nazareth Amulike (31) mkazi wa Kurasini Shimo la Udongo, Dar es Salaam, MT 18568 Sajini Taji Mathew Pallangyo (50) mkazi wa Ubungo ambaye amelazwa katika Hospitali ya JWTZ kambi ya Lugalo, Dar es Salaam.

Askari mwingine ni MT 76162 Koplo Usu Emmanuel Harisson (32) mkazi wa Sinza.

Watuhumiwa ambao ni wafanyakazi wa NMB, ni Bw. Juma Nyundo (45) ambaye ni dereva, mkazi wa Ubungo na Bw. Ally Lumbilumbi (46) dereva wa NMB tawi la Morogoro.

Wafanyakazi wengine wa NMB wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi huo ni Peter Mjata (44), Mdhibiti wa Fedha NMB Bank House, mkazi wa Magomeni na Simon Kaaya (43) tarishi wa NMB tawi la Wami Morogoro, mkazi wa Rokangazi Morogoro.

Wengine ni wafanyabiashara, Bw.Yassin Juma (47) ambaye ni mkazi wa Magomeni, Kagera, Bw. Hamis Mjaka (44) mkazi wa Mwanakwerekwe, Zanzibar na Bw. Juma Memba au Mustafa (33) ambaye ni mkulima mkazi wa Mbweni JKT.

Kamishna Manumba alisema tukio hilo lilikuwa kubwa zaidi likilinganishwa na matukio mengine ya ujambazi yaliyowahi kutokea nchini.

"Nasema ni tukio kubwa, kwa sababu ya mazingira yake yalivyotokea na silaha zilizotumika pale zilikuwa ni za kivita ikiwa ni pamoja na SMG na LMG ambayo hadi leo hatujafanikiwa kuipata, lakini walioshuhudia tukio wanasema ilitumika," alisema.

Awali akielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea, DCI Manumba alisema ilikuwa Aprili 20 mwaka huu saa 6.30 mchana, ambapo magari mawili ya NMB yaliyokuwa yakisafirisha sh. bilioni moja kuzipeleka kwenye tawi la NMB Wami mkoani Morogoro.

DCI Manumba alisema katika msafara huo, lilitangulia gari namba SU 34390 Toyota Land Cruiser, likiwa na fedha zote, likiendeshwa na Bw. Lumbilumbi ambapo kwenye kiti cha mbele alikaa karani wa NMB tawi la Wami Bw. Ernest Manyonyi na polisi wawili D.6866 Koplo Adim na D.6861 Konstebo Abdallah.

Alisema katika gari la pili namba SU 36177 lililokuwa likiendeshwa na Juma Nyundo lilibeba vifaa vya ofisini na polisi namba C.2199 Meja Wales na E. 9784 Konstebo Venance ambapo askari wote walikuwa na silaha aina ya SMG.

DCI Manumba alisema msafara huo ulianza safari kuelea Morogoro lakini ilipofika saa 6.30 mchana, ukiwa katika eneo la Ubungo kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Nelson Mandela walivamiwa na majambazi ambao wanakadiriwa idadi yao kufikia 10.

"Mara baada ya kufika katika eneo hilo, ghafla msafara ulizuiwa kwa mbele na gari aina ya pick up nyeupe, ambapo majambazi karibu wote walikuwa na silaha na walianza kuwashambulia kwa kasi, kiasi kwamba askari waliokuwa wanasindikiza msafara huo, hawakupata nafasi ya kujibu mashambulizi hayo," alisema DCI.

Alisema katika mashambulizi hayo, Konstebo Abdallah na Bw. Manyonyi ambao walikuwa katika gari la mbele waliuawa, na majambazi kupora makasha mawili yaliyokuwa na sh. milioni 150.

Wakati majambazi wakiendelea kupora fedha, polisi wa kikosi cha usalama wa barabarani, Koplo Solomon Adam aliyekuwa anaongoza magari katika eneo hilo, alifanikiwa kuchukua bunduki moja kutoka kwa askari waliojeruhiwa na kuwashambulia majambazi hao huku akifanya mawasiliano na polisi wengine.

DCI Manumba alisema majambazi baada ya kuona wanashambuliwa waliondoka katika eneo hilo na kuacha sh. milioni 850 zikiwa ndani ya makasha mawili, hata hivyo pamoja na kupora sh. milioni 150, pia walipora na bunduki moja ya Polisi ambayo ilikuwa na magazini mbili zenye risasi 60.

Alisema katika eneo la tukio, zilipatikana bastola mbili na risasi 20, askari watatu waliokuwa kwenye msafara pamoja na raia sita, akiwamo dereva Nyundo ambapo waliobaki walikuwa ni wapita njia. Hata hivyo majeruhi wote hali zao zimeripotiwa kuendelea vizuri.

DCI alisema mara baada ya tukio, polisi waliendesha msako mkali kwa kutumia magari na helikopta ya Polisi lakini majambazi walitokomea kwa mtindo wa kuteka na kubadilisha kwa nyakati fofauti, kisha kuyatelekeza katika maeneo tofauti.

Aliyataja magari yaliyotekwa na kutelekezwa kuwa ni namba T 848 AHF Toyota Surf lililokuwa likiendeshwa na Doto Ally (32) ambalo lilitekwa Tabata Matumbi na kutelekezwa Ilala Good Shed barabara ya Nyerere.

Lingine ni namba T761AHG Toyota Corolla, lililokuwa linaendeshwa na Bw. Said Dafi walilolipora katika barabara ya Nyerere na kulitelekeza karibu na Bwalo la Maofisa wa Kambi ya JWTZ Mgulani Twalipo.

Alisema ndani ya gari hilo, lilipopekuliwa na polisi lilikutwa na silaha tatu aina ya SMG na risasi 75 na bastola moja.

Gari Namba T34 ALY, Toyota Rav4 lililokuwa likiendeshwa na Bw. Daniel Michael liliporwa eneo la Tabata Relini karibu na Chuo cha St. Mary's na kutelekezwa katika eneo la Kipunguni A karibu na kambi ya JWTZ Airwing.

Alisema mafanikio ya polisi kukamata watuhumiwa hao yanatokana na ushirikiano mkubwa, uliotolewa na wananchi ambapo alisisitiza kuwa walionesha uzalendo wa aina yake kwa kupiga simu na wengine kuandika na kuweka taarifa zao kwenye makasha ya maoni Polisi. Alisema polisi waliandaa gwaride maalum la kuwatambua watuhumiwa wa ujambazi huo ambapo raia waliokuwa eneo la tukio na askari waliwatambua watano kati ya 10 wanaotuhumiwa wawili kati yao ni hao askari wa JWTZ.

"Hata hivyo kukamatwa kwa askari wa JWTZ kusilihusishe Jeshi hilo, kwa sababu hata kwenye taasisi zetu nyingine wapo wabovu, lakini si taasisi zenyewe ni kama vile Mtanzania yeyote anavyoweza kufanya uhalifu, lakini si vyema kuwahusisha Watanzania wote," alisema DCI Manumba.

Alisema Jeshi la Polisi litaendelea kusaka wengine waliohusika katika tukio hilo na kuahidi kuwa litashirikiana kwa karibu zaidi na raia wakiamini kwamba ndiyo silaha yao kuu.

"Hapa ninapenda kusisitiza, kwamba Jeshi letu linahitaji ushirikiano wa karibu zaidi na raia katika kukomesha uhalifu, tutaendelea kuwaficha watoa taarifa wetu na tunawahakikishia usalama wao," alisema DCI Manumba.

Akizungumzia kutotumiwa kwa magari maalumu ya kusafirishia fedha ambayo yanaaminika kuwa na uwezo wa kuzuia risasi, DCI alisema hali hiyo inatokana na historia ya nchi yetu.

Alifafanua hilo kwa kusema, kwamba nchi yetu imezoea amani ambapo matukio ya uhalifu yaliyokuwapo yalikuwa ni uvunjaji wa majumba, kuteka magari na kupora abiria, lakini hivi sasa kiwango cha ujambazi kimeonekana kuchukua sura mpya zaidi.

"Nafikiri mmejionea wenyewe matukio ya ujambazi yanayotokea kwenye mabenki, zaidi fedha zinazosafirishwa, lakini hii imetokana na jitihada za kufanikiwa kudhibiti wizi wa fedha wa kughushi, hivyo hata hili pia itafikia kipindi matukio haya yatadhibitiwa kwa kuwa na vifaa maalumu," alisema.

JAMBAZI LA UBUNGO LANASWA MUHIMBILI

2006-04-25 14:58:56
Na Moshi Lusonzo, Muhimbili
Mtu mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi aliyehusika katika tukio la uporaji uliofanyika Ubungo Alhamisi iliyopita ametiwa mbaroni baada ya kwenda kutibiwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Mifupa,MOI.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, jamaa huyo ambaye aliuchuna tangu wiki iliyopita, baada ya kuona donda la risasi alizotandikwa linaongezeka, juzi aliamua liwalo na liwe na akakimbilia Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, jamaa huyo wakati anafikishwa Muhimbili watu waliompeleka, walidai kuwa alijeruhiwa katika ajali ya gari.

Hata hivyo madaktari hao waliingiwa na hofu, baada ya kuona mgonjwa huyo hakuwa na PF3 na pia alikuwa akigoma kuvuliwa nguo na watumishi wa hospitali.

'Yeye alitaka avuliwe nguo na mmoja wa jamaa zake waliomfikisha hospitalini,' kikasema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mgonjwa huyo alipelekwa katika chumba cha X-Ray ambapo ilionekana jeraha alilonalo ni la risasi na pia bado kuna risasi mwilini. Kwa mujibu wa chanzo hicho, kutokana na ushahidi huo pamoja na taarifa nyingine zilizokusanya, jamaa huyo aliwekwa chini ya ulinzi. Msiri huyo amesema kuwa baada ya jamaa kuhojiwa alihusishwa moja kwa na tukio hilo na kwamba jana idadi ya askari wa kumlinda iliongezwa.

'Jana waliongezwa askari wengine wenye silaha,' chanzo hicho kikasema.
Chanzo hicho kimesema kitendo cha kuwekwa kwa ulinzi huo mkali kimewatia hofu wagonjwa wengine ambao wanatibiwa katika wodi hizo binafsi.

'Uongozi wa hospitali umeamua kumhamishia kwenye vyumba vya watu muhimu yaani VIP,' kikasema chanzo hicho. Habari zaidi zinasema majeruhi huyo ambaye jina lake bado limefanywa siri alitajwa na mwenzake ambaye alinaswa katika hospitali ya Lugalo. 'Inasema mtuhumiwa huyo aliyenaswa Lugalo alipobanwa alimtaja mwenzake,' chanzo hicho kimesema.


UJAMBAZI UBUNGO: SIRI YAFICHULIWA

2006-04-22 15:39:29
Na Daniel Mkate, Jijini
Siku mbili baada ya kutokea kwa uporaji wa kutisha katika eneo la Ubungo, watu mbalimbali wameibuka na hoja nzito zinazotoa mwanga wa watu waliohusika na unyama huo.

Mmoja wa askari waliojeruhiwa katika tukio hilo, Sajenti Wallace amesema majambazi yaliyohusika na tukio hilo ni yale yaliyokubuhu si wale ni majizi uchwara.

'Ni wazi tukio hilo lilipangwa na lilikuwa la kiufundi,' afande huyo ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na majeraha ya risasi alizomiminiwa katika tukio hilo amesema.

Amesema inaonekana kabisa timu iliyosuka dili zima ni ya mafundi na ambao wanafahamu vizuri matumizi ya silaha za kisasa.

Julius Masanja ambaye ni askari wa jeshi la wananchi mstaafu, amesema tukio zima kuanzia mwanzo hadi mwisho linaonyesha lilipangwa na watu wenye ujuzi wa hali ya juu.

Akasema majambazi wa kawaida kamwe hawawezi kujipanga vizuri kama hao walivyofanya.

'Inavyoonekana baada ya kusuka dili nzima, yaliifanyia mazoezi na kuona inawezekana,' akasema.

Ameongeza kuwa kama si huyo trafiki aliyekuwa pale kwenye mataa, huenda majambazi hayo yangezoa pesa na kuyoyoma wakati magari yakiwa kwenye foleni.

Mjeshi mwingine ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe amesema utaalam uliotumika ni wa hali ya juu ambao mtu asiyepitia mafunzo kama hayo hawezi kuwa nao.

'Mbinu zote zilizotumika ikiwa ni pamoja na kutumia magari tofauti, zinatumiwa na majambazi yenye ujuzi wa hali ya juu,' akasema.

Hata hivyo wananchi kadhaa walioongea na gazeti hili wamesema kuna uwezekano mkubwa majambazi hayo yalipigwa tafu na 'wajeshi' walioko kwenye system.

'Inaonyesha walichorewa raketi nzima na watu wanaofahamu mfumo mzima wa ulinzi hapa kwetu...kama si hivyo, majambazi hayo yasingepata ujasiri wa kubwaga gari lao pale kwenye kambi la jeshi la Twalipo, Mgulani' akasema mkazi huyo.

Katika tukio hilo lililoonekana kama moja ya sinema za wakali wa Hollywood wa kule Marekani, watu wawili waliuawa papo hapo na wengine watano kujeruhiwa.

Pia jumla ya shilingi milioni 150 mali ya benki ya NMB zilizokuwa zinapelekwa kwenye tawi la benki hilo la Wami, ziliibwa.

Wakati 'mchezo huo mchafu' uliodumu kwa takribani dakika 15 hivi unafanyika, askari mmoja wa kikosi cha usalama barabarani, Solomon Adam, aliyekuwa akiongoza magari hapo, alishuhudia unyama huo na kuamua kutimua mbio kuelekea kituo kidogo cha polisi kilichopo Ubungo Terminal.

'Wengi walidhani anajisalimisha kuogopa kuuawa, lakini kumbe alikuwa shujaa wa tukio hilo...yaani baada ya kufika kituoni hapo alitoa taarifa kwa polisi wenzake na kisha kuchukua silaha na kurejea eneo la mapambano,' akasema mtu mwingine aliyeshuhudia tukio hilo.

Akizungumza na Alasiri huku akionekana kutoamini kile kilichotokea, Koplo Solomon, akasema aliwahi kuchukua silaha kituoni ili aweze kupambana na majambazi hayo yaliyokuwa na silaha nzito huku yakichakaza ovyo risasi.

'Nilijificha huku nikirusha risasi za mapigo, lakini mijambazi ile ikaniona na kunirushia risasi, nikafanikiwa kuiona na kujitupa katika mtaro, ile risasi ikampata mpita njia mguuni,' akasema Koplo Solo.

Huku akiwa amechafuka na mavazi yake meupe yakiwa hayatamaniki, Koplo Solomon, akasema juhudi zake hata hivyo inawezekana ndizo zilizosaidia majambazi hao kushindwa kuondoka na maboksi mengine mawili ya chuma yaliyokuwa na pesa nyingi zaidi.


VINARA WA UPORAJI UBUNGO WATAJWA

2006-05-01 16:50:16
Na Adam Fungamwango, Jijini
Watu kadhaa ambao wanashukiwa kuwa vinara waliohusika kuchonga dili nzima iliyosababishwa kuporwa kwa mamilioni ya pesa za benki ya NMB wametajwa kwa majina. Hatua hiyo ambayo ni muhimu katika upelelezi wa sakata hilo la aina yake, imefikiwa baada ya jambazi mmoja kudakwa na kisha kubanwa hadi 'kufanya usaliti'.

Taarifa za kipolisi zinasema jambazi huyo aliyewataja wenzake ameuawa katika majibishano ya risasi na polisi mkoani Arusha. Jambazi huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Frank Lyatuu 31, ambaye inasemekana alikiri kabisa kuhusika na wizi huo.

Alitwangwa risasi wakati alipochomoa bunduki yake aliyokuwa ameficha sehemu za siri na kuanza kuwamiminia risasi polisi. Wakati hayo yakitendeka, jambazi huyo alikuwa akiwapeleka polisi mafichoni kwao ambako huwa wanaficha silaha.

Polisi mkoani Arusha wamesema walimkamata jambazi huyo Ijumaa iliyopita eneo la kwa Idd kwenye gereji moja na baada ya kumhoji akakiri kuhusika kabisa na matukio mbalimbali ya ujambazi likiwemo lile la kwenye mataa ya Ubungo.

Katika sakata hilo, polisi wanasema kuwa wakati anasindikizwa na askari ili akawaonyeshe 'ghala' lao la silaha, ghafla kama vile makomandoo na 'mastelingi' wa sinema za kibabe wanavyochomoka maadui zao baada ya kutekwa, alichomoka na kuanza kutimua mbio, huku akimimina risasi.

Polisi wanasema alianza kufyatua risasi kwa nia ya kuwatisha askari ili kujinusuru, lakini maaskari shujaa walifanikiwa kumlamba shaba iliyomdondosha chini na alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali na mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa wa Arusha Mount Meru.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha Matei Busilo, amesema majambazi yaliyotajwa mengi yalichomewa utambi na marehemu Lyatuu ambapo baada ya kumbana kisawasawa aliwataja wenzake ambao alishirikiana nao kwenye ujambazi huo.

Waliotajwa ni pamoja na Allen Charles Urio, a.k.a Katengo ambapo huyu ametajwa kuwa ni jambazi hatari, kwani ndiyo kiongozi wa majambazi katika Nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Katengo ambaye yeye alikamatwa hivi karibuni, inadaiwa kuwa yeye ndiye kiongozi wa majambazi wote katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

Jambazi mwingine aliyetajwa ni Richard Paul, ambaye imedaiwa kuwa ni rafiki wa karibu na Bw Justine Nyari ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka thelathini jela.

Mwingine aliyetajwa kushiriki katika uporaji huo ni Phillipo Charles ambaye ni maarufu kwa jina la Mpolee, Ramadhani Abraham a.k.a Dodo na Frank Mromboo. Mwingine aliyetajwa ni Wycliff Lumumba na Allen Urio ambao inadaiwa wameshatoroka gerezani nchini Kenya walikokuwa wamekamatwa. Katika tukio la Ubungo, jumla ya shilingi milioni 150 ziliporwa. Watu wawili akiwemo askari walipoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa.


27.07.2007 0126 EAT
KESI YA WIZI DUKA LA TRUST YANGURUMA

Na Yohanes Mbelege, Moshi

SHAHIDI wa pili katika kesi ya uporaji wa sh. milioni 138 katika duka la kubadilishia fedha la Trust la mjini hapa, Mrakibu wa Polisi, Bw. Narcis Misama, jana aliieleza Mahakama namna alivyoendesha gwaride la utambuzi kwa watuhumiwa wa Kenya wanaokabiliwa na kesi hiyo.

Bw. Misama aliieleza Mahakama hiyo kuwa gwaride hilo lilifanyika Januari 20 mwaka jana na baadhi ya wafanyakazi wa duka la Trust waliwatambua watuhumiwa hao. Huku akihojiwa na Wakili wa Serikali, Bw. Juma Ramadhan, Bw. Misama alidai alipata maagizo ya kuendesha gwaride hilo kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Hezromn Kigondo. Mbele ya Hakimu Mkazi, Bw. Hurbet George, Bw. Misama alidai gwaride hilo liliendeshwa mara tano huku watuhumiwa hao wakichanganywa na watu wengine.

Alidai kila gwaride lilikuwa likichukua kati ya dakika kumi au 20 na kwamba siku hiyo gwaride lilifanyika katika kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (KIA) wilayani Hai. Hata hivyo Mahakama ililazimika kumwonya Bw. Misama apunguze munkari wakati akihojiwa na Wakili wa utetezi, Bw. Loomu Ojare wa Arusha.

Hakimu George alilazimika kumsihi Bw. Misama awe akijibu maswali kwa utulivu na kwamba mara zote awe akiyajibu maswali anayoulizwa.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 6, mwaka huu itakaposikilizwa tena ambapo hadi jana ni mashahidi wawili tu waliokwishatoa ushahidi wao.

Wakenya wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Wilfred Onyango (26) mkazi wa Kilelesha Estate, Peter Gikula (46) wa Kiambuu na Jimy Njoroge wa Ngogi. Wengine ni Patrick Muthee (35) wa Madaraka Estate, Simon Githinji (37) wa Dondora Estate-Embakasi, Boniphace Mwangi (27) wa Thika Estate na David Ngigi (33) wa Komboko Estate.

Wote wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama na kupora kiasi cha sh. milioni 138 katika duka hilo la kubadilishia fedha, mali ya Bw.Vincent Laswai wa mjini hapa.


MAJAMBAZI: AMA ZAO AMA ZETU

2007-07-26 16:55:35
Na USU-EMMA SINDILA, JIJINI
Vita kali inayoongozwa na Jeshi la Polisi nchini dhidi ya majambazi inaendelea kushika kasi ya aina yake na tayari Jeshi hilo limefanikiwa kulinasa jambazi moja tishio Jijini Dar huku pia orodha ya majambazi wengine wanaojipenyeza nchini wakitokea kwao Kenya ikianikwa hadharani katika kile kinachoonekana kuwa sasa ni ama zao, ama za polisi.

Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi, mapambano hayo ya polisi wakisaidiwa na raia wema dhidi ya majambazi yamezaa mafanikio ya kutiwa mbaroni kwa jambazi hatari lililokuwa tishio Jijini Dar, linalofahamika kwa jina la Emmanuel Clement, 33. Taarifa za kipolisi zinasema jambazi Clement ameshafanya uporaji kadhaa wa kutumia silaha kabla ya kukimbia kifungo chake cha miaka 15 jela.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa huo, Bw. Liberati Sabas, amesema wamelikamata jambazi hilo hivi karibuni na kwamba hatua hiyo ni ya ushindi mkubwa kwao katika kuwanasa wengine zaidi.

Akasema hapo kabla, Clement alikuwa akisakwa na jeshi lao kutokana na tuhuma za ushiriki wake wa matukio mbalimbali ya kijambazi, yakiwemo yale yaliyohusisha uporaji wa mali za watu kwa kutumia silaha za moto.

Akasema Sabas kuwa katika tukio mojawapo la kijambazi, Clement alikutwa na hatia na mahakama ikamfunga jela miaka 15 huku yeye akiwa keshaingia mitini siku nyingi.

Hatutarudi nyuma katika vita hii… tunaamini wananchi wataendelea kutupa ushirikiano zaidi ili tuwanase mmoja baada ya mwingine, akasema Sabas.

Akasema Sabas kuwa Clement amenaswa na majambazi wengine wawili kule Mbezi Beach Jijini, katika tukio lililohusisha ukamatwaji wa gari aina ya Land Cruiser Lexus Station Wagon, yenye namba T 257 AFL, ambalo liliibiwa saa 8:00 mchana katika maeneo ya Sea Cliff mnamo Julai 15 mwaka huu.

Kuhusu majambazi toka Kenya, taarifa zaidi za kipolisi zinasema majina ya wale walio tishio zaidi yameshanyakwa na jesho la polisi nchini na msako dhidi yao unaendelea.

Taarifa hizo za kipolisi zinasema ushirikiano na Jeshi la Polisi nchini Kenya na lile la Kimataifa, Interpol, umewezesha kupatikana kwa majina ya majambazi hatari na picha zao (baadhi wanaonekana pichani mbele).

Taarifa hiyo inawataja majambazi hatari toka Kenya kuwa ni Agnes Kamene, Bonifece Ochieng, Charles Njoroge, Cyrprian Kwayera, Deepak Chamanlal, Enoch Anthony, Evans Mathyaka, Jackson Irungu, John Njoroge, Joseph Irungu, Justus Kariuki, Martin Kyalo, Muthee Peter, Peter Nderitu, Protus Massawe, Rashmi Chamanlal, Samuel Gitau na Yusuf Mwangi.

20 MBARONI, WAMO WANAWAKE 5

2007-08-01 08:41:11
Na Jackson Kimambo, PST Moshi
Watu 20 wakiwemo wanawake watano, wametiwa mbaroni mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la uporaji wa zaidi ya Sh. milioni 239.2 za benki ya National Microfinance (NMB), tawi la Mwanga. Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Bw. Lucas Ng'hoboko alisema watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika Wilaya za Mwanga, Moshi, Hai, Siha mkoani Kilimanjaro na jijini Arusha.

Hata hivyo, Kamanda Ng'hoboko hakutaja majina ya watuhumiwa hao kwa maelezo kuwa yamehifadhiwa kutokana na sababu za kiupelelezi lakini alisema miongoni mwa watu hao ni pamoja na raia wawili wa Kenya na 18 ni Watanzania. Aliwataja watuhumiwa raia wa Kenya kuwa ni Samweli Gitau Saitoti (30) maarufu kama Simon au Josee, mkazi wa Ngong-Nairobi na Michael Kimani (30), maarufu kama Joachim au Kim, mkazi wa Thika, Nairobi nchini Kenya pamoja na mwenyeji wao, Samson Chonjo (26), mkazi wa Ngulelo, jijini Arusha ambao walikamatwa mjini Arusha.

Kamanda Ng'hoboko alisema polisi wanaendelea na upelelezi wa kina kwa kushirikiana na wananchi na kutoa rai kwa kila mwenye taarifa yoyote kuhusu waliohusika kuitoa katika kituo cha polisi ili waweze kukamatwa. "Kama kuna mtu ama watu wanaendelea kuwahifadhi wahalifu hao, ni vyema wakatoa taarifa polisi ili tuweze kuwakamata Hatutawachukulia hatua zozote wote watakaotoa taarifa,` alisema.

Tukio la uporaji katika benki hiyo lilitokea Julai 11, mwaka huu saa 1:40 katika benki hiyo ambapo kundi la watu zaidi ya sita wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, walivamia benki hiyo na kumuua askari mwenye namba E.6825 PC, Michael Milanzi na kumjeruhi mwingine, F 6973 PC Naftali.

Watu hao waliingia katika benki hiyo kwa kutumia gari ya Meneja wa benki hiyo yenye namba za usajili T 524 AED na baada ya mauaji hayo walipora silaha mbili aina ya Sub Machine Gun (SMG) na risasi 60 na kisha kufanikiwa kupora kiasi hicho cha fedha.

Mmoja wa watuhumiwa hao, Peter Mbugua Ndung`u (37), aliuawa na polisi waliokuwa doria katika eneo la YMCA mjini Moshi baada ya kutokea mapambano makali ya kurushiana risasi waliokuwa katika gari dogo aina ya Toyota Corolla 100 lenye namba za usajili T 979 AMY. Baada ya kupekuliwa alitambuliwa kuwa ni raia wa Kenya.

Alisema baada ya tukio hilo, upelelezi makini ulianza na kwa ushirikiano na raia wema na wananchi kutoka maeneo mbalimbali mjini Mwanga, Moshi, Arusha na kuweza kubaini watu waliokuwa wamewahifadhi watuhumiwa hao kabla na baada ya tukio.

Watanzania hao walikamatwa na kutoa ushirikiano uliosaidia kufahamika kwa nyumba ya Njiro jijini Arusha ambapo majambazi wawili raia wa Kenya waliweza kumamatwa baada ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha kutoa nguvu kubwa ya askari, ili kukabiliana nao. Walikuwa wamejizatiti kwa silaha za kivita katika jumba la kifahari mnamo Julai 20, mwaka huu, alisema.

Watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliwateka Meneja wa benki ya NMB tawi la Mwanga, Bw. Robert Marando (56) na familia yake pamoja na Meneja Uendeshaji wa benki hiyo, Bi. Salome Matemu (54) na familia yake na kisha kuwaamuru kuchukua funguo za chumba maalum cha kuhifadhia fedha (strong room) na kufanikiwa kupora kiasi hicho cha fedha na baadaye kuwafungia ndani ya chumba hicho.

Hivi karibuni, Kamanda Ng`hoboko alikaririwa akisema polisi kwa kushirikiana na raia wema pia wamefanikiwa kupata gari aina ya Toyota Landcruiser lililodaiwa kutumika katika tukio hilo likiwa limetelekezwa katika kijiji cha Orkoriri, Kata ya King'ori wilayani Arumeru mkoani Arusha usiku wa kuamkia Julai 14, mwaka huu.

Alisema gari hilo lilitambuliwa kuwa ni mali ya ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) ambalo liliibwa kwenye ofisi hizo mkoani Arusha Julai 5, mwaka huu.
 
Kitabu bora cha UJASUSI na USALAMA kiitwacho "IJUE HISTORIA" chenye kurasa 470 kinachoongelea historia za UJASUSI, UPELELEZI, SIRI ZA DUNIA, UGAIDI na UHALIFU kimeshatoka na kinapatikana kwa sh 25,000 tu.

Pia kundi la "ijuehistoria" (WhatsApp group) lipo kwa gharama ya sh 3000 kwa mwezi.

Namba za mawasiliano na malipo ni - TIGO 0679 95 93 08 (namba ya Whatsapp pia)


SEHEMU YA KWANZA

UJAMBAZI MKUBWA BENKI YA NMB KILIMANJARO

Na. COMRADE SABOUR/ G.H. MASHERETO (Ijue Historia)

Hii ni makala ya ujambazi inayoongelea moja ya ujambazi mkubwa na wa akili nyingi sana kuwahi kutokea katika ardhi ya taifa la TANZANIA na kuongelewa sana wakati wake tukio hili likiwa limetokea maana lilisimamisha taifa kwa muda na vyombo vya ulinzi na usalama kuhangaika kila kona kudili na ujambazi huu.

Ujambazi huu mkubwa na wa akili nyingi sana ulitokea mkoani KILIMANJARO wilayani MWANGA ambapo washiriki wa ujambazi huu walikuwa wanatokea mataifa mawili tofauti ambayo ni KENYA na TANZANIA na ijulikane mataifa haya ni jirani sana kwa kupakana.

Ujirani mwema na undugu wa mataifa haya ambao unajulikana umeimarishwa na waasisi wao kwa TANZANIA ni MWALIMU JULIUS NYERERE na KENYA ni bwana JOMO KENYATTA ulitumika vibaya na hawa majambazi kwa kushirikiana kupanga na kutekeleza ujambazi huu katika benki kubwa ya NMB.

Majambazi hawa walichofanya katika benki ya NMB wilayani MWANGA imebaki kuwa historia inayokumbusha kipindi cha matukio mengi ya ujambazi nchini TANZANIA ambayo yalianza mwisho mwa karne ya 20 [1990’s] kuingia karne ya 21 [2000’s].

Kiufupi kipindi cha utawala wa raisi BENJAMIN MKAPA na JAKAYA KIKWETE vitendo vya ujambazi na uhalifu kwa ujumla vilikuwa vimeshamiri sana nchini TANZANIA na viongozi hawa waliotawala vizuri TANZANIA huu udhaifu wa kushindwa kukabiliana na ujambazi ulioshamiri vipindi vyao vya utawala hawawezi kuukwepa.

Kwenye uongozi na siasa ni jambo la kawaida kwa kila utawala kuwa na mazuri na mabaya yake [uimara na udhaifu wake], sasa hawa majambazi waliokwenda kuweka historia katika ardhi ya WAPARE pale wilayani MWANGA kiongozi “mastermind” wao alikuwa ni MKENYA.

MKENYA huyu alikuwa akijulikana sana kwa jina lake la utani MACHO MBAYA [MACHO MABAYA, Kiswahili cha KIKENYA hakiko vizuri], kwa miaka ya 2000’s nchini KENYA ukisikia jambazi MACHO MBAYA na genge lake wamepiga sehemu tukio ujue haukuwa tu uwizi wa unyang’anyi kwa kutumia silaha tu bali ni vita.

MACHO MBAYA na genge lake ujambazi wao ulikuwa ni vita kutokana na kutumia silaha za kivita kama AK-47 na mabomu kitu ambacho sio cha kawaida na genge hili la MACHO MBAYA walikuwa wakifanya hivi ili wahanga wao na jeshi la polisi wawaogope kwa kuwaona kama ukoma.

MACHO MBAYA na genge lake walikuwa wanajua kuzitumia silaha ipasavyo utafikiri wamewahi kupitia jeshi lolote na kupata mafunzo, na ukiachana na uwezo mkubwa wa kutumia silaha hizo pia MACHO MBAYA yeye binfasi ni mzuri wa mapigano ya ngumi na alivyopanda juu [mrefu] ndo kunamuongezea uimara katika mapigano ya ngumi.

MACHO MBAYA kiufundi nchini KENYA alikuwa ameshindika na anatafutwa sana na vyombo vya ulinzi na usalama vya KENYA kwa kesi zake nyingi za mauaji na ujambazi maana yeye haoni shida kuua pale kunapotokea kiwingu cha kutaka kumkwamisha ujambazi wake.

Sasa baada ya kusumbua sana KENYA akahamia nchini TANZANIA na wakati huo kulikuwa na wimbi kubwa la majambazi wa KENYA kuja nchini TANZANIA kushirikiana na majambazi wazawa wa huko kutekeleza ujambazi wao katika taasisi za kifedha ambako ni uhakika kuna fedha za kutosha hakuna ubahatishaji.

Jambazi kama MACHO MBAYA na genge lake kuamua kuja TANZANIA kutekeleza matukio ya ujambazi ilikuwa habari mbaya sana na hawakuwa wamekuja kwaajili ya tukio moja la benki ya NMB bali kwa matukio mengi yani walikuja kuweka kambi ndo maana walipitisha mzigo mkubwa wa silaha na mabomu.

MACHO MBAYA na genge lake kwa ubora wao uliopelekea kushindikana nchini KENYA wakakutana na ubora wa jeshi la polisi la TANZANIA ambao ulisaidiwa na kauzembe kadogo walichoteleza wakina MACHO MBAYA na kupelekea “WAR IN ARUSHA”.

KUZALIWA KWA WAZO

Kabla ya kuelekea kuona wazo la ujambazi huu mkubwa wa benki ya NMB ulivyozaliwa kwanza kabisa tumjue MACHO MBAYA ni nani…? ambaye ndo “mastermind” wa ujambazi huu nchini TANZANIA na hata matukio mengine ya ujambazi huko nchini KENYA.

Kwanza ifahamike MACHO MBAYA kwa majina yake halisi anaitwa SAMUEL GITAU SAITOTI amezaliwa mwaka 1973 katika kaunti ya KAJIADO katika jimbo la RIFT VALLEY na wengi wanajua au kudhani MACHO MBAYA ni mzaliwa wa kaunti ya NAKURU.

Sababu inayopelekea kudhani MACHO MBAYA ni mzaliwa wa kaunti ya NAKURU ni maisha yake ya umaarufu kama jambazi hatari kuenea akiwa kaunti ya NAKURU na alipapenda sana na kuwa kitovu chake cha ujambazi yani eneo lake la kujidai akisifika na kutukuzwa kama shujaa fulani kumbe jambazi tu.

MACHO MBAYA kabila lake ni MKIKUYU halisi na kabila la WAKIKUYU ndo kabila kubwa na lenye nguvu nchini KENYA kwa kutawala nyanja mbalimbali kisiasa, kibiashara, kiuchumi, kielimu n.k na MACHO MBAYA wakati akikua katika kaunti ya KAJIADO alikuwa mtoto mtundu na mjanja sana.

MACHO MBAYA shule kwake ilikuwa kama kituo cha polisi na alikuwa akisoma ili mradi iende sababu ya kulazimishwa na wazazi/walezi wake, na akiwa kijana baada ya balehe alibadilika kutoka kuwa mtundu kwenda mdokozi/kibaka [mwizi wa vitu vidogo].

Safari yake ya kwenda kuwa jambazi hatari iianzia hapo na wakati akizidi kuwa kijana mkubwa kipindi hicho miaka ya mwanzoni mwa 1990’s nchini KENYA na barani AFRIKA kwa ujumla kulikuwa na genge hatari sana lijulikanalo kama MUNGIKI.

Genge la MUNGIKI asili yake ilikuwa ni kabila la WAKIKUYU ambalo ndo kabila la MACHO MBAYA, kwa genge hatari hili kujihusisha na kila aina ya uhalifu nchini KENYA sio uwizi, sio mauaji, sio ubakaji, sio uuzaji wa mihadarati, sio vurugu n.k yani kila takataka ya uvunjifu wa amani ilikuwa ikifanywa na genge hili la WAKIKUYU.

Vijana wengi nchini KENYA hasa WAKIKUYU ambao wameamua kujihusisha na mambo ya kihalifu walikuwa wanapenda kujiunga na kundi la MUNGIKI maana ilikuwa ndo kundi hatari linaloogopeka mpaka na serikali ya KENYA na vyombo vyake vya ulinzi na usalama.

Pia ilikuwa fahari kwa kijana kujulikana au kujitambulisha yeye ni mwanachama wa MUNGIKI na MACHO MBAYA alianzia hapa ila alikuwa wale wanakundi wa ngazi ya chini kabisa ambao ndo wanatumika na viongozi wa MUNGIKI kutekeleza uvunjifu wa amani nchini KENYA.

Kwa ngazi ya kina MACHO MBAYA walikuwa wanapewa silaha za jada kama mapanga, visu, mashoka n.k na rasmi akawa amehama nyumbani kwa kuishi kwenye makambi na maghetto ya wanachama wenzie wa MUNGIKI na utumiaji wa vilevi na mihadarati kama bangi ulianzia hapa.

Maghetto na makambi ya MUNGIKI kulikuwa na mafunzo ya mapigano na ikumbukwe MUNGIKI ilikuwa mpaka na wanachama kutoka vyombo vya ulinzi na usalama ambao walichangia sana kutisha kwa genge hili kwa kuwa wakufunzi kwa vijana wa MUNGIKI ili wawe hatari sana.

Ubora wa mapigano kwa MACHO MBAYA ulitengenezwa hapa akiwa mwanachama mdogo wa MUNGIKI na toka ajiunge genge hilo hakukaa sana yeye na vijana wengine walipangiwa kazi jijini NAIROBI [mji mkuu wa KENYA] ambako ndo kulikuwa kitovu cha genge la MUNGIKI.

Hapo jijini NAIROBI genge la MUNGIKI lilikuwa likikusanya kodi kwa wafanyabiashara, wakazi wa uswahilini, MATATUS [usafiri maarufu nchini KENYA] n.k kama vile wao ni serikali na asiyekubali kutoa hela kwa MUNGIKI basi cha mtema kuni atakipata na hana pa kwenda kulalamika maana walikuwa tishio nchini humo.

Genge la MUNGIKI walikuwa na utawala wao ndani ya utawala wa serikali ya KENYA na waliokuwa wanaumia ni wanachi sababu kodi ya serikali iko palepale kwahiyo kunalipwa kodi mara mbili na bora kodi ya serikali isilipwe kwa mlipaji kodi kufanya janja janja ila sio kodi ya MUNGIKI ambayo ni lazima na haitakiwi masihara kabisa.

Sasa MACHO MBAYA yeye jijini NAIROBI alikuwa amepangiwa kukusanya kodi kwa magari ya MATATUS akipozi kama mpigaji debe kwa kushinda kwenye vituo vikuu vya usafiri akifanya kazi ya genge lake na kipindi hicho hicho wamiliki na waendeshaji wa MATATUS walikuwa ni mamafia kwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu.

Ndo maana leo hii ukipitia rekodi ya majambazi wakubwa na tishio katika historia ya taifa la KENYA unakuta wengi wao chimbuko lao walianzia kwenye familia kama wamiliki, madereva, makonda au wapigaji debe wa MATATUS na mfano ni jambazi hatari WACUCU n.k

MACHO MBAYA kutokana na kuwa karibu na jumuiya ya MATATUS alivutiwa na namna mamafia hao wanavyofanya uhalifu wao na baada ya hapo kila mtu anapata gawio lake huku wakiendelea na biashara ya usafiri huo tofauti naMUNGIKI jinsi ilivyokuwa ikijiendesha.

MUNGIKI waliokuwa wanafaidi ni viongozi wao wa chini wanatumika tu kuzalisha mapato kwaajili ya wakubwa zao na kubakia maskini maisha yao yote na ikitokea vurugu zozote wanatangulizwa wao kwa kukamatwa, kujeruhiwa au kuuliwa huku viongozi wanakula kuku kwa mrija.

Kwa MUNGIKI hakukuwa na usawa ila kwa MATATUS angalau kulikuwa na usawa na MACHO MBAYA akaona isiwe tabu akajihusisha na jumuiya ya MATATUS na kwa sifa zake za kimuonekano ziliwatia hamasa WANAMATATUS kumuona mali.

MUNGIKI walikuwa na utaratibu wa kuua wanachama wao wanaojitoa sababu sheria yao mtu akijiunga MUNGIKI kitakachomtenganisha na kundi hilo ni kifo na MACHO MBAYA alikuwa anajua hilo ila sheria hiyo ilikuwa ikitekelezeka kwa viongozi wa MUNGIKI hao wanachama wa chini mpaka awe msaliti na wajue ndo watamuua.

MACHO MBAYA alikuwa mwanachama wa chini hakuna anayemzingatia na akaachana na MUNGIKI kwa kujiunga na familia ya MATATUS ambapo alikabidhiwa basi na kuwa dereva na rasmi akawa mwanafamilia wa MATATUS kuweza sasa kuhusishwa na umafia wa familia hiyo ya usafiri maarufu nchini KENYA.

MACHO MBAYA alikuwa dereva na mhalifu hapo hapo na matumizi ya silaha za moto kama bunduki, mabomu alianza kujifunzia kutoka kwa familia yake mpya hiyo na pia alijifunza uwizi mkubwa zinafanyikaje huku kichwani mwake akiwa na ndoto siku aje kujitegemea kwa kuanzisha kundi lake binafsi.

MACHO MBAYA muda mfupi toka ajiunge na familia ya MATATUS alijiona kule MUNGIKI alikuwa akijichelewesha maana sasa anajua uhalifu ule ambao alikuwa akiutaka sio mambo ya vurugu kutawala sana, kusumbuana na kukusanya kodi n.k

MUNGIKI walikuwa wakifanya kila aina ya uvunjifu wa amani ila ya uwizi ilikuwa chini na matukio madogo yakulinganishwa na ukibaka sio wa kutekeleza matukio makubwa kama uwizi katika mabenki, utekaji magari, n.k ndo maana MUNGIKI walikuwa wakitegemea ukusanyaji wa kodi.

MACHO MBAYA akiwa anajifunza huku akijishughulisha na uhalifu wa maana sio wa ukibaka kulianza kutokea mzozo kati ya wamiliki na waendeshaji wa MATATUS dhidi ya MUNGIKI na kikubwa hapo ni wanafamilia wa MATATUS kuchoshwa na kodi wanazochajiwa na MUNGIKI halafu hapo hapo tena serikali nao wanawakamua.

Wanafamilia wa MATATUS wao ni mamafia sasa kwanini waendelea kuwachekea genge la MUNGIKI hata kama ni wazuri kwenye vurugu na uwingi wao, wanafamilia wa MATATUS wakasitisha kutoa chochote kwa genge la MUNGIKI na wako tayari kwa vita yoyote dhidi yao.

Mwaka 2002 vita waliyokuwa wako nayo tayari wanafamilia wa MATATUS ilianzishwa na MUNGIKI na ilikuwa hatari sana kwa kuuana, kujeruhiana na kukamatwa na polisi ambao walikuwa wakivamia kutuliza ghasia hizo sababu zilikuwa zinaathiri mpaka wananchi wa kawaida.

Vurugu hizi zilipelekea serikali ya KENYA na vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuamka na hali ya amani ikawa chini maana operesheni kali iliendeshwa ya kukamata kwa malundo wanachama wa pande zote mbili na MACHO MBAYA akaona hali ishakuwa tete na kukimbilia kaunti ya NAKURU.

Hapo kaunti ya NAKURU alifikia mji wa NAVASHA na vurumai zilizotokea jijini NAIROBI kati ya MUNGIKI na wanafamilia wa MATATUS ilikuwa tiketi ya MACHO MBAYA kuanzisha utawala na genge lake mwenyewe kwa vijana wenzie kutokea pande zote mbili zilizokuwa zinagombana na kukimbia kama yeye kuwasajili na kuwa kiongozi wao.

Utawala wa kihalifu wa MACHO MBAYA ulianzia mwaka 2003 na aliweza kushawishi vijana wenzie kujiunga naye kutekeleza matukio ya kihalifu kwa kuachana na magenge ya wanafamilia wa MATATUS na MUNGIKI ambao wapo kwenye bifu kubwa sana.

Vijana waliokuwa tayari walimfuata MACHO MBAYA huku wengine walishindwa kushawishika naye sababu ya ugeni wake katika uongozaji wa kundi la kihalifu, MACHO MBAYA na genge lake walianza na uhalifu wa utekaji magari katika barabara kuu ya NAIVASHA-NAIROBI kujipatia fedha za kuweza kununua silaha zitakazotumika kwa ujambazi mkubwa.

Silaha za kufanyia uhalifu wao walikuwa wanazichukua kimagendo kutoka nchini SOMALIA ambako kulikuwa na migogoro na mapigano yasiyoisha toka mwaka 1991 na kupelekea uwepo wa silaha nyingi nchini humo na rahisi kwa wahalifu wa mataifa ya jirani kwenda kununua huko.

KENYA na SOMALIA ni nchi jirani na silaha huko nchini SOMALIA ni bei ya chini sana sababu zipo nyingi sana na muda mwingine wanunuzi wa silaha za kimagendo hizo wanabadilishana na vitu kama vyakula kwa silaha kutokana na hali ya njaa iliyopo nchini humo kwa WASOMALI kukosa muda wa kuzalisha chakula.

Hii sio SOMALIA tu ni mataifa yote ambayo yamegubikwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe kama BURUNDI, RWANDA, KONGO, SUDAN n.k kumekuwa na silaha bwelele na wahalifu wa mataifa jirani hutumia fursa kununua kutoka mataifa hayo kwa bei ya chini.

MACHO MBAYA soko rahisi la silaha nchini SOMALIA alilijua kupitia wanafamilia wa MATATUS kwa kujua wauzaji wa nchini SOMALIA, bei kwa kila aina ya silaha na mifereji ya kupitisha silaha hizo kutoka nchini SOMALIA kuja KENYA ambapo kulikuwa na mawakala rasmi wa kazi hiyo hupitisha silaha za wateja tofauti na wanajua ni vipi wanawapooza wanausalama na walinzi wa mpakani.

Kipindi hicho KENYA alikuwa hajaimarisha ulinzi na ukaguzi mkali mipakani mwa taifa lake na SOMALIA sababu AL-SHABAB ilikuwa haijazaliwa bado migogoro na mapambano yalikuwa hayahusishi makundi ya KIISLAMU yenye msimamo mkali kwahiyo uingizaji wa silaha ulikuwa sio mgumu kama miaka ya sasa.

MACHO MBAYA na genge lake mwaka huo huo 2003 wakiwa na silaha nzito baada ya mzigo kuwafikia kutoka nchini SOMALIA walianza utekelezaji wa ujambazi mkubwa wa pesa nyingi kwa kulenga taasisi za kifedha kama mabenki, maduka ya kubadilisha fedha n.k

Genge la MACHO MBAYA walianza na duka moja kubwa la kubadilisha fedha jijini MOMBASA liitwalo FORT JESUS na walichagua hili duka sababu ya kupatiwa taarifa kuwa linamzunguko mkubwa wa fedha kutokana na wateja wengi kubadilisha fedha zao dukani hapo.

Genge la MACHO MBAYA wakavamia duka hilo na kutekeleza ujambazi wao ambao ulifanikiwa na kuwa mwanzo mzuri kwa genge la MACHO MBAYA maana sasa wakawa na hela ya kutosha zaidi kuweza kuagiza mzigo mkubwa zaidi wa silaha na mambo mengine kama kula bata.

Kufikia mwaka 2005 genge la MACHO MBAYA lilikuwa hatari sana nchini KENYA na mtu ajulikanae MACHO MBAYA akawa midomoni mwa vyombo vya ulinzi na usalama huku wakiwa hawamjui sura yake bado ila jina lake walilisikia sana kama jambazi chipukizi hatari anayekuja kwa kasi ya 5G.

Nchini KENYA miaka hiyo ilikuwa kama TANZANIA kugubikwa na matukio makubwa ya kihalifu pamoja na majambazi sugu wenye majina yao na kwa mwaka 2005 jambazi MACHO MBAYA alikuwa akionekana kama jambazi sugu chipukizi maana kulikuwa na majambazi kama SILAS MUGENDI NJERU, GODFREY MULWA KITHEKA n.k

Na hao majambazi wakubwa waliokuwa na majina wakina SILAS MUGENDI NJERU walikuwa gerezani ila bado vitendo vya kihalifu vilikuwa vikishamiri na kuambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa MACHO MBAYA ni hatari ndiye anayesumbua taifa la KENYA na genge lake kwa kupiga matukio ya kihalifu miji mbalimbali nchini humo.

MACHO MBAYA na genge lake kuwa hatari na tatizo jipya nchini KENYA mwaka huo huo 2005 walikwenda kuweka rekodi na kujisimika yeye na genge lake sio majambazi chipukizi tena bali majambazi sugu wanaotakiwa kuzimwa haraka na vyombo vya ulinzi na usalama nchini humo kwa usalama wa raia na mali zao.

Tukio hilo lilikuwa kwenda kuvamia gereza la EMBU GK na kutorosha wafungwa ambao ndani yake kulikuwa na vijana wake ambao walikuwa wamekamatwa na kuhifadhiwa humo na ndo hao baada ya kuhojiwa walimtaja kiongozi wao ni MACHO MBAYA na jina hilo kuanza kutamkwa sana midomoni mwa polisi wa KENYA.

Wazo la kuokoa vijana wake pamoja na wafungwa wengine gerezani EMBU GK halikuwa lake kwa yeye tayari kunyoosha mikono juu kuwa amepoteza hao vijana wake na anasajili vijana wengine kuziba mapengo yao kama vile magenge mengine ya kihalifu mwanachama akishatiwa nguvuni na vyombo vya ulinzi na usalama ndo basi hawamuhesabii tena labda aje kuachiwa kama hatafungwa kifungo cha maisha au kunyongwa.

Kwa kesi ya vijana wake MACHO MBAYA ilikuwa nitolee sababu walikuwa na mashtaka ya mauaji ya polisi na raia, wazo la kuvamia gereza lililetwa na jambazi sugu SILAS MUGENDI NJERU ambaye tarehe 22 juni 2005 na wenzie walitoroka gereza la SHIMO LA TEWA.

Wakina SILAS MUGENDI NJERU hawakutoroshwa na mtu ni wenyewe wakiwa gerezani walijipanga na kutoroka, na baada ya tukio hili jambazi sugu NJERU akataka kurudisha utawala wake wa ujambazi ila akakutana na ugumu wa genge lake kusambaratika kwa wengine kuwa magerezani na wengine wameanzisha magenge yao hawawezi tena kuwa chini yake.

Jambazi NJERU alionekana zama zake zimeshaisha baada ya kukamatwa na kufungwa gereza la SHIMO LA TEWA na sehemu ya watu wake wakina MBURU, WATHIGO, KARIUKU, n.k tayari walikuwa majambazi wa kimataifa hawashikiki.

Hao waliokuwa wanakundi wa jambazi NJERU mwaka 2004 walikuwa wametoka kufanya tukio la kihistoria nchini TANZANIA mkoani KILIMANJARO wilayani MOSHI katika benki ya NBC kwa kuiba kiasi kikubwa cha fedha katika historia ya taifa la TANZANIA ambacho kilikuwa shillingi bilioni 5.3.

Sasa majambazi wake wameshiriki katika uwizi mkubwa kama huo na wako vizuri kifedha waanze kumfikiria jambazi NJERU tena ambaye hapo alipo anatafutwa sana kwa kutoroka gerezani, ilikuwa ngumu sana kwa kuhesabika zilipendwa.

Jambazi NJERU akaona namna pekee ni kutorosha watu wake walioko magerezani kwa kuachana na hao ambao wameshaota mapembe na aliamini utawala wake utarudi sababu hao atakaowatorosha watamuona yeye kama Mungu mtu kuwaepusha na kifungo cha maisha au kunyongwa mpaka kufa kwa makosa yao ya ujambazi na mauaji.

Gereza ambalo lina watu wake lilikuwa EMBU GK na kuona hapo ndo pakuchorea mchoro kwenda kukomboa watu wake wawe huru tena na arudishe utawala wake wa ujambazi, na baada ya kulichagua gereza hilo ambalo ndo lenye majambazi wenzie wamefungwa akaona bado kuna shida moja ambayo ni hawezi mwenyewe kufanya tukio hilo kubwa ikizingatiwa na yeye ametoroka gerezani na anatafutwa sana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Jambazi NJERU akamkumbuka jambazi MACHO MBAYA ambaye ndo alikuwa kwenye ubora wake na wanajuana kiasi fulani kwa kuweza kumshawishi washirikiane katika uvamizi huo gerezani EMBU GK na pia itakuwa fursa kwake MACHO MBAYA kutorosha vijana wake waliokamatwa na kufungwa gerezani humo.

Jambazi MACHO MBAYA kufuatwa na jambazi NJERU kuelezewa tukio hilo la uvamizi gerezani EMBU GK alikubali na kwa pamoja wakakaa chini kuandaa mchoro wa tukio hilo na uzoefu wa jambazi NJERU kukaa gerezani ulisaidia kuandaa mchoro mzuri kuhakikisha wanawakomboa majambazi wenzao.

Kila kitu kuwa sawa ikabaki kuvamia gereza la EMBU GK na mwezi agosti ndo ilikuwa utekelezaji wa mchoro wao na mashuhuda wa tukio hili wanasema ilikuwa kama wanaangalia filamu za HOLLYWOOD kumbe ndo uhalisia wenyewe na kuamini kinachoigizwa kwenye filamu za nje kinawezekana kutendeka.

Kwanza watekelezaji wakina MACHO MBAYA walikuwa na silaha za kutosha pamoja na mabomu kuhakikisha wanachopeleka gerezani EMBU GK ni vita kwa kujizungusha mikanda ya risasi ili wawe wanamimina tu na katika mchoro wao walishajua wanakamata wapi kuhakikisha gereza la EMBU GK linakuwa chini yao.

Grereza la EMBU GK ni kama magereza mengine duniani kwa askari magereza wanaoshika silaha za moto wanakuwa wale wa lango kuu la kuingilia gerezani pamoja na wale wa mnarani ila askari magereza wengine wanakuwa na silaha za jadi kama rungu, manati n.k ambazo hutumia kutuliza ghasia za wafungwa pale kunapotokea vurumai gerezani.

Ni sawa kuwa hivyo sababu ya mazingira ya gerezani kwa wafungwa kotukuwa na hatarishi yoyote kufanya askari magereza wote kutembea na silaha za moto na hiyo hali wakina MACHO MBAYA walitembea nayo wakijua nani anakuwa na silaha za moto kuweza kupambana naye kwanza na pia kuwahi kukimbilia ghala la silaha ili askari magereza wasikimbile kwenda kuchukua silaha .

Askari magereza wengi kutoshika silaha za moto haimaanishi hakuna silaha za moto za kutosha magerezani, na ikitokea kuna tukio kubwa limetokea gerezani linalohitaji silaha za moto kushikwa na askari wote basi haraka huelekee kwenye ghala lao la silaha ambako wanapewa silaha za moto hizo na huko ndo wakina MACHO MBAYA walipanga kupawahi kukamatwa wakishazama gerezani ili kujihakikishia hawapati upinzani wa ziada.

Siku ya tukio wakina MACHO MBAYA wakiwa na silaha wakafika gerezani EMBU GK wakiwa kamili na kufika getini ambako lazima ukaguzi ufanyike wakashuka na mitutu yao na kuanza kumimina kusafisha njia ili wazame gerezani ndani.

Wakina MACHO MBAYA walikuja kibabe hakuna stori wala kuchekeana ni wanamimina tu na polisi magereza mpaka wenye silaha walitupa na kukimbia kusikojulikana kwa wengine kujifungia majumbani mwao, wengine kuparamia ukuta na kutoroka n.k

Wakina MACHO MBAYA waliwasawazisha na sababu lilikuwa tukio lisilotegemewa kwa askari magereza ni walikuwa kama wamechanganyikiwa na ghala la silaha kama mchoro wao ulivyosema lilidhibitiwa na askari magereza aliyekuwa zamu ghalani hapo aliuliwa.

Wakina MACHO MBAYA hawakuhangaika na askari magereza waliokuwa wakikimbia kuokoa maisha yao sababu sio lengo lao, wenyewe walielekea moja kwa moja kwenye vyumba vya magereza kuwafungulia majambazi wenzao na wafungwa wengine waliobahatika.

Wafungwa waliokombolewa walikabidhiwa silaha hapo hapo kwaajili ya kujihami na wakateka magari ya askari magereza ili kuwapakia wenzao na kuondoka eneo la tukio wakiwa wameacha vifo vya watu wanne huku mmoja wao akiwa jambazi mwenzao waliyezama naye ndani.

Tukio hili lilikuwa aibu kwa taifa la KENYA na kuonesha majambazi wamewashindwa mpaka wanakuja kuwaokoa wenzao gerezani humo na mbaya zaidi matukio hayo ya wafungwa kutoroka mikononi mwa jeshi la magereza kwa kutoroka wenyewe au kutoroshwa na wenzao yalikuwa yamefuatana toka mwaka 2004 mpaka mwaka huo 2005 ila hakuna mabadiliko kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuzuia matukio hayo ya aibu.

Mwaka 2004 kulitokea matukio mawili ya utorokaji wafungwa ambayo yalikuwa ya gereza la NAVASHA ambalo linahesabika ni gereza lenye ulinzi mkali zaidi ila wafungwa wapatao 28 walitoroka tena wale walioshindikana ambao ingekuwa hiari yao KENYA basi wangewaua ili roho zao zipumzike kuwa wasumbufu wao hawapo tena duniani.

Tukio la pili lilikuwa utoroshwaji wa wafungwa 29 wakiwa mahabusu ndogo ya mahakama ya MERU wakisubiria kesi zao kusikilizwa na wale wale wanaotoroshwa ni majambazi na wauaji ambao hawana la kupoteza sababu wanajua hata wakibaki mikononi mwa mamlaka za magereza vifungo vyao ni maisha jela au kunyongwa mpaka wafe.

Kwahiyo mwaka 2004 na 2005 nchini KENYA kuachana na matukio ya ujambazi yaliyokuwa yanaendelea pia mchezo wa wafungwa kutoroka au kutoroshwa ulikuwepo na habari tena ya raia wao kutekeleza uwizi wa kihistoria nchini TANZANIA pale benki ya NBC ulizidi kuwachanganya kuona wao sasa wamegeuka chuo cha ujambazi AFRIKA MASHARIKI NA KATI.

Sifa hiyo ya KENYA kuwa chuo cha ujambazi AFRIKA MASHARIKI NA KATI ilikuwa ya kweli maana sio TANZANIA tu hata UGANDA, KONGO, MSUMBIJI n.k kote huko wanalia na majambazi wa KENYA kuja kushirikiana na majambazi wa mataifa yao kutekeleza ujambazi mkubwa.

Hapo mwaka 2005 gereza la EMBU GK limeshavunjwa na kutoroshwa wafungwa miezi miwili mbele wale majambazi wake wa zamani NJERU ambao walihusika na ujambazi wa bilioni 5.3 NBC MOSHI TANZANIA walikwenda nchini MSUMBIJI kwaajili ya kuumiza na huko tena yani hawapoi wala kuridhika.

Hii tabia ya majambazi wa KENYA kutorosha wenzao magerezani au mahakamani walijaribu kuleta TANZANIA kuokoa majambazi WAKENYA wenzao kupitia vyoo vya mahakama wakidhani ni rahisi kama ilivyokuwa kwao kwa kusahau au kutojua vyombo vya ulinzi na usalama vya TANZANIA ni vinara wa ujasusi.

Vyombo vya ulinzi na usalama vya TANZANIA vilitoa funzo jinsi ya kudili na majambazi wanaotaka kujaribu visivyojaribika maana kitendo cha uwokozi wa wafungwa sugu walioshindikana ni hatari sana kwa usalama wa raia na mali zao, pia ni aibu kubwa sana isiyoelezeka ambayo kwa nchi zilizoendelea lazima viongozi wahusika watajiwashibisha wenyewe kupunguza aibu hiyo.

Kwa taifa la KENYA wahusika walikaa kimya kama hakujatokea jambo huku nguvu kubwa ikitumika kupoozesha tukio hilo la uvamizi gerezazi EMBU GK na KENYA walichofanya ndo mataifa mengi ya AFRIKA hufanya kwa kutotaka kuwajibika na badala yake huminya vyombo vya habari visieleze ukweli jamii ni kilitokea kwa undani na wapi uzembe ulifanyika.

Jambazi NJERU na MACHO MBAYA jambo lao lilitiki na kila mmoja aliendelea na mambo yake na watorokaji wake huku vyombo vya ulinzi na usalama vya KENYA vikiwa vimechachamaa kusaka wavamizi na watorokaji gerezani huku wakiwasihi wafungwa waliotoroka wajisalimishe wenyewe kabla nguvu kubwa haijatumika na kujitengenezea kesi nyingine mpya.

Kwenye utoroshaji wa wafungwa kuna wafungwa ambao hawakuwa kwenye orodha ya jambazi NJERU na MACHO MBAYA kutakiwa kutoroka, ni wenyewe walitumia nafasi ya sintofahamu iliyotokea gerezani baada ya uvamizi kutoroka kusikojulikana na hawakuangana na timu ya majambazi waliokuja kuvamia gereza la EMBU GK na ndo hao walikuwa wakishauriwa kujisalimisha ili kuwapunguzia kazi vyombo vya ulinzi na usalama wabaki kudili na masugu.

Vyombo vya ulinzi na usalama kwa tukio hili la uvamizi wa gereza la EMBU GK liliweza kumjua jambazi MACHO MBAYA vizuri mpaka muonekano wake na kuingizwa kwenye orodha ya watu wanaohitajika sana, na jeshi la polisi walikuwa wametangaza vita dhidi yake.

MACHO MBAYA kujua amewekwa kwenye orodha ya watu wanaohitajika sana hakujali hilo aliendelea na matukio yake ya ujambazi na pia aliona fahari kupata umaarufu hasi huo, na matukio yake mengine makubwa na maarufu aliyoyaongoza ni mwaka 2006 alifanya ujambazi jijini MOMBASA na kuua askari wawili.

Tukio hili la MOMBASA lilisikitisha na kukasirisha sana jeshi la polisi kwa kupoteza nguvu kazi yao kwa mtu hatari wanayehangaika kumtafuta usiku na mchana nchini humo, na MACHO MBAYA na genge lake walikuwa wanafanya kama kulipiza kisasi kutokana na polisi kuendesha operesheni ya kuua majambazi sugu yani hata wakiwa kwenye nafasi nzuri ya kuwakamata au kusalimu amri ni wanawaua.

Kipindi hicho KENYA ilikuwa ikisikika majambazi sugu yaliyoshindikana yameuwawa na sio kukamatwa hai na kupelekwa mahakamani, tukio lingine kubwa na maarufu MACHO MBAYA na genge lake walitekeleza mjini NJORO kaunti ya NAKURU tarehe 4 januari 2007.

Tukio lingine kubwa na maarufu zaidi ambalo lilikuwa la mwisho kwa MACHO MBAYA na genge lake nchini KENYA lilikuwa jijini MOMBASA katika benki ya HABIB tarehe 17 januari 2007 na ndo tukio la kihistoria kwa genge la MACHO MBAYA nchini KENYA.

Kihistoria kwa tukio hili, ni tukio la ujambazi ambalo genge la MACHO MBAYA waliiba fedha nyingi ambazo zilikuwa shillingi za kitanzania zaidi ya milioni 700 kwa kutowahi kuiba fedha nyingi kwa tukio moja toka kuanzisha utawala wake wa ujambazi mwaka 2003.

Tukio hili la ujambazi ndo tukio pekee kwa genge la MACHO MBAYA kutumia akili nyingi kuliko nguvu maana walikuwa na silaha ila hawakuzitumia na kuacha vyombo vya ulinzi na usalama kushindwa kung’amua akili kubwa iliyotumika na genge lake.

Tukio hili jambazi MACHO MBAYA alishirikiana na wafanyakazi ndani ya benki hiyo ambao ndo walimtaarifu tarehe 17 januari 2007 kuna fedha nyingi zinaletwa ndani ya benki hiyo jioni kabla ya benki kufungwa na wao wavizie muda huo kuondoka na mzigo mkubwa huo wa fedha.

Siku na muda kufika genge la MACHO MBAYA walifika eneo la tukio na wafanyakazi wa benki waliokula nao dili wakazima mfumo wa kamera ili tukio lisirekodiwe na muda mchache kabla ya benki kufungwa majambazi wawili wakaingia benki wakivizia kuwa wa mwisho ambapo benki huwa inafunga mlango kwa mteja mwingine yoyote asiingie ndani kwa wale wateja waliopo ndani ndo watahudumiwa wa mwisho na benki kwa siku hiyo itafungwa.

Walinzi wako nje hawajui kiendeleacho ndani na wanajua muda wa wateja kuruhusiwa kuingia benki umeisha wakawa hawana presha ya ulinzi na hali ya ulinzi mkali ikasizi huku wakisubiria kwa hamu gari la kubadilisha zamu kupita ili waondoke na wenzao wengine waingie lindo.

Sasa wakati majambazi wawili wako ndani huku nje majambazi wengine wawili kwa msaada wa wafanyakazi wa benki waliwachorea njia rahisi ya kuingilia mlango wa siri ambao unajulikana na benki ya HABIB pekee, na mlango huo unawapeleka kweye ushushaji wa fedha zilizoletwa ndani ya benki na huko kunaaminika usalama ni mkubwa sana kwahiyo hakuhitaji walinzi na mitutu yao.

Majambazi kufika kwenye ushushwaji wa fedha wakawadhibiti wahusika kimya kimya na kuchukua mzigo kiulaini na kuelekea eneo la kuhudumia wateja ambako waliwakuta wenzao wameshawaweka chini ya ulinzi watu wote waliobakia nao na kutoka wote kama wateja waliomaliza kupata huduma yao ndani na walinzi hawakuwahisi vibaya sababu wao tayari wanafikiria kuondoka majumbani kwao wakapumzike.

Tukio la ujambazi linakuja kushtukiwa tayari wakina MACHO MBAYA wameshapotea eneo la tukio bila ghasia yoyote na baadae uchunguzi kufanyika ndo vyombo vya ulinzi na usalama vikagundua genge la MACHO MBAYA limehusika na ujambazi huo kwa kushirikiana na wafanyakazi wa benki wasio waaminifu.

Jambazi MACHO MBAYA na genge lake baada ya kujulikana wamehusika tena na ujambazi mkubwa huo nguvu zaidi ziliongezwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya KENYA kupambana na genge hilo na baadhi ya vijana wake MACHO MBAYA waliuliwa na kukamatwa maana msako ulikuw hatari sana.

Huku mlengwa mkuu hapo akiwa jambazi MACHO MBAYA ambaye ndo vyombo vya ulinzi na usalama vya KENYA vilikuwa vinamtamani sana wagawane mwili wake kutokana na jinsi alivyowatesa na kuwasumbua na matukio yake ya ujambazi.

MACHO MBAYA na genge lake ambao alibakia nao walikuwa wanahama miji leo NAIROBI, kesho KISERIAN, kesho kutwa MOMBASA n.k, ni hawatulii sehemu moja kuhofia kukamatwa au kuuliwa na wakati MACHO MBAYA na wenzie wanahama hama hivyo vichwani mwao kukazaliwa wazo kwanini wasihamishe harakati zao za ujambazi nchi jirani ambayo ni TANZANIA.

Pia matokeo mazuri ya matukio ya ujambazi yaliyokuwa yanafanywa na majambazi wenzao WAKENYA huko nchini TANZANIA kwa kushirikiana na wazawa wa huko walikuwa wakiyasikia sana yakitekelezwa na kufanikiwa katika mikoa ya ARUSHA, KILIMANJARO na DAR ES SALAAM, sasa wakaona kwanini na wao wasiwe sehemu ya historia hiyo ya majambazi WAKENYA kutekeleza na kufanikiwa matukio yao ya ujambazi nchini TANZANIA .

Wao wakina MACHO MBAYA walijua wakihamia huko watakuwa kama wamezaliwa upya sababu hawana rekodi yoyote ya ujambazi nchini TANZANIA wala kutafutwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya TANZANIA, na hapa kuzaliwa wazo la kuhamia nchini TANZANIA ndo mwanzo wa kuzaliwa wazo la ujambazi mkubwa benki ya NMB wilayani MWANGA mkoani KILIMANJARO.

Wazo la kuhamia nchini TANZANIA limezaliwa ila kukubaliana kwa genge la MACHO MBAYA ilikuwa bado na nani atakuwa mwenyeji wao nchini TANZANIA ni moja ya swali gumu sana kwao maana majambazi wote wa KENYA wanaokuja kutekeleza matukio yao ya ujambazi nchini TANZANIA au mataifa mengine jirani lazima wawe na wenyeji.

Sio rahisi wao wenyewe waamke na kuhamia nchini TANZANIA au nchi nyingine na kujiongoza kutekeleza ujambazi sababu wanakuwa wageni na muda wa kukaa na kuzoe mazingira ili wawe wenyeji hawana sababu ya haraka kutaka kufanya matukio yao ya ujambazi au kuhofia kuhisiwa vibaya na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi husika waliyokwenda.

Sababu bado genge la MACHO MBAYA hawajakubaliana kwahiyo swali gumu hilo la mwenyeji wao nchini TANZANIA kulipuuzia kwanza mpaka wazo lipitishwe na wote, genge la MACHO MBAYA wakakaa kikao kujadili wazo lililozaliwa kwa kuangalia faida na hasara za kuhamisha harakati zao za ujambazi nchini TANZANIA.

Pia kuangalia nchi mbadala kama TANZANIA itakuwa na hasara nyingi upande wao na kikao kizito kukaliwa na majadaliano ya hapa na pale kwa kila mwanagenge wa MACHO MBAYA kutoa uzoefu wake juu ya taifa la TANZANIA kwa namna anavyolijua basi mwishoe wazo likapitishwa kwa wote watahamia nchini TANZANIA kuwaletea vita maana ujambazi wao ni kama vita afe kipa afe beki
Unamjua bwana SAITO. AU SAITOTI?
 
Usije kuta na wewe ni mhalifu mbona una details namna hii? anyway ni jokes tu ila umejitahidi sana kutuhabarisha sema kuna sehemu ulikuwa unarudia rudia.
Hii inafaaa kabisa kutengenezewa filamu hii ni kama mapambano ya kikomandoo.
Kwa nchi za wenzetu matukio ya kutisha kama haya yakitokea yanatengenezewa filamu yake na serikali wanatoa kibali.
Kwa kufanya hivyo haimanishi ni kufundisha watu uhalifu bali pia majeshi yetu ya usalama nayo katika medani zao yanajua mbinu nyingi na kuzidi kujizatiti kupunguza au kuuondoa huo uhalifu.
Kuna jamaa mmoja Marekani jambazi liliteka ndege na mabulungutu ya hela nitatafuta jina lake baadae nitarudi niweke habari zake hapa.
Jamaa alitumia ujambazi akiwa peke yake kwa kutumia akili nyingi mno aliruka na parachute polisi wamehangaika miaka na miaka kutatafuta lakini hawajampata hadi leo imepita miaka mingi sana na katika harakati zake hakuua mtu yeyote.
Toka siku hiyo alionekana shujaa na hata majeshi ya usalama walikuwa wanatumia tukio lake kwenye mafunzo yao na hata mashirika ya ndege kuna mlango unaitwa jina la huyo jambazo ngoja nitarudi baade kidogo niongezee.
 
Usije kuta na wewe ni mhalifu mbona una details namna hii? anyway ni jokes tu ila umejitahidi sana kutuhabarisha sema kuna sehemu ulikuwa unarudia rudia.
Hii inafaaa kabisa kutengenezewa filamu hii ni kama mapambano ya kikomandoo.
Kwa nchi za wenzetu matukio ya kutisha kama haya yakitokea yanatengenezewa filamu yake na serikali wanatoa kibali.
Kwa kufanya hivyo haimanishi ni kufundisha watu uhalifu bali pia majeshi yetu ya usalama nayo katika medani zao yanajua mbinu nyingi na kuzidi kujizatiti kupunguza au kuuondoa huo uhalifu.
Kuna jamaa mmoja Marekani jambazi liliteka ndege na mabulungutu ya hela nitatafuta jina lake baadae nitarudi niweke habari zake hapa.
Jamaa alitumia ujambazi akiwa peke yake kwa kutumia akili nyingi mno aliruka na parachute polisi wamehangaika miaka na miaka kutatafuta lakini hawajampata hadi leo imepita miaka mingi sana na katika harakati zake hakuua mtu yeyote.
Toka siku hiyo alionekana shujaa na hata majeshi ya usalama walikuwa wanatumia tukio lake kwenye mafunzo yao na hata mashirika ya ndege kuna mlango unaitwa jina la huyo jambazo ngoja nitarudi baade kidogo niongezee.
D.B Cooper Uzi wake umo humu umeelezewa vzuri story yake inasisimua
 
Unamjua bwana SAITO. AU SAITOTI?
Tukio la Njiro nalikumbuka vyema Maana nilikuwa miongoni mwa wananchi waliojaa kushuhudia. Ni kweli DC alikuwa Kepten Evans Balama na Mkuu wa mkoa alikuwa Ndomba ambaye baadaye akateuliwa kuwa mnadhimu wa JWTZ.
Ila siku Ile kulikuwa na weaknesses kwa vikosi vyetu hasa decisions nini kifanyike..
Hasa baada ya kufika JWTZ wao walitaka tuu kulipua nyumba na hizo rpg..
Naelewa huyu anasema hiki, huyu vile, wananchi kelele, mzazi wa binti yowe, DC, Rc... Kulikuwa na sintofahamu kidogo Maana tukio lilikuwa sio la kawaida.
Ila at the end hekima ndio ilishinda mpaka kuwatoa humo ndani wakiwa hai.

Hongera sana vyombo vya ulinzi na usalama kwa ku risk maisha kiasi kile.
 
D.B Cooper Uzi wake umo humu umeelezewa vzuri story yake inasisimua
Ni kweli bwana Kipozi nimeona hadi picha yake yakuchora.D.B Cooper alipata umaarufu hadi leo kwenye ndege kuna kifaa kimetengenezwa maalum kwa ajili ya kuzuiya mlango wa ndege usifunguke ikiwa angani wamekipa kifaa hicho heshima ya huyu jamaa kinaitwa Cooper vane.
Kila mwaka mwezi wa 11 mjini Portland kuna sherehe maalum inafanywa na mashirika ya ndege kusherehekea tukio la huyo jambazi ambapo uchunguzi wake umechukua miaka 45 hadi wakaamua kuacha rasmi mwaka 2016.Tukio lenyewe lilifanyika mwaka 1971.
Hadi leo hii hawajampata huyu mtu mwenye akili nyingi kwa kuiba kwenye ndege na kuruka na parachute na bila kuua mtu yeyote badala ya kumuona jambazi ameonekana ni shujaa.
Ndio maana nikatoa wazo matukio kama haya ni vizuri yakatengenezewa filamu ili mashirika ya ujasusi na polisi wapate cha kujifunza ili kujizatiti kwenye usalama.
Hii hadithi ya D.B Cooper kama mtu anataka kuisoma ilitolewa na Msingidan humu andika maneno haya kwenye find kisha fungua tafuta ni hadithi ya kuvutia.
haya fungua haya maneno chini kwenye JF Someni kisa hiki cha kusisimua
B.D. Cooper, Mtekaji wa ndege aliyetafutwa na FBI zaidi ya miaka 45 bila kuonekana

ngoja niwawekee na picha ya D.B Cooper
 

Attachments

  • cooper.jpg
    cooper.jpg
    213.4 KB · Views: 74
Duuh..nasikia kuna hela zingine zilipotea humo humo kwenye nazingira ya kutatanisha....
 
Uzi una point chache maneno yasiyohitajika yamekuwa mengi mno nimeshindwa kuumaliza
 
Kama nimekuelewa vizuri umeandika kwamba una kitabu juu ya ishu hii na bila shaka hiki ni kipande cha hicho kitabu chako. I'la br mwandiko wako ni wa kushangaza sana. Unachanganya herufi ukifanya msisitizo was maneno kama Njeru, Saitoti, ama Macho Mbaya kama mfano.
Sijaona haja ya kuandika kwa herufi kubwa.
Nb.
Story ni nzuri.
 
kwanza anavyoandika ni hovyo ,mpaka aelezee kilichotokea atazunguka sana na kuingia kwingine ,ana mtindo mbovu sana wa uandishi au wa kizee
Acha roho mbaya na wivu mkuu😄😄
Mkuu Ijue Historia umenishangaza sana na hii story, kuna details umeziongea sikutegemea mtu wa kawaida azijue kama ulivyomtaja Kim na dungu....
Hii imenifanya nikuhisi kwamba either ww ni mpelelezi kwenye hiyo kesi au ulikua mahakamani....

Nikurekebishe tu vitu vichache...yule Mama Manager Hakua kabisa kwenye original plan yule alienda kuamshwa maana alikua anakaa hapo hapo bank ..na ndio alikua na funguo...za strong room...

Macho Mbaya jina lake la huku TZ tulikua tunamwita seymo...Kim alikua mshkaji wake sana....
Yule askari ndie alietoa mchongo na aliwapa watz..watz wakawatafuta wa k...ndio movie ikaanza..

Kama kuna details unataka kuijua ujazie kwenye story niulize dm nitakupa ili story ikae poa kuna details nyingi sana umeziruka au kudistort..naweza kukusaidia kuziweka sawa

By the way umenikumbusha mbali...sana...😄
Nnawenge huyu mwamba atakuwa Usarama
 
Back
Top Bottom