Mwadilifu Mdhulumiwa
JF-Expert Member
- Jul 22, 2021
- 419
- 640
Ajali za moto katika jamii yetu zimekuwa ni majanga yanayohitaji mjadala makini kutokana na athari kubwa yanazosababisha pindi yanapozuka katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika taasis za umma kama vile vyuo, mashule na katika vituo vya biashara kama vile masoko na maeneo mengine.
Athari zake huweza kuwa kubwa zaidi hasa yanapotokea nyakati za usiku wa manane ambapo msaada huwa ni mdogo. Athari hizi ni pamoja na kusababisha vifo vya wahanga wa tukio na pia uharibifu mkubwa wa mali unaoleta hasara kubwa za ghafla.
Mathalani katika tukio la moto lililotokea mwezi Agosti 2019 mkoani Morogoro, ambapo lori la mafuta liliporipuka na kusababisha vifo vya raia wenzetu zaidi ya 100. Huku wengine wakibakia na ulemavu wa viungo.
Yapo pia masoko yaliyoteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa kwa wafananchi na wafanya biashara, kama vile Soko la Mwanjelwa (Mbeya), Soko la Mandela (Sumbawanga), Soko la Kariakoo(Dar Es salaam), Soko kuu la Mpanda (Katavi) na mikoa mingine.
Kuendelea kutokea kwa majanga haya ya moto kunadhihirisha wazi kuwa kama taifa bado hatujalipa suala hili umaanani na uzito linaostahili.
Bado tunalichukulia suala hili kama jambo la dharura ama linalotokea kwa bahati mbaya na hivyo likipita yanasemwa mawaidha machache, wakukamatwa anakamatwa, wakufukuzwa au kuathibiwa anaadhibiwa kisha kila mmoja anaendelea na shughuli zake.
Katika makala haya nitajadili sababu zinazochangia kuendelea kutokea kwa majanga ya moto na mbinu za kuyaepuka au kukabiliana nayo.
Sababu Za Kuzuka Kwa Majanga Ya Moto;-
Zipo sababu kadhaa zinazopelekea kuendelea kuzuka kwa majanga ya moto nchini. Miongoni mwa sababu hizi ni pamoja na:-
Ajali za moto zimekuwa ni chanzo cha vifo na uharibifu wa mali unaosababisha hasara kubwa za bila kutegemea na hivyo kurudisha nyuma maendeleo binafsi ya wananchi na taifa zima kwa ujumla.
Hivyo ni wakati sasa kwa serikali kulichukulia janga hili kwa uzito unaostahili na kulipatia ufumbuzi wa kudumu. Mkazo zaidi uwekwe katika kutunga sera na sheria kali dhidi ya uzembe wowote utakaosababisha ajali ya moto sambamba na kutoa elimu kwa makundi yote ya kijamii kuishi kwa kuzingatia tahadhari zote za moto.
Wito kwenu wananchi na jamii nzima kwa ujumla kila mmoja ajione ni mdau muhimu na ashiriki moja kwa moja katika kupambana na janga hili.

- Ukosefu wa elimu ya majanga ya moto.
- Hali hii husababisha watu kujisahau wanapokuwa katika mazingira hatarishi ya kusababisha moto na hivyo ujinga wao kuwa sehemu ya chanzo cha mlipuko wa moto husika.
- Mathalani katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro mwezi Agosti 2019 na kupelekea vifo vya zaidi ya wananchi 100, Uchunguzi unaonyesha kuwa moto ulilipuka kutokana na mmoja wa wananchi kutikisa nyaya za betri ya lolri lile wakati wakigombea mafuta yaliyokuwa yakimiminika toka kwenye tanki la lori hilo lililokuwa limepata ajali , kitendo cha kushika nyaya za betri kilisababisha cheche ambazo zilidakwa na mafuta na hivyo kuzua moto ulioripuka na kuenea katika eneo lote yalipokuwa yamemwagika mafuta yale.
- Baadhi ya wanachi kukosa uelewa juu uhifadhi wa mazingira.
- Katika maeneo mengi ya vijijini kumekuwapo na matukio mengi ya uchomaji hovyo wa misitu na mapori yanayozunguka maeneo hayo. Wananchi hao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo ili kutafta wanyama kwa ajili ya kitoweo au kusafisha maeneo kwa ajili ya kilimo au kuazisha makazi mapya. Vitendo hivi vimekuwa vikiambatana na uharibifu mkubwa wa maliasili zetu ikiwemo kutoweka kwa wanyama na uoto mzuri wa asili.
- Uthibiti mdogo katika fani za ufundi umeme na mitambo.
- Katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka mafundi wengi wa umeme na mitambo wasiokuwa na ujuzi wa kutosha, ambao wamekuwa wakitengeneza miundombinu ya umeme na mitambo mbalimbali kiwemo ya gesi kwa wananchi wengi. Kutokana na ufundi wao mbovu wamekuwa wakitengeneza miundombinu hiyo bila kuweka tahadhari ya moto. Hivyo miundombinu hiyo imekuwa ikipata hitilafu za mara kwa mara na kusababisha moto kuripuka katika maeneo hayo.
- Ukosefu wa vifaa na njia za kisasa za kuishi kwa tahadhari ya moto
- Katika maeneo mengi ya umma kumekuwa hakuna tahadhari ya kutosha ili kuepuka majanga ya moto. Mathalani katika maeneo mengi hakuna vikosi maalumu katika eneo husika vinavyokuwa na jukumu la kuyalinda mazingira husika na moto wowote unaoweza kujitokeza. Aidha vifaa kama Fire Alarms, ambavyo ni muhimu kwa ajili kutoa taarifa juu ya hatari ya uwepo moto katika mazingira husika navyo vimengwa maeneo machache sana.
- Kukosekana kwa taasisi imara na yenye mtandao mpana wa kupambana na moto.
- Mpaka sasa katika Tanzania nzima taasisi inayohusika na majanga ya moto ni kitengo cha jeshi la zimamoto kilichomo ndani ya jeshi la polisi. Pamoja na kuwa jeshi la polisi lina mtandao nchi nzima, lakini kiuhalisia kitengo cha zimamoto bado hakijawezeshwa vyakutosha kuweza kukidhi mahitaji. Yanapozuka majanga ya moto jeshi la zimamoto huchelewa kupeleka vifaa vya kuzimia moto na sehemu nyingine vifaa hivi hukosekana kabisa kutokana na kuwa mbali mno na tukio la moto lilipotokea.
- Gharama kubwa za vifaa vya kupambana na moto
- Vifaa vya kisasa vya kuzimia moto kwa kutumia gesi vimekuwa vikiuzwa gharama kubwa ambazo wananchi wengi wamekuwa wanashindwa kununua vifaa hivyo na kuishi navyo majumbani kwao ikiwa ni tahadhari dhidi ya moto wowote utakazuka ndani au nje ya nyumba zao. Hali hii imekuwa ikisababisha moto mdogo ambao ungeweza kuthibitiwa mapema, kukuwa na kuwa mkubwa usiothibitika kirahisi.
- Hivyo kuleta madhara makubwa ambayo yangeweza kuepukika kama moto husika ungethibitiwa mapema.
- Urasimu uliopo ndani ya jeshi la zimamoto
- Kuna baadhi ya watendaji katika jeshi la zimamoto nchini, hasa matawi ya mikoani wanapopewa taarifa ya kuwepo kwa tukio la moto, huanza kutoa sababu kadhaa huku nyingine zikiwa ni za uwongo ili tu kutaka rushwa au kukwepa majukumu na uwajibikaji. Mathalani unaweza kutoa taarifa ya moto mapema tu, lakini ukaambiwa gari haina mafuta hivyo rusha pesa ya kununulia mafuta ili gari ikachukuwe maji, Mara utaambiwa dereva hayupo au ni mgonjwa na nyinginezo zinazofanana na hizo.
- Wananchi wengi kufanya shughuli zao bila kuchukua tahadhari ya moto
- Suala la tahadhari ya moto limekuwa likipuuzwa na wananchi wengi wanapokuwa katika maemeo ya shughuli zao za kiuchumi licha ya kuwa katika hatari ya moto. Maeneo haya ni pamoja na masoko ya biashara na vituo vya uzalishaji bidhaa na malighafi za aina mbalimbali.
Mathalani utakuta mpaka leo kwenye masoko mengi vibanda vingi vimejengwa kwa miti na mbao kavu huku pia vikiwa vimerundikana na kubanana huku vimeunganishwa na vibanda vinavyotumia moto. - Utovu wa nidhamu katika taasisi za kijamii hasa mashuleni na vyuoni
- Uthibiti mdogo wa vitendo vya utovu wa nidhamu mashuleni na vyuoni umekuwa ni chanzo cha vyuo na mashule mengi nchini kuchomwa moto na wanafunzi wanaosoma hapohapo.
- Kuna taasisi zingine vitendo hivi vinajirudia mara kadhaa katika taasisi moja kama ilivyojitokeza katika shule ya Sekondari ya Geita huko mkoani Geita na hivyo kuleta hasara kubwa na kusababisha shule kufungwa na kusitisha huduma.
- Serikali na jamii nzima kwa ujumla tuwekeze vya kutosha katika kuelimishana juu ya kuepuka mazingira na vitendo vyote vinavyoweza kusababisha moto.
- Zitungwe sheria kali dhidi ya mafundi holela wa umeme na mitambo ya aina mbalimbali, leseni zitolewe kwa wale tu wenye sifa na vigezo vya kutosha.
- Serikali kwa kushirikiana na wadau wote iweke utaratibu wa kuhakiki vifaa vya kisasa vya kutoa taarifa ya moto vinafungwa kila taasisi au kituo cha shughuli zozote za kiuchumi na pawepo na kikosi cha usalama wa eneo kitakachokuwa maalumu kwa moto tu na kuwe na mbadilishano(shifting) utakaowezesha ulinzi wa masaa 24.
- Wahusika wawe ni wadau wa hapohapo ili kupunguza gharama. Mfano mashuleni na vyuoni wawe ni wanafunzi na kwenye masoko ya biashara wahusike wafanya biashara wenyewe.
- Jeshi la zimamoto lifumuliwe na badala yake Serikali ianzishe wizara maalum kwa ajili ya majanga ya dharura.
- Wizara hii iwezeshwe vyakutosha kwa mbinu na vifaa vya kisasa ili ibebe pia jukumu la kushughulikia majanga ya moto kwa uzito unaostahili. Chini ya wizara hii vianzishwe vikosi kazi vya sungusungu wa moto kila mtaa nchini kote.
- Serikali itowe ruzuku kwa viwanda na makampuni yote yanayouza vifaa vya kupambana na moto ili kuwezesha vifaa hivyo kupatikana kwa gharama nafuu ili wananchi wengi waweze kuvinunua na kuwa navyo majumbani kwao kama tahadhari dhidi ya moto.
- Serikali itunge sheria kali zitazokomesha vitendo vya utovu wa nidhamu na migogoro inayosababisha wanafunzi kuchoma moto shule na vyuo.
- Serikali ianzishe utaratibu wa kuadhimisha siku ya moto kitaifa kila mwezi ambapo siku hiyo yawe yanaitishwa makongamano nchi nzima yenye kuhamasisha jamii njia mathubuti za mapambano dhidi ya moto.

Upvote
1