Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Mboga za majani huchangia sehem ndogo sana ya mlo wa watanzania wengi.Naamini moja kati ya mambo yanayofanya watu wengi hawapendi mboga za majani nipamoja na upishi mbaya wa mboga.
Majani ya kunde ni mboga ya kawaida sana,na makabila mengi hapa nchini yana njia namna mbalimbali za kupika mbaga hii.
Kule ujaluoni kwa mfano.Majani ya kunde huchemshwa kwa muda mrefu sana,yanawekewa maziwa mengi wakati wa kuchemshwa na
huachwa yalale siku moja kabla ya kuliwa upishi huu ni mzuri sana,kwani mboga huwa na ladha nzuri sana na wingi wa virutubisho kutoka kwenye maziwa.
Nisichopenda kwenye upishi huo,ni uchemshaji wa muda mrefu sana ambao kwa upande mwingine ni wamuhim kwani majani ya kunde ni magumu,na ugumu huo huongezeka pale majani yanapokomaa.
Kwakua napenda upishi wa wajaluo wa majani ya kunde,nimefanya marekebisho kidogo ya pishi lao ili kulipa wepesi wa kupika.
Mahitaji
1.Chemsha maji kidogo kwenye sufuria adi yatokote,weka majani ya kunde,chemsha adi yaive na maji yakauke.
2.Katika sufuria,unga mafuta na vitunguu,vikikaribia kuiva ongeza binzari nyembamba na ivisha pamoja. Ongeza nyanya na nyanya ya kopo,Kaanga adi nyanya na mafuta vitengane kwenye sufuria.
3.Ongeza majani ya kunde(yasiwena maji kabisa ) na chumvi kaanga kwa muda kidogo ili mboga na nyanya vishikane.Ongeza maziwa ,geuza kila mara adi maziwa yapungue na mboga iwe nzito.Tayari kw akula.
-Pishi hili sijaliwekea vipimo.Pima kila kitu kwa kuzingatia wingi wa mboga yako.
Maelezo ya ziada

- Majani ya kunde machanga
- Vitunguu
- Binzari nyembamba(jira)-ukipenda
- Nyanya
- Nyanya ya kopo
- Maziwa fresh
- Mafuta
- Chumvi
1.Chemsha maji kidogo kwenye sufuria adi yatokote,weka majani ya kunde,chemsha adi yaive na maji yakauke.
2.Katika sufuria,unga mafuta na vitunguu,vikikaribia kuiva ongeza binzari nyembamba na ivisha pamoja. Ongeza nyanya na nyanya ya kopo,Kaanga adi nyanya na mafuta vitengane kwenye sufuria.
3.Ongeza majani ya kunde(yasiwena maji kabisa ) na chumvi kaanga kwa muda kidogo ili mboga na nyanya vishikane.Ongeza maziwa ,geuza kila mara adi maziwa yapungue na mboga iwe nzito.Tayari kw akula.
-Pishi hili sijaliwekea vipimo.Pima kila kitu kwa kuzingatia wingi wa mboga yako.
Maelezo ya ziada
- kuchemsha majani ya kunde kwenye maji ya mototo kunafanya yaive kwa haraka na yasipoteze rangi yake.
- Jir/binzari nyembamba ni moja kati ya viungo vichache ambavyo harufu na ladha yake hupendeza sana kwenye mboga za majani.Si lazima kuweka ila nashauri ujaribu ili uone tofauti.
- Ni vyema kutumia majani machanga kwasababu ni laini,huitaji kuchemsha kwa muda mrefu hivyo hayapotezi virutubisho.
- Majani ya Kunde ni moja kati ya mboga zenye rangi ya kijani iliyokooza/kolea,Mboga hizi husifika kwa kubeba virutubisho vingi,hasa Madini .