Majaribio ya kumuua Mobutu

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,774
Reaction score
47,866
Mnamo mwaka 1986 rais wa zaire marechal mobutu sese seko anaamua kuunda kikosi maalumu cha ulinzi wake binafsi kilichojulikana kama Division Spéciale Présidentielle (special presidential division/ Dsp)

Kikosi hiki cha jeshi kina wanajeshi wanao kadiriwa kufikia elfu 10, wengi wao kutoka kabila la mobutu la ngbandi
Wanajeshi hawa wanapewa mafunzo nchini israel ,pamoja na vifaa vya kisasa kabisa

Itakumbukwa kuwa kabla ya mobutu ,congo iliongozwa na rais wake wa kwanza aliyeitwa joseph kasavubu, huyu alilindwa na mwanajeshi mmoja au wawili na hakuwa na msafara bali gari moja tu mara nyingi alipokua akitembea

Wanajeshi wa DSP walilipwa vizuri mno na mara kwa mara na mobutu na aliwaamini,mara nyingi kila alipoenda kuishi kijijini kwake (badae kukawa mji) huko gbadolite alisindikizwa na wanajeshi mia tatu kwa ulinzi

MAJARIBIO YA KUMUUA MOBUTU

Ijumaa ya tarehe 16/5/1997 mobutu anusurika kufa

Wakati akiwa uwanja wa ndege wa ndiji akiwa anaondoka jiji la kinshasa mobutu yumo ndani ya ndege,dakika za mwisho ndege iruke mkuu wa usalama wa mobutu kanali motoko anapokea taarifa ya kiintelijensia kuwa pembeni ya uwanja wa ndege kwenye shamba kubwa kuna gari la jeshi aina ya jeep likiwa na ground to air missile kwa ajili ya kudungua ndege ya mobutu

Kanali motoko anamwambia rubani wa ndege ya rais abadili uelekeo wa kurusha ndege
Rubani anakataa kwa kudai upepo hauruhusu kufanya hivo, motoko anamwambia mobutu, mobutu anawaambia marubani "fanyeni anavyotaka"

Ndege inabadili uelekeo,wale wanajeshi waliokua wakimsubiri wamtungue wanahaha kukimbia karibu ndege inakorukia ili waitungue ,katika kufanya hivo wanapata ajali na kufa papo hapo,mobutu anaenda gbadolite

JARIBIO LA PILI CHATEAU DU KAWELE( kasri la kawele)

Pembeni kidogo ya mji wa gbadolite, juu kabisa ya mlima,mobutu alijenga jumba la kifahari lenye kitanda cha remote, kama mobutu hajalala kinakua kama swimming pool,akibonyeza remote maji yanaachana kitanda kinapanda juu kutoka ardhini mobutu analala

Sasa baada ya kufika hapa kawele .anakuja mwanajeshi mmoja anamuulizia mobutu getini kutoka kikosi cha DSP anadai anaujumbe kutoka kwa jenerali nzimbi kwa mobutu

Kanali motoko anakataa huyo mwanajeshi kumuona mobutu ,anamwambia "nipe ujumbe huo nitampa marechal mimi mwenyewe"

Yule mwanajeshi anakataa .inabidi akaguliwe mwili mzima haraka na kukutwa kajifunga mabomu anaulizwa ya nini ?
Anaamua afunguke anasema alitaka kujilipua ajitoe muhanga ili afe mobutu
Alitumwa na nani ? Wakuu wa kikosi cha DSP

mwanajeshi huyu aparently alipigwa sana. na alimuomba mobutu msamaha
Kilichofata sijajua ila huenda alipigwa risasi

JARIBIO LINGINE LA KUMUUA MOBUTU,MOANDA AIRPORT

Hali inakua mbaya mno (hapa nafupisha)
Msaidizi wa mlinzi mkuu wa mobutu
Major ngani yanda mokomba
Anafanya patrol (mobutu alimkataza ila yeye akaondoka)
Huko njiani anakutana na kikosi cha DSP kinarudi gbadolite huku wanaimba (mobutu msaliti,ndugu yake nzimbi amekimbilia brazaville katuacha sisi tufe,twendeni tukamkamate mobutu huko kawele)

Major ngani anarudi kawele haraka na kumuuliza boss wake
Marechal yuko wapi ? Inabidi tutoloke
Kanali motoko:emu jaribu wewe labda utaweza mi nimemwambia tukimbie anasema tumchukue mkewe na pacha wa mkewe , yeye tumuache afie hapa

Major ngani anaenda mpaka chumba cha mobutu anamkuta mobutu kavaa yale mashati yake bila vesti na viatu bila soksi

Anamwambia watoloke,mobutu anakataa anadai anataka kufia nyumbani

Major ngani anambeba mobutu mgongoni (baada ya kumuomba samahani sababu hairuhusiwi mlinzi wa rais kumshika rais)

Mobutu anabebwa mgongoni (aliumwa prostate cancer hivo hakuweza kusimama)

Huko airport major ngani aliiteka ndege ya urussi iliyokuwa imeleta vifaa vya kijeshi kwa jonas savimbi( huyu alikua ni guerrila wa angola rafiki wa mobutu)

Kwanini major ngani aiteke ndege ya jeshi la urusi akati rais hua ana ndege ?

Hili ni swali ambalo wengi mnajiuliza,ila jibu ni kuwa
Uzi uliopita nilimzungumzia kongolu mobutu,huyu alikimbilia brazzaville hivyo akamuambia baba yake "baba tumekwama huku brazzavillle"
Mobutu akatuma ndege yake ikamchukue mwanae,ilivofika huko ilikataliwa na serikali ya brazaville

Hivyo mobutu akabaki bila ndege

Ndio maana ikabidi msaidizi wa mkuu wake wa ulinzi aiteke ndege pekee pale uwanja wa ndege ili kumtorosha mobutu

Mobutu akaingizwa kwenye yale mandege makubwa ya kivita yeye na gari lake kwa sababu zile ndege hazina viti

Wakati inaruka,kikosi cha DSP kikaingia uwanja wa ndege na kumrushia mobutu mabomu na risasi
Akiwa anaumwa sana na mwenye mawazo,mobutu akamuambia daktari wake "hii sio zaire yangu tena ,sina tena cha kuifanyia nchi hii"

Mobutu aliondoka mpaka rome ambako alipokelewa na rafiki yake wa muda mrefu ,na badae akaenda morocco ambapo alipokelewa na king hassan
Mobutu alikaa huko muda mfupi akafa kwa internal bleeding
Alikufa akiwa na chini ya kilo 40 akiwa hana damu kabisa



Haya ni ya mwezi may mwaka 1997, kuna uwezekano mkubwa yapo mengi
 
Kabila Snr kaingia ofisi 17May 1997 ,means mambo yalikwisha haribika hadi hapo
 
Mobutu alikuwa gwiji wa ndumba Kama walivo madikteta wote,lkn pamoja na yote ikiwemo walinzi walishindwa kumuokoa asipinduliwe.
Kweli kabisa
Walinzi walimuibia mno miaka ya mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…