Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Vyombo vya Habari vya serikali nchini Korea Kaskazini vimetoa picha zinazosema kuwa zilichukuliwa kutokana na majaribio ya kombora lake kubwa zaidi kutoka mwaka 2017.
Picha hizo zinaonesha sehemu za rasi ya Korea na maeneo yaliyo karibu yakionekana kutoka angani.
Korea Kaskazini ilisema kuwa kombora hilo lilikuwa la masafa ya kati ya Hwasong-12.
Korea Kusini na Japan zilisema lilifikia umbali wa kilomita 2,000 (maili 1,242) kabla ya kuanguka kwenye maji kutoka Japan. Nchi zote mbili zimeshutumu jaribio hilo, ambalo ni la saba mwezi huu.
Picha hizo, zilizotolewa na shirika la kitaifa la habari la Korea Kaskazini, KCNA, ziliripotiwa kupigwa kwa kutumia kamera zilizowekwa kwenye kichwa cha kombora lililofanyiwa majaribio.
Picha mbili za kurusha kombora la Korea Kaskazini na mbili za Dunia zilizochukuliwa kutoka kwenye kombora hilo angani ambazo zinaonyesha wakati wa kurushwa na nyingine inaonyesha kombora likiwa katikati ya safari, iliyopigwa kutoka juu.
Maafisa wa Japan na Korea Kusini wanakadiria kuwa kombora hilo lilipaa kwa dakika 30 kwa umbali wa kilomita 800.
Credit: Star TV