Majaribio ya SGR kutoka DSM - Morogoro kufanyika February 2023

Majaribio ya SGR kutoka DSM - Morogoro kufanyika February 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linatarajia kuanza majaribio ya kutoa huduma katika Reli ya Kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro mwezi Februari 2023

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alisema kazi ya ujenzi wa SGR, awamu ya kwanza kilometa 1,219 kati ya Dar es Salaam na Mwanza na kwamba kipande cha Dar es Salaam – Morogoro kilometa 300 imefikia asilimia 99.77.

Msigwa aliwaeleza waandishi wa habari Dodoma kuwa lipande cha Morogoro – Makutupora kilometa 422 kazi imefikia asilimia 91.79, kipande cha Makutupora – Tabora kilometa 368 kazi imefikia asilimia 3.95 na kipande cha Tabora – Isaka kilometa 165 kazi imeanza.

Alisema kipande cha Isaka – Mwanza kilometa 341 ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 22.71.
“Awamu hii ya kwanza pekee inatarajiwa kugharimu Sh trilioni 16. Na kati ya fedha hizo tayari, serikali imeshatoa kuwalipa wakandarasi kiasi cha Sh trilioni 8.143,” alisema.

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

Alisema awamu ya pili itahusisha kipande cha Tabora – Kigoma, kilometa 506 zinazojumuisha njia kuu za kilometa 411 na mapishano kilometa 95 na kwamba mkataba wa ujenzi umesainiwa na wakandarasi wapo eneo la mradi.

Msigwa alisema kipande cha Uvinza – Msongati – Gitega kilometa 367, mchakato wa ununuzi kwa ajili ya kupata wakandarasi unaendelea na kipande cha Isaka – Rusumo – Kigali, kilometa 365 serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi.

“Huu ni mradi mkubwa ambao sio tu utainufaisha nchi yetu kwa mapato makubwa ya bandari, usafirishaji na ajira bali pia utasaidia kulifungua kibiashara eneo hili la maziwa makuu na hivyo kuboresha maisha ya wananchi,” alisema.

Kuhusu ununuzi wa mabehewa alisema 14 mapya yaliyotengenezwa Korea Kusini yamewasili nchini na yanasubiriwa mabehewa 45.

Alisema vichwa 17 vya treni za umeme na seti za treni aina EMU 10 vinaendelea kutengenezwa Korea Kusini kwa mkataba wa miezi 34 unaogharimu dola za Marekani milioni 295.74 (takribani Sh bilioni 680).

Msigwa lisema pia yameagizwa mabehewa 1,430 ya mizigo kwa mkataba wa unaogharimu dola za Marekani milioni 127.2 (sawa na takribani sh bilioni 292 za Tanzania.

HABARI MAELEZO
 
Siasa tupu. Mabehewa mmeshaleta na nini ya umeme ama.
 
Njia Ya Muongo Ni Fupi
Muongo Muongoze
Zilongwa Mbali, Zitendwa Mbali

Kila Mwaka Mnakuja Na Jipya, Yaani Mnavyozidi Kupanua Ndiyo Wanavyozidi Kutamani, Hayo Ndiyo Maendeleo
By Mama Wa Mboga
 
Haya sasa February hiyo hapo bado wiki mbili, tuone uongo wao.
 
Hayo ni Majaribio yapi tena? Mabehewa yakiwa na Abiria wa kulipia, au Abiria Mainjinia Mawaziri, makatibu wakuu na CCM kwa ujumla?

Mada haijitoshelezi na taarifa inayo ambatana nayo.

Habari na Maelezo??
 
Deal ya mabehewa ya kizamani itawatesa sana hao..... Haiingii akilini karne hii kufanya majaribio ya mangongo ya kizamani kwenye reli mpya na teknolojia ya kisasa.....

Hovyo kabisa! 😡
 
Deal ya mabehewa ya kizamani itawatesa sana hao..... Haiingii akilini karne hii kufanya majaribio ya mangongo ya kizamani kwenye reli mpya na teknolojia ya kisasa.....

Hovyo kabisa! 😡
🤣🤣😂🤣
 
Back
Top Bottom