Majasusi wa Urusi (FSB) wambaini M-Ukraine aliyetega bomu Urusi na kumuua binti mwandishi wa habari (Darya Dugina)

Majasusi wa Urusi (FSB) wambaini M-Ukraine aliyetega bomu Urusi na kumuua binti mwandishi wa habari (Darya Dugina)

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2019
Posts
2,926
Reaction score
15,634
Shirika la kijasusi la Urusi (FSB) limembaini raia wa Ukraine aliyetega bomu kwenye gari Urusi na kumuua binti mwanadishi wa habari aitwaye Darya Dugina.

Chombo hicho cha upelelezi cha Urusi kimechapisha video iliyokusanya matukio kadhaa ikimuonesha raia wa Ukraine wa kike kwa jina la Natalya Vovk akiingia Urusi na mtoto wake wa kike (teenager), akiingia pia kwenye jengo alilokuwa akiishi Darya (mwandishi wa habari aliyeuawa), kisha ikimuonesha akiondoa kwa haraka mno mara baada ya bomu kulipuka na kumuua Darya.

Binti huyo muuaji aliingia Urusi July 23 akiwa na gari lenye number plate ya Jamuhuri ya Watu wa Donetsk (ili kukwepa kuchunguzwa zaidi), alipokuwa Urusi akabadili na number plate ya Kazakhstan, nchi rafiki ya Urusi. Baada ya shambulio, siku ya jumapili (19 August) akaondoka Urusi kuelekea Estonia akitumia number plate ya Ukraine. Binti huyo ni askari ktk kikosi cha neo-Nazi Azov Regiment.

Ikumbukwe kuwa Ukraine iliwahi kujitenga haraka haraka na shambulio hilo baada ya kutokea.
====

SmartSelect_20220822-210831_Chrome.jpg

SmartSelect_20220822-211016_Chrome.jpg

SmartSelect_20220822-211030_Chrome.jpg

 
Hiyo sio sura yake huyo atakuwa sio mwenyewe picha ya kuchonga
 
Back
Top Bottom