Majasusi watauona ufalme wa Mungu?

Ujasusi uko enzi na enzi. Joshua wa Biblia alifanya ujasusi, alikuwa jasusi na hatimaye akawa mrithi wa Musa na kuwa kiongozi mkuu wa wana wa Israel alipigana vita aliangusha ngome za maadui na kuwauwa kisawasawa Huu ni mfano mmoja.

Masharti ya kuingia mbinguni yalikuwa wazi enzi hizo kabla ya ujio wa Bwana Yesu hapa duniani pia yako wazi baada ya kuja kwa Bwana Yesu hapa duniani. Sasa sioni upekee wa jasusi ukilinganisha na binadamu wengine katika kuingia ufalme wa mbinguni. Bwana Yesu ndie njia pekee ya kweli na uzima na kwa Maneno yake Yesu mwenyewe anasema"Mimi ndimi njia ya kweli na uzima mtu haji kwa Baba yangu/Mungu ila kwa kupitia mimi" Huwezi fika kwa Mungu (mbinguni) bila ya kumpokea Bwana Yesu kuwa Kiongozi wako katika maisha haya tunayo ya ishi. Huu ndio ukweli mchungu kuukubali na kuumeza kwa baadhi yetu. Lakini ndio ukweli ambao mwanadamu kaachiwa aukubali au aukatae kwa hiari na utashi wake mwenyewe.

Kwa kumalizia ndugu majasusi mlio lengwa katika huu uzi jiulize kwa nini pilato alipolazimika kumhukumu Bwana Yesu ilibidi achukue maji na kunawa mikono yake? Fanyeni majukumu yenu kwa utii na uaminifu inapobidi/ikilazimu nawa mikono yako.

Mchina wajF.
Na washawasha!
 
Uislamu upi huo mkuu unao uongelea wewe sunni, kardiani, tablji au ushia? Maana wako wanaojiita waislamu safi na bado tuko tuna dukuliwa.

Mchina wajF.
Na washawasha!





 
Mdau ustadh Malcom Lumumba amemaliza kila kitu. Umeandika nilichotaka kuandika, japo nikiri, nisingeandika vema kama ulivyoandika. Heko kwako!
 
Mbaya zaidi kuna wachungaji, mapadre, na maimamu ambao ni majasusi na wanahubiri kutoa mawaidha misikitini na makanisani
 
Ukisoma Biblia, katika kitabu cha Yoshua sura ya pili, wanaongelewa majasusi wawili waliotumwa na Yoshua kwenda kuipeleleza Yeriko. Walifikia kwa kahaba mmoja anaitwa Rahabu. Rahabu ili kuwatunza wasiuawe, aliwaficha darini na akadanganya wameshaondoka. Hivyo kupitia uongo wake, aliwaokoa majasusi hao. Pia Rahabu mwisho akaolewa na waisraeli na katika mathayo 4, ametajwa katika ukoo wa Yesu.

Kuna Ibrahimu anayetajwa kama baba wa imani, huyu naye mara mbili alidanganya kuwa Sarah si mkewe ili asiuawe. Je, kwa mifano hiyo michache, Ibrahim na Rahabu hawataingia mbinguni?
 
Nasubiri majibu
 
Hizi nyuzi za kikubwa aisee unaweza ukapita hivihivi bila kuchangia acha mimi niwe msomaji tu.
 
Nenda kaangalie movie ya November man utapata majibu murua
 
Binadamu wengi hawana mungu nafsini mwao, Hasa viongozi wa nchi.Na kama kila kiongozi au kila binadamu haia duniani angekuwa na mungu moyoni mwake. Kusingekuwa na mauaji. Shetani ndiye anawashawishi watu wafanye maovu.kama wote tungekuwa tunafuata mafundisho na sheria za mungu, shetani asingekuwa na uwezo wa kushawishi nafsi zetu zifanye maovu. Hivyo kwa uejewa wami. Jasusi au muuaji yeyote hana nafasi kwa mungu. Viongozi wanashawishiwa na shetani kufanya maovu kwa matakwa yao binafsi.
 
Mmmmh Lumumba uko more than deep nahisi limeulizwa swali kwenye field yko
 

Only GOD can judge
Khaaaaaaaaaaaaaa
 
Mkuu hongera kwa kujibu kwa undani lakini pia kwa rejea mbali mbali.

Lakini katika majibu yako kuna maeneo yenye ukakasi na umejibu kwa 'humane perspective' na sio religious perspective. Mfano unaposema kwamba Jasusi anafanya kazi kwa niaba ya Taifa lake na ukatoa mifano ya ufaransa, Libya n.k. Tukumbuke Mungu anahukumu nafsi/mtu mmoja mmoja na sio kundi (serikali/taifa). Mungu ataita kila mmoja kwa dhambi alizofanya.

Pili, ni vyema ukitambua neno la Mungu sio subjective, halina muda, halina mahali, halina nani aliyelisema. NENO LA MUNGU LITASIMAMA, MAMBO YOTE YATAPITA. Bahati mbaya, binadamu wakiwemo baadhi ya wanathiolojia wamekuwa wakitafsiri neno la Mungu ili kuunga mkono hoja na agenda zao.

Pia niseme kwamba, siku hizi watu wanatumia mbinu nyingi ili ku justify dhambi, ikiwepo hii hoja ya 'Muktadha' wa kile kilichotamkwa kwenye Vitabu vya Mungu. Ukweli ni kwamba, Amri za Mungu zilikuwa na zitaendelea kuwa kipimo cha jambo flani ni dhambi ama si dhambi. Ukizini, Ukiua, Ukidanganya ili kuokoa maisha ya mtu huoni kama hiyo ni dhambi mkuu

Pia Ieleweke, sisemi kwamba mimi ni mwema sana. Pamoja na hilo nimeona bado kuna haja ya kuangazia namna MAJASUSI walivyo na changamoto katika kutafuta Ufalme wa Mungu
 
Kuna hoja hapo, ila je wakati huo makatazo yaliyopo kwenye Amri 10 za Mungu yalikwishatolewa?
 
Kuna hoja hapo, ila je wakati huo makatazo yaliyopo kwenye Amri 10 za Mungu yalikwishatolewa?
Kwa Ibrahim ilikuwa bado. Kwa habari ya Yeriko, ilikuwa imeshapita miaka takribani 42 tokea Mungu atoe hayo makatazo katika mlima sinai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…