Majasusi watauona ufalme wa Mungu?

Majasusi watauona ufalme wa Mungu?

Yaani stori ndeeefu kutetea dhambi, mpaka hapo una Zero, bora tu usiendelee. Halafu umeelezea upande mmoja, Kwa Uislam hujagusa, hapo ndo ujue kwa upande ulioulezea inawezekana hayo ni sawa. Kwa uislam huna ulijualo, so usijumuishe kwamba halali kwakuwa upande wenu poa. Lete aya za qur an na hadith kwamba kuua kwa kutumwa ni sawa
 
Kwa Ibrahim ilikuwa bado. Kwa habari ya Yeriko, ilikuwa imeshapita miaka takribani 42 tokea Mungu atoe hayo makatazo katika mlima sinai.
Sawa mkuu, ndio maana nimeikubali una hoja. Lakini kwasababu yalifanywa na manabii haimaanishi si dhambi. Nakumbuka hata Musa kuna wakati alimuudhi Mungu, na Mungu alimuudhibu kwa kumnyima fursa ya kukanyaga nchi ya ahadi. Pengine hata hao watumishi wa Mungu waliotenda dhambi kwa namna moja au nyingine waliadhibiwa
 
Yaani stori ndeeefu kutetea dhambi, mpaka hapo una Zero, bora tu usiendelee. Halafu umeelezea upande mmoja, Kwa Uislam hujagusa, hapo ndo ujue kwa upande ulioulezea inawezekana hayo ni sawa. Kwa uislam huna ulijualo, so usijumuishe kwamba halali kwakuwa upande wenu poa. Lete aya za qur an na hadith kwamba kuua kwa kutumwa ni sawa
dini ya kiislam haijakakamaa wala so legelege,inaelekeza kuifata kwa kujali mazingira halisi yanayomkabili mja,nguruwe haram kayika mazingira ya kawaida lakini si katika mazingira ya njaa kufa,Leo hii huwezi kwenda kuishi tu saudia kwa kuwa wewe no muislam,watakugomea tu,nchi yako no hii,lakini kama nchi tuna maadui au watu wasiopenda mustakabali mwema wa nchi,unawazuwiaje wasilete naqma nchini itayosababisha waumini washindwe kufanya ibada?jamii isivurugike? no kupitia taasisi kama hizo(jeshi,ujasusi nk) cha msingi ukitakiwa kumdhuru MTU jiridhishe ni kwa maslahi mapana ya nchi..I'll wengine wamwabudu mungu kwa a mani na kumuhubiri..sioni tatizo lolote katika hili
 
Najishangaa mimi ambae sijawahi japo kumchanja mtu na kiwembe huku wengine wanamwaga damu ya binaadamu mwenzao na bado anaamini mbinguni ataingia
Wengine hata kuchinja kuku kwa ajili ya kitoweo ni shughuli pevu!
 
Amani iwe nanyi

Katika kuwaza jinsi ya kuingia kwenye Ufalme wa Mungu kuna mambo mengi nimekuwa nikijiuliza ikiwepo akina nani kutokana na nature ya kazi zao wana nafasi nzuri ya kufika Paradiso na akina nani wako destined kutouona Ufalme wa Mungu kutokana na majukumu yao ya kikazi. Hapo ndipo nilipokutana na hii kazi.... MAJASUSI

Inafahamika kwamba kila nchi ina mfumo wake na vyombo vyake vya kiusalama katika kuhakikisha Taifa husika lipo salama.

Kwa mfano Marekani wana CIA(Agency ya kiataifa) /FBI (agency ya ndani ya nchi), Uingereza wana MI6, na Urusi wana GRU. Upande wa China ipo MSS, Pakistan ISS, Israel ipo MOSSAD na South Africa ipo SSA. Hizi ni baadhi ya Agency za kiintelijensia duniani zenye uwezo mkubwa unaosababishwa na teknolojia kubwa waliyo nayo pamoja na Majasusi wabobezi.

Katika kutimiza majukumu yao hawa Wana intelijensia wamekuwa wakifanya mambo mbali mbali ili kufanikisha kazi/assignment zao, na ili kukamilisha kazi zao kwa mtazamo wangu wanalazimika kufanya mambo mengi yasiyo mpendeza Mungu.

Kuua. Kuna misamiati kama ku-eliminate threat imekuwa ikitumika sana, hasa kwenye siasa za Africa, kwenye usalama wa nchi za Asia na dunia na kwenye Uchumi wa nchi za Magharibi. Kinachostua zaidi kuna wakati wanashughulikia hata mwenzao pale wanapoamini anaweza kuwaharibia, wanaita kawa COMPROMISED. Maneno ya Mungu yanasema USIUE.

Kuzini.Kuna majasusi wa kike au hata wa kiume ambao wana jiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi ili kupata taarifa. Wengine wanaingilia mpaka ndoa za watu/target katika kukusanya taarifa zao, wengine mpaka wanapata watoto ili tu kufanikisha kazi zao. Wanazini, maandako yanasema USIZINI.

Kusema uongo. Hii ni kati ya sifa kubwa walionayo wana intelijensia duniani. Hii sifa ipo katika namna mbili, namna ya kwanza ni KUTUNZA SIRI (sio dhambi) lakini kuna wakati ili Kutunza siri wanalazimika kusema Uongo. Kuna wana intelligentsia wengi wanadanganya wanafamilia zao kwamba wanafanya kazi flani kumbe kazi zao ni nyingine. Pia huwa wanasema uongo mkubwa zaidi ya huu katika kufanikisha mission zao.

Kuiba. Katika harakati za kufanikisha kazi zao, hawa jamaa wamejikuta wakiiba, hapa simaanisha fedha ama mali... La hasha, wamekuwa wakiiba taarifa kimtandao, nyaraka katika maeneo mbali mbali n.k ili kupata taarifa ambazo pengine wasingezipata kwa njia ya kawaida.

Je hawa jamaa, wana nafasi ya kuuona Ufalme wa Mungu? Je Walokole/Waislamu washika dini wana nafasi kwenye kazi kama hii?
Kama wewe uko njia panda na ni Mkristo wa kweli unaye mpenda Mungu wa kweli,naomba usome maandiko yafuatayo,huku ukimuomba Roho Mtakatifu akusaidie kuyaelewa.Naomba usidanganyike na maelezo au mafundisho yaliyojaa hila na uvuvio wa Shetani,yenye nia ya kupotosha ukweli,Mungu hajabadilika,aliyesema usiue kwenye amri zake kumi ndiye huyo huyo aliyeko leo..
1.Warumi 1:28-32.
2. 2Timotheo 3:1-5
3.1Timotheo 6:6-10
4.Waefeso 5:1-7
5.Marko 7:21-22.
Msitari wa saba Efeso 5 unasema wazi,"Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana;kwa kuwa kwa sababu ya hayo, hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi."
Nimalizie kwa kusema "Mwana wa Mungu" hana nafasi kwenye ujasusi na niongeze kwenye majeshi yote na siasa.Ila kuurithi ufalme wa Mungu inawezekana,ila chances ni very slim.
 
Ukisoma Biblia, katika kitabu cha Yoshua sura ya pili, wanaongelewa majasusi wawili waliotumwa na Yoshua kwenda kuipeleleza Yeriko. Walifikia kwa kahaba mmoja anaitwa Rahabu. Rahabu ili kuwatunza wasiuawe, aliwaficha darini na akadanganya wameshaondoka. Hivyo kupitia uongo wake, aliwaokoa majasusi hao. Pia Rahabu mwisho akaolewa na waisraeli na katika mathayo 4, ametajwa katika ukoo wa Yesu.

Kuna Ibrahimu anayetajwa kama baba wa imani, huyu naye mara mbili alidanganya kuwa Sarah si mkewe ili asiuawe. Je, kwa mifano hiyo michache, Ibrahim na Rahabu hawataingia mbinguni?
Kuna Uongo na uongo Mtakatifu(Uongo uliotakaswa na Mwenyezi Mungu au uliokubaliwa),kuna Uuaji/Mauaji na Uuaji/Mauaji Matakatifu (hapa unakutana na neno Vita takatifu).Sasa Vigezo vya kuwa Uongo/Vita takatifu hiyo ni mada nyingine na majibu ameyagusia mtaalamu Malcom
 
Amani iwe nanyi

Katika kuwaza jinsi ya kuingia kwenye Ufalme wa Mungu kuna mambo mengi nimekuwa nikijiuliza ikiwepo akina nani kutokana na nature ya kazi zao wana nafasi nzuri ya kufika Paradiso na akina nani wako destined kutouona Ufalme wa Mungu kutokana na majukumu yao ya kikazi. Hapo ndipo nilipokutana na hii kazi.... MAJASUSI

Inafahamika kwamba kila nchi ina mfumo wake na vyombo vyake vya kiusalama katika kuhakikisha Taifa husika lipo salama.

Kwa mfano Marekani wana CIA(Agency ya kiataifa) /FBI (agency ya ndani ya nchi), Uingereza wana MI6, na Urusi wana GRU. Upande wa China ipo MSS, Pakistan ISS, Israel ipo MOSSAD na South Africa ipo SSA. Hizi ni baadhi ya Agency za kiintelijensia duniani zenye uwezo mkubwa unaosababishwa na teknolojia kubwa waliyo nayo pamoja na Majasusi wabobezi.

Katika kutimiza majukumu yao hawa Wana intelijensia wamekuwa wakifanya mambo mbali mbali ili kufanikisha kazi/assignment zao, na ili kukamilisha kazi zao kwa mtazamo wangu wanalazimika kufanya mambo mengi yasiyo mpendeza Mungu.

Kuua. Kuna misamiati kama ku-eliminate threat imekuwa ikitumika sana, hasa kwenye siasa za Africa, kwenye usalama wa nchi za Asia na dunia na kwenye Uchumi wa nchi za Magharibi. Kinachostua zaidi kuna wakati wanashughulikia hata mwenzao pale wanapoamini anaweza kuwaharibia, wanaita kawa COMPROMISED. Maneno ya Mungu yanasema USIUE.

Kuzini.Kuna majasusi wa kike au hata wa kiume ambao wana jiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi ili kupata taarifa. Wengine wanaingilia mpaka ndoa za watu/target katika kukusanya taarifa zao, wengine mpaka wanapata watoto ili tu kufanikisha kazi zao. Wanazini, maandako yanasema USIZINI.

Kusema uongo. Hii ni kati ya sifa kubwa walionayo wana intelijensia duniani. Hii sifa ipo katika namna mbili, namna ya kwanza ni KUTUNZA SIRI (sio dhambi) lakini kuna wakati ili Kutunza siri wanalazimika kusema Uongo. Kuna wana intelligentsia wengi wanadanganya wanafamilia zao kwamba wanafanya kazi flani kumbe kazi zao ni nyingine. Pia huwa wanasema uongo mkubwa zaidi ya huu katika kufanikisha mission zao.

Kuiba. Katika harakati za kufanikisha kazi zao, hawa jamaa wamejikuta wakiiba, hapa simaanisha fedha ama mali... La hasha, wamekuwa wakiiba taarifa kimtandao, nyaraka katika maeneo mbali mbali n.k ili kupata taarifa ambazo pengine wasingezipata kwa njia ya kawaida.

Je hawa jamaa, wana nafasi ya kuuona Ufalme wa Mungu? Je Walokole/Waislamu washika dini wana nafasi kwenye kazi kama hii?

Jibu ni ndiyo;

Ushahidi unapatikana kuanzia hapa Mathayo 1 ambacho ni kitabu cha historia ya ukoo wa Yesu. Kuna jasusi linaitwa Rahabu "5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu;Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu;Obedi akamzaa Yese; 6 Yese akamzaa Daudi mfalme.... "

Musa alitumwa na Mungu kutengeneza majasusi kwa kuchagua watu vipanga( vichwa hasa) na kati ya hao wawili Joshua na Kaleb waliuona Ufalme wa Mungu. Kasome Hesabu 13

"1 Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia,

2 Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao.

3 Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na Bwana; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli."

Kuna mifano mingi hadi Agano jipya kuna jasusi liliitwa Paulo n.k sitaki kuandika kitabu hapa.

Ufalme wa Mungu ndio unaongoza kwa ujasusi. Ishu sio ujasusi, ishu ni matumizi ya ujasusi. Ukifanya ujasusi kwa maslahi ya taifa( iwe kweli sio kwa kujidanganya) haina shida, lakini ujasusi kwa maslahi binafsi ni dhambi. Binafsi ni pamoja na maslahi ya wanasiasa na matumbo yao. It has to be purely for the greater course.
 
Uislamu upi huo mkuu unao uongelea wewe sunni, kardiani, tablji au ushia? Maana wako wanaojiita waislamu safi na bado tuko tuna dukuliwa.

Mchina wajF.
Na washawasha!
Uislam ni mmoja hivyo ni vikundi tuu wametengeneza watu so Mtume SAW hakuacha kitu cha namna hiyo
 
Back
Top Bottom