Majasusi watauona ufalme wa Mungu?

Yaani stori ndeeefu kutetea dhambi, mpaka hapo una Zero, bora tu usiendelee. Halafu umeelezea upande mmoja, Kwa Uislam hujagusa, hapo ndo ujue kwa upande ulioulezea inawezekana hayo ni sawa. Kwa uislam huna ulijualo, so usijumuishe kwamba halali kwakuwa upande wenu poa. Lete aya za qur an na hadith kwamba kuua kwa kutumwa ni sawa
 
Kwa Ibrahim ilikuwa bado. Kwa habari ya Yeriko, ilikuwa imeshapita miaka takribani 42 tokea Mungu atoe hayo makatazo katika mlima sinai.
Sawa mkuu, ndio maana nimeikubali una hoja. Lakini kwasababu yalifanywa na manabii haimaanishi si dhambi. Nakumbuka hata Musa kuna wakati alimuudhi Mungu, na Mungu alimuudhibu kwa kumnyima fursa ya kukanyaga nchi ya ahadi. Pengine hata hao watumishi wa Mungu waliotenda dhambi kwa namna moja au nyingine waliadhibiwa
 
Pakistani ni ISI
Ni kweli mkuu, tatizo hizi simu zina vimbelembele, niliandika ISI, yenyewe ikaweka hilo neno, ntakuwa muangalifu zaidi next time kwenye kuhakiki nilichokiandika
 
dini ya kiislam haijakakamaa wala so legelege,inaelekeza kuifata kwa kujali mazingira halisi yanayomkabili mja,nguruwe haram kayika mazingira ya kawaida lakini si katika mazingira ya njaa kufa,Leo hii huwezi kwenda kuishi tu saudia kwa kuwa wewe no muislam,watakugomea tu,nchi yako no hii,lakini kama nchi tuna maadui au watu wasiopenda mustakabali mwema wa nchi,unawazuwiaje wasilete naqma nchini itayosababisha waumini washindwe kufanya ibada?jamii isivurugike? no kupitia taasisi kama hizo(jeshi,ujasusi nk) cha msingi ukitakiwa kumdhuru MTU jiridhishe ni kwa maslahi mapana ya nchi..I'll wengine wamwabudu mungu kwa a mani na kumuhubiri..sioni tatizo lolote katika hili
 
Najishangaa mimi ambae sijawahi japo kumchanja mtu na kiwembe huku wengine wanamwaga damu ya binaadamu mwenzao na bado anaamini mbinguni ataingia
Wengine hata kuchinja kuku kwa ajili ya kitoweo ni shughuli pevu!
 
Kama wewe uko njia panda na ni Mkristo wa kweli unaye mpenda Mungu wa kweli,naomba usome maandiko yafuatayo,huku ukimuomba Roho Mtakatifu akusaidie kuyaelewa.Naomba usidanganyike na maelezo au mafundisho yaliyojaa hila na uvuvio wa Shetani,yenye nia ya kupotosha ukweli,Mungu hajabadilika,aliyesema usiue kwenye amri zake kumi ndiye huyo huyo aliyeko leo..
1.Warumi 1:28-32.
2. 2Timotheo 3:1-5
3.1Timotheo 6:6-10
4.Waefeso 5:1-7
5.Marko 7:21-22.
Msitari wa saba Efeso 5 unasema wazi,"Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana;kwa kuwa kwa sababu ya hayo, hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi."
Nimalizie kwa kusema "Mwana wa Mungu" hana nafasi kwenye ujasusi na niongeze kwenye majeshi yote na siasa.Ila kuurithi ufalme wa Mungu inawezekana,ila chances ni very slim.
 
Kuna Uongo na uongo Mtakatifu(Uongo uliotakaswa na Mwenyezi Mungu au uliokubaliwa),kuna Uuaji/Mauaji na Uuaji/Mauaji Matakatifu (hapa unakutana na neno Vita takatifu).Sasa Vigezo vya kuwa Uongo/Vita takatifu hiyo ni mada nyingine na majibu ameyagusia mtaalamu Malcom
 

Jibu ni ndiyo;

Ushahidi unapatikana kuanzia hapa Mathayo 1 ambacho ni kitabu cha historia ya ukoo wa Yesu. Kuna jasusi linaitwa Rahabu "5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu;Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu;Obedi akamzaa Yese; 6 Yese akamzaa Daudi mfalme.... "

Musa alitumwa na Mungu kutengeneza majasusi kwa kuchagua watu vipanga( vichwa hasa) na kati ya hao wawili Joshua na Kaleb waliuona Ufalme wa Mungu. Kasome Hesabu 13

"1 Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia,

2 Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao.

3 Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na Bwana; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli."


Kuna mifano mingi hadi Agano jipya kuna jasusi liliitwa Paulo n.k sitaki kuandika kitabu hapa.

Ufalme wa Mungu ndio unaongoza kwa ujasusi. Ishu sio ujasusi, ishu ni matumizi ya ujasusi. Ukifanya ujasusi kwa maslahi ya taifa( iwe kweli sio kwa kujidanganya) haina shida, lakini ujasusi kwa maslahi binafsi ni dhambi. Binafsi ni pamoja na maslahi ya wanasiasa na matumbo yao. It has to be purely for the greater course.
 
Uislamu upi huo mkuu unao uongelea wewe sunni, kardiani, tablji au ushia? Maana wako wanaojiita waislamu safi na bado tuko tuna dukuliwa.

Mchina wajF.
Na washawasha!
Uislam ni mmoja hivyo ni vikundi tuu wametengeneza watu so Mtume SAW hakuacha kitu cha namna hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…