Majembe Auction Mart huu ni Wizi - Tumewachoka sasa

Governor of Bettors-GB

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
10,568
Reaction score
9,710
Habari wakuu.
Hembu nipeni njia ya hawa Majembe jinsi wanavyofanya kazi.

Kuna gari zangu Carry zimo kwenye biashara.
Niliwahi kwenda TRA na Halmashauri kuhusu kuomba vibali wakaniambia kwamba wanatoa vibali kuanzia Tani 3.5 na sio chini ya hapo.
Kwahiyo gari zikawa zinafanyakazi na vibali vyote vinavyoruhusu kutembea,maana Carry ni chini ya kiwango chao.

Sasa leo Kuna Driver weangu mmoja amekamatwa Pale Pugu na hao Jamaa wa Majembe.
Hali jinsi ilivyokuwa ni kwamba,wanadai eti walipwe Laki Nne.
Na wamekuwa wanamharasi sana Driver na kumtisha kwamba watampeleka polisi na kesho gari inaenda Makao makuu na faini itakuwa kubwa zaidi.

Sasa diver aliponipigia nikampigia Mwanasheria wa Halmashauri akasema kwamba tuwaulize wao wamepewa Mamlaka hayo na Kitengo kipi cha Serikali.
Alipowauliza wakasema kwamba wao hawataki kuulizwa maswali,na tukijifanya kujua watu wa serikalini ndio charge itakuwa kubwa kwa usumbufu.

Driver wangu ame experince ujanja pale baada ya kuwaambia kuwa wanawasiliana na mwanasheria wa Serikali na katika hali hiyo kila mmoja anamtupia mwenzie mpira.
Mwanasheria wa Manispaa kanishauri kwenda Polisi kutoa taarifa juu ya hilo,ili wao waleleze mamlaka iliyowapa kumata gari zenye chini ya Tani iliyowekwa na Serikali na kwa mamlaka ipi.
Na Kwa Jeuri ya mmhusika mmoja wa Majembe anasema kwamba hizi Carry zimekuja kuuwa biashara ya Center kwahiyo tutazikama sana.
Sasa hii inaonyesha kwamba Canter ambazo ni 3.5 tani ndio zilikuwa zinawapa ulaji.

Nimemuamrisha Driver aiche gari na aende polisi,halafu pia achukue picha ya kitupo na wahusika.
Na nitazirusha muda sio mrefu hapa.

Maana naambiwa hata risiti hazionyeshi jina la mwenye gari wala aliemkamata muhusika.

Subiri nitawa update baada ya Diver kutoka Polisi,then kesho na cross Dar nitawapa update zaidi.
Na kama kuna sehem nyingine ya kwenda mnaweza kunishauri ili ni complie yote kwa pamoja.

Unless iwe ni sahihi utaratibu,la sivyo nitaondoka na mtu
 
pole sana mkuu,, tuko pamoja sana, Siku hizi kumezuka ujambazi wa serikali na wadau wake, WAJASIRIAMALI, WAHANGAIKAJI, WAFANYABIASHARA, Wananyanyaswa sana nchi hii.

Tatizo hawana watetezi kabisa, tulipaswa kuwa na wabunge wetu maalum wa kututetea kama yalivyo makundi mengine ya kijamii. mwambie driver akusanye picha za kutosha hata magazetini wapewe
 
Safi sana mkuu...jaribu kuwapa lesson ...hii sio miaka ya 90 ...watu wana akili zao timamu sasa ivi..
 
Update:
Wakuu suala limeisha hivyo hivyo ki utata utata.
Maana nimehofu gari yangu kalala siku mbili maana Jana ililazwa kwakuwa muda ulikuwa umaisha

Baada ya leo kwenda,nilianza kuonana na wahusika ikiwemo Polisi wa kituo cha Karibu.

Nilichogundua ni kwamba hizi Sectors za Serikali kutokuwa na link zenye maelezo sahihi kwa pamoja,kila mmoja ana lake.
Ufupi nimelipa laki mbini na kitu pamoja na elfu kumi na kama charge ya kulaza gari kwenye Yard ya Majembe.

Maelezo:-
Ningependa ku share na wenzangu juu ya suala hili,nikwamba baada ya hizi Carry kuwa nyingi mjini nakuuwa kazi za Center ,basi Majembe sasa hivi wana deal na Carry kwa kasi sana.Na walisema uso kwa uso pale,kwamba Carry zimeuwa biashara ya Center lazima zilipiwe zote bila kujali ni ya biashara au binafsi maana mtu huwezi kutembelea Carry.

Haijalishi ni Private au ni la Biashara. Maana wameniambia kwamba Gari kuwa ya biashara sio lazima ikae Stand inasubiria,hata kama una Carry yako unabeba majani ya ng`ombe kupeleka Shambani lazima ulipe kama ya biashara maana wale wanyama wanakuzalishia. Na pia kama unaduka lako mwenyewe na unatumia kubebea mizigo,basi lazima ulipe maana ile gari ndio inayokuzalishia kukuchukulia mizigo yako na imo kwenye biashara.

So,lazima iwe na Utililty Card (sijui kama nimeiweka sawa). Kwahiyo ukiangalia ni kwamba ni trofauti na zamani wale wenye pick up zao wanaozenda mashambani au katika kazi binafsi bila usmbufu,ila kwa sasa wakikunasa na mzigo hata kama ni private lazima ulipishwe faini na uambiwe ukalipia TRA kodi mpya ya kwamba gari yako ni ya Biashara ili upewe Card.

Sasa tatizo jingien ni kwamba Ofisi za TRA wao ukienda wanakuambia hawaitambui kodi hiyo,maana wao bado wanalist ya kuanzia tani 3.5 ndio ilipiwe kodi ya aina hiyo. Sasa yule Polisi aliniambia kwamba utaratibu huo upo.Na hata kama gari ni ya kwako inabeba hata vifanga tu kupeleka shambaa lazima ulipie hiyo Card kwamba ni gari ya Biashara la sivyo majembe watakukamata tu.

Na akanishauri na kuniambia inapoelekea ni kwamba hakuna Carry itakayokuwa ni Private,maana zote zinawekwa kwenye list ya gari za Biashara kama ilivyokuwa kwa center zamani. Sasa nikauliza mbona wakati Carry hazijaanza kuwa nyingi mbona wenye pick up na doubel cabins cars walikuwa wanabeba vitu vyao kwenda shamba bila usumbufu,nikaambiwa ilikuwa zamani sio sasa,hata wao wakinaswa watalipa na kusajili kwamba ni gari inayowasidia katika mambo ya shamba na inazalisha pia.

Nilikaa kimya,nimelipa fine na nimeona bora niwajuze wenzangu juu ya suala hili na wenye gari za aina hii pindi wakiingia mikononi mwa vijana wa kazi Majembe wajue pa kuanzia. Ila muhim tu ukikamtwa nenda kituo cha polisi kutoa taarifa ili upate maelekezo na usilipe pesa mkononi.
Mie nimelipia leo through Bank.

Ningeomba tu vyombo vya serikali kuwa na melezo sahihi juu ya haya masuala,maana la sivyo hi hali italalamikiwa kila siku. Ukiuliza idara husika inakupa maelezo mengine,na ukienda idara nyingine unaambiwa mengine. Sasa wale wenye Carry hata kama ni binafsi,basi kulipia Car hiyo ni 424,000 kwa mwaka na Center 728,000 kwa mwaka. La sivyo wakikunasa imekula kwako kama ilivyokula kwangu kwa kubeba mzigo wa shambani.
 

pole mpendwa
 
Mh ushuru wa carry ni 120,000 ukienda TRA why tena 424,000?
Mkuu nimeambiwa ni Kodi ya gari ya kuzalisha,wakaniambia kwamba TRA kuna kodi nyingi nahii imo na ndio muhim kama gari yako ikigundulika inatumika kwa ajili ya kuzalisha au kukusaidia katika kazi za uzalisha,kama ikiwa Carry inabeba bidhaa zako za shambani yaani unaitumia shambani,au hata kama ume park dukani kwako basi uilipie kama ya kuzalisha.
Nilimuachia mdogongo wangu achukue Receipt,ngoja jtatu nita attach hapa.
Yaani naona tunachanganywa tu,na hadi askari wanasema the same,utalolikuta majembe basi na kwao hilohilo.
Sasa hapo inakuwa ni kujumuisha hiyo na hizi nyingine zinazoibuka,naona zitafikia milioni sasa kwa mwaka
 

Hiyo hela umelipa wapi TRA au Majembe? (Usinijibu bank, sababu bank sio walipwaji ila ni channel ya kulipia)
 
Hiyo hela umelipa wapi TRA au Majembe? (Usinijibu bank, sababu bank sio walipwaji ila ni channel ya kulipia)
Kodi ni ya TRA ila Bank Details ni za Majembe Auction Mart ndio wanaotaka kulipwa na kusema ni mawakala wao katika matukio kama haya.
 
Kuna matapeli wanatumia jina LA Majembe kutapeli.
Weka picha za Hao watu wa Majembe waliokamata gari lako hapa kwanza ili wahusika waweze kuwatambua
 
Kuna matapeli wanatumia jina LA Majembe kutapeli.
Weka picha za Hao watu wa Majembe waliokamata gari lako hapa kwanza ili wahusika waweze kuwatambua

Huyu katapeliwa kwa Nina la majembe! Polisi wanaushirika na matapeli. TRA hawana mawakala ambao wanatoa nyaraka zenye nembo ya TRA,
 
Kodi ni ya TRA ila Bank Details ni za Majembe Auction Mart ndio wanaotaka kulipwa na kusema ni mawakala wao katika matukio kama haya.
mkuu naomba uende tra upewe majibu ya uhakika,hao majembe ni matapeli wakubwaa hasa hao vijana wake,ngoja ni kuPM namba ya sethi motto majembe CEO wao umueleze uonevu uliofanyiwa
maana kunasiku walitaka kunitapeli nilipompigia akaja kumbe sio wafanyakazi wa majembe ili hali wanakila kitu cha kuwatambulisha ni majembe
 

Duh pole sana.
Nikuulize masuali.
Hizo gari ambazo sio za biashara lakini kutokana ni aina ya pickup, lazima ulipie hizo gharama unazo sema.
Sasa jee usajili wa number ya gari unakuwa wa biashara? Ninavyo fahamu mimi kwamba kuna number rangi ya yellow na white, katika moja hio ni ya biashara.
Wallah sikumbuki tena, wakati nilipokuwa dar es salaam, nilikuwa nikibadilisha hizo number kutoka private in to business, gari za campany.

Jee hao mabwana wakubwa husimamisha tu magari yoyote yenye mfumo wa kubeba mzigo aina ya pickup? Mana nyengine sio za biashara kama zilivyo sajiliwa number zake.
 
Wanaweza kukamata raia mi polisi tu na kwa maeneo ya shughuli za jiji na mgambo wao.
Raia mwengine hana mamlaka wala hakuna sheria ya wewe kukubali kukamatwa nao.
Cha kukufanya ni kogoma kuwasikiliza na kuondoa gari. Wakinisha wabamize gari ukitowe .
Imekua desturi kila mwizi anaweka road block na kukamata magari.
Tufike mahali tuseme no.
Hivyo nakushauri usikubali kukamatwa au kusimamishwa na mtu ambaye sie polisi au mgambo wa jiji.
Una haki ya kukataa kikatiba .
Akikataa mmoja na wengine wote wakikataa hawa vibaka majembe kampuni ya Sumaye hii ni wizi mtupu.
Hivyo musikubali kukamatwa nao mwambie huna amri ya kunikamata na akikufanyia fujo ondoa gari kwa nguvu.
Ujinga huu kila ikikaribia uchaguzi ndio unazidi watu wanatuibia kwa vile serikali imelala na huwa haijali tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…