Majembe mawili ya Yanga kutua kesho asubuhi, ni kutoka Zimbabwe na Ghana

Majembe mawili ya Yanga kutua kesho asubuhi, ni kutoka Zimbabwe na Ghana

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
SALAAM

KIUNGO chipukizi wa Ghana, Joseph Tetteh Zutah na mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma kwa pamoja wanawasili kesho nchini kwa ajili ya kuja kujiunga na Yanga SC.

Zutah aliyezaliwa Agosti 22, mwaka 1994 anatokea klabu ya Medeama ya kwao, wakati Ngoma anatokea FC Platinum ya kwao pia na wote watafika asubuhi.

Yanga SC imekwishafanya mazungumzo ya awali na wachezaji hao na wanatarajiwa kuja kusaini mikataba.

Yanga SC iliitoa Platinum katika hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu, lakini kocha Mholanzi Hans van der Pluijm akavutiwa mno na Ngoma, aliyecheza mechi moja tu ya Zimbabwe baada ya kukosa mechi ya Dar es Salaam kwa sababu alikuwa majeruhi.

Na Pluijm ambaye amewahi kufundisha Ghana, ndiye aliyempendekeza Zutah ambaye uongozi wa Yanga SC haujawahi kumuona kabisa, lakini vyanzo vinasema huyo ni mchezaji mzuri anayeweza kucheza pia kama beki wa kulia.

Akiwa na umri wa miaka 26, Ngoma ni mchezaji mwenye uwezo na uzoefu mkubwa, kwani amekwishaichezea Zimbabwe hadi kwenye Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).

UPDATES:
Wachezi wawili wa kigeni kutoka GHANA NA ZIMBABWE watua leo.
 
Attachments

  • 1-1.jpg
    1-1.jpg
    62.8 KB · Views: 196
unayajua hayo unayoyaita majembe ? labda huyo ngoma angalau tulimuona kwenye chani a.kusini lakini sio huyo mghana
 
asante kwa taarifa njema. ..lakini kwa nini wasije juzi ili leo akawajaribu kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa???????
 
asante kwa taarifa njema. ..lakini kwa nini wasije juzi ili leo akawajaribu kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa???????

Sio kila mchezaji ni wa kujaribiwa. Mfano Ngasa
 
Mi Yanga lkn wadau wa Yanga na Simba tuna tambo za ajabu sana ikifika wakati wa usajili. Timu zeti zina miaka zaidi ya hamsini lkn hata kikombe kimoja cha Africa . Kuna mafanikio kweli? Tujipime
 
Mi Yanga lkn wadau wa Yanga na Simba tuna tambo za ajabu sana ikifika wakati wa usajili. Timu zeti zina miaka zaidi ya hamsini lkn hata kikombe kimoja cha Africa . Kuna mafanikio kweli? Tujipime

Simba imesajili mchezaji mwenye rekodi ya Messi (original) na Ronaldo
 
tuone kazi sasa sio maneno mengi. kipindi cha usajili bongo kuna kuwa na mbwembwe sana
 
Back
Top Bottom