A
Anonymous
Guest
Mimi ni mwananchi na mfanyabiashara mmojawapo miongoni mwa wamiliki wa nyumba na viwanja zaidi ya 100 vilivyopo katika eneo la Ubungo Riverside, pembezoni mwa stendi ya basi (Riverside).
Eneo hili la kibiashara, nina nyumba yangu halali yenye hatimiliki ya uwekezaji ikiwemo biashara na makazi mbalimbali, sio eneo la uvamizi; ni makazi na maeneo halali ya kibiashara lakini leo hii, uwekezaji wangu na wa majirani zangu umekuwa chanzo cha maumivu na umaskini mkubwa kwa miezi na miaka nenda rudi.
Mambo yalianza mwaka 2019 wakati viongozi na wataalamu wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) walipokuja na kutupa taarifa kuwa eneo letu linahitajika kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya mwendokasi (kwa ajili ya kugeuzia mabasi).
Mnamo mwaka 2020, maafisa kutoka TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam walikuja na kufanya zoezi rasmi la ushaminishaji (valuation) wa nyumba zetu zote. Baadaye, walituletea hesabu kamili za fedha za fidia ambazo kila mmmiliki angelipwa.
Pamoja na hesabu hizo, tulipewa sharti gumu na zito: "Kuanzia leo, ni marufuku kwa mtu yeyote kuendeleza, kukarabati au kujenga kitu chochote katika eneo hili kwa sababu malipo yatafanyika muda wowote."
Tangu mwaka huo wa 2020 hadi leo, TANROADS wametoweka na kukaa kimya kabisa.
Uchakavu wa Majengo: Kwa sababu ya marufuku ya kutokarabati, majengo yetu yamechakaa vibaya sana. Mabati yameoza kwa mvua za Dar es Salaam, kuta zimepasuka (kucrack), na biashara zetu kama guest house na fremu zimekufa kabisa kwa sababu maeneo hayatakikani tena kwa matumizi ya kibinadamu.
Hasara ya Kiuchumi: Tumepoteza wapangaji, tumepoteza kipato cha kila siku, lakini bado tunaendelea kushikiliwa mikono na kuzuiliwa kufanya chochote kwenye maeneo yetu wenyewe.
Kila tukijaribu kuomba kibali cha kukarabati angalau tuokoe majengo yasibomoke, tunakumbana na kuta ngumu. Wanakataa na kuja kupiga stop.
Mwezi wa Pili 2026, niliandika tena barua rasmi kuomba kuendeleza eneo langu. Majibu niliyoyapata kutoka kwao yalinichoma sana moyoni: Walisema ushaminishaji wa mwaka 2020 ulishapita muda wake (expired), fedha zilizokuwa zimetengwa zilishapelekwa kufanya miradi mingine, na kwamba wapo kwenye mchakato wa kuja kufanya ushaminishaji mpya!
Niliamua kwenda hadi Wizarani kuonana na Katibu Mkuu. Nilimuonyesha barua zote zenye nembo, saini, na mihuri rasmi ya TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam. Cha kusikitisha, hata huko wizarani majibu yao ni kuwa "hawawaelewi hao watu wa mkoa" na kuahidi tu kuwa "watafuatilia."
Sisi sio wavamizi, tumewekeza kwa jasho letu na tuna hati halali za umiliki. Hivi ni haki gani mwananchi anyanyaswe kwenye ardhi yake halali kwa miaka 8 mfululizo?
Tunaomba serikali kuu na mamlaka za juu zituokoe kwenye janga hili:
Kama mradi bado upo, TANROADS watulipe fidia zetu stahiki mara moja kulingana na thamani ya sasa ya soko ili tuondoke tukatafute maisha mengine.
Kama mradi umefutwa au haupo tena, watutangazie rasmi na watuondolee vizuizi hivyo ili tupate uhuru wa kukarabati na kuendeleza mali zetu zilizochakaa kabla hazijaporomoka kabisa.