Majeshi ya nchi nyingine za kizalendo yaungane na JWTZ kuzuia vibaraka wa Wazungu M23 wasiuteke Mji wa Goma

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Inakera sana kuona Baadhi ya Nchi za Kiafrika zimejikausha na kuisusa DRC Kwa kuiacha inagukie kwenye mikono ya Jeshi la Vibaraka wa Wazungu M23 Kupitia Rwanda.

Ni kama Wameisusia Tanzania peke yake kiasi kwamba inaweza ikawa ngumu Kwa JWTZ Kuzuia hao Vibaka kuuteka Mji wa Goma ikizingatiwa kwamba watakuwa wanapewa vifaa vya Kisasa ,kusaidia inteligensia nk na Mabeberu. Soma JWTZ yatoa sababu 200 zilizoifanya Tanzania ipambane na waasi wa M23

Wananchi wa DRC wa Imani na JWTZ lakini Sina hakika kama wao yao wataweza kuwazuia M23 ikizingatiwa kwamba JWTZ Iko huko kulinda amnani na sio mstari wa mbele wa Vita,wanatakiwa kuwa mstari wa mbele NJ Jeshi la DRC lakini ndio Hilo limezidiwa.Inatia sana hasira.👇👇

View: https://youtu.be/Fs7jEBnCRJU?feature=shared
My Take
Nchi zingine za Kizalendo Ziungane kuzuia huu uhuni wa Rwanda.

Ikumbukwe Rwanda Kwa Sasa imepunguza sana biashara na Tanzania na bidhaa zao nyingi wanapitishia Bandari ya Mombasa.

View: https://youtu.be/yi8VlUZYe84?feature=shared
 
Kagame atamchukua Rais muda si mrefu. Mimi umoja umoja wa nchi za kiafrika unanichekesha sana sijui huwa una faida gani. Nchi hizi zote ni wanachama wa EAC lakini wala hazikemeani kwa kuambiana ukweli wala kulindana
 
It's true kwamba hali ya usalama mashariki mwa DRC, hususan katika Mji wa Goma, ni ya kusikitisha na inahitaji hatua za haraka. Ni wazi kwamba kundi la M23 linaungwa mkono kwa njia moja au nyingine na maslahi ya kigeni, jambo linalosababisha changamoto kubwa kwa majeshi ya DRC na hata kwa vikosi vya kulinda amani kama JWTZ.

1. Ushirikiano wa Kikanda
Tatizo hili haliwezi kushughulikiwa na JWTZ pekee. Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinapaswa kushirikiana kwa dhati kuhakikisha amani na usalama vinapatikana. Ushirikiano wa kijeshi, kiintelijensia, na kifedha kati ya nchi hizi ni muhimu katika kuzuia juhudi za vibaraka wa kigeni kama M23 kuleta vurugu zaidi.

2. Mgogoro wa Kihistoria
Mgogoro wa M23 si jambo jipya, bali ni suala la muda mrefu linalotokana na changamoto za kikabila, rasilimali, na ushawishi wa kigeni. Hatupaswi kupuuza kwamba DRC ni nchi yenye rasilimali nyingi zinazotamaniwa na mataifa makubwa. Hili limefanya baadhi ya nchi jirani kushawishika kuunga mkono vikundi vya waasi kwa maslahi yao binafsi.

3. Udhibiti wa Rasilimali
DRC ina rasilimali za kutosha kuinufaisha Afrika nzima, lakini badala yake, rasilimali hizi zimekuwa chanzo cha migogoro na ushawishi wa nje. Kama Afrika, tunapaswa kuungana ili kulinda rasilimali hizi kwa manufaa ya watu wa DRC na bara lote. Vita vya M23 si vita vya ukombozi, bali ni juhudi za kulinda maslahi ya mabeberu kupitia vibaraka wao.

4. Mapendekezo ya Haraka

Umoja wa Mataifa unapaswa kuongeza msaada wake kwa MONUSCO ili kuhakikisha wanajeshi wa kulinda amani wanapata vifaa na msaada wa kutosha.

Vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia vinapaswa kuwekwa dhidi ya nchi yoyote inayothibitika kuhusika na kufadhili M23.

AU na EAC zinapaswa kuongeza juhudi za kidiplomasia kwa kushawishi mazungumzo ya amani kati ya DRC na nchi jirani zinazotuhumiwa.


5. Ushauri kwa JWTZ
JWTZ linapaswa kuendelea kushikilia wajibu wake wa kulinda amani bila kuvuka mipaka ya majukumu yake. Tukumbuke kwamba JWTZ liko DRC kulinda amani, si kushiriki moja kwa moja katika vita. Hili ni muhimu ili kulinda taswira ya jeshi letu kimataifa na kuepuka matokeo ya muda mrefu kwa Tanzania.

6. Umuhimu wa Diplomasia
Badala ya kupigana vita vya moja kwa moja, juhudi za kidiplomasia zinapaswa kuimarishwa. Rwanda na nchi nyingine zinapaswa kushauriwa kuachana na siasa za kuunga mkono vikundi vya waasi. Hili linaweza kufanikishwa kupitia shinikizo la kidiplomasia na kisiasa kutoka kwa AU na jumuiya ya kimataifa.

Mwisho wa yote::;
Mgogoro huu hauwezi kutatuliwa na jeshi moja pekee au nchi moja pekee. Tunahitaji mshikamano wa kikanda na wa bara zima kuzuia uchokozi huu wa M23 na kuhakikisha kwamba DRC inabaki kuwa nchi huru na salama.
 
Kagame atamchukua Rais muda si mrefu. Mimi umoja umoja wa nchi za kiafrika unanichekesha sana sijui huwa una faida gani. Nchi hizi zote ni wanachama wa EAC lakini wala hazikemeani kwa kuambiana ukweli wala kulindana
Kwa kweli inashangaza ,haya maumojanyasiyo.na maana Bora Kujitoa tuu.

Yaani EAC Wameshindwa kuwakanywa Rwanda ,kwanza Inaelekea Tanzania pekee ndio Wazalendo wengine wote waliotuzunguka ni mawakala wa Mabeberu kina Rwanda,Uganda,Kenya nk.

Bila Tanzania hata Burundi ingeshaanguka Kwa vibaraka.
 
Wamefeli Kwa kupenda au Kwa kuzidiwa na vibaraka wa Mabeberu kina Rwanda na wengineo?

Hao wanatakiwa kusaidiwa acha upuuzi
 
Kagame atamchukua Rais muda si mrefu. Mimi umoja umoja wa nchi za kiafrika unanichekesha sana sijui huwa una faida gani. Nchi hizi zote ni wanachama wa EAC lakini wala hazikemeani kwa kuambiana ukweli wala kulindana
Wakemeane vipi wakati wote ni warafi wa madaraka na mafisadi.

Umoja wa afarika na east afrika bajeti inatolewa na mabeberu.

Waonikupeleka matumbo yao tu kwemye vikao na kula posho huku wakijadiri inshu yepesi nyepesi tu
 
Hiyo habari ya MONUSCO hapana Kwa sababu wamekuwepo hapo hakuna Cha maana wamefanya.

Swala.la.kuweka wanajeshi wa kulinda kinachoitwa amani ila hawawezi kwenda msituni kuwafurusha waasi Haina maana.

Rwanda inadai hao wa Tutsi wa huko Mashariki mwa DRC sio raia wake ila wanalazimishwa kuwa WanyaRwanda so inajihami Kwa kuhakikisha vita havivuki Rwanda.

Kwa staili hii kuna siku Nchi Mpya itapatikana hapo na ndio utakuwa Mwanzo wa DRC yote kusambaratika.

Sioni Nchi tofauti na Tanzania ya kusaidia.

Binafsi napendelea DRC ikubali kupata usaidizi wa Nchi za Kigeni Kwa makubaliano ya malipo ya Rasilimali maana hawana hela ila tuu Waasi wafurushwe wote Hadi kuweka na usalama wa kutosha na Jeshi lao liwe na uwezo wa kudhibiti Kila kitu.
 
DRC wana jeshi la nchi?
 
Binafsi napendelea DRC ikubali kupata usaidizi wa Nchi za Kigeni Kwa makubaliano ya malipo ya Rasilimali maana hawana hela ila tuu Waasi wafurushwe wote Hadi kuweka na usalama wa kutosha na Jeshi lao liwe na uwezo wa kudhibiti Kila kitu.
Kwa nini wasitumie hizo rasilimali zao kulipa wanajeshi wao wenyewe badala ya kuzipa nchi nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…