Maji Bwawa la JNHPP Yafikia Ujazo wa Mita Bilioni 6

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MAJI BWAWA LA NYERERE (JNHPP) YAFIKIA MITA ZA UJAZO BILIONI 6

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema wanaridhishwa na kasi ya ujazaji maji Bwawa la Kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere Hydro Power (JNHPP) ambapo kwa sasa ujazo wa maji umefika mita za ujazo Bilioni 6.

“Zimebaki mita kumi na tatu tu, kufikia kiwango cha maji yatakayoweza kuzungusha mitambo ya kufua umeme”.

Waziri Makamba amesema kiwango hiko ni kizuri na kimezidi matarajio yaliyokuwepo awali wakati wa uzinduzi wa ujazaji maji uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Maendeleo mazuri ingawa kazi bado ipo, kwa mujibu wa takwimu, kiwango cha maji yaliongia wiki mbili zilizopita, ni mengi kuliko maji yaliyoleta mafuriko 2019/2020, hii maana yake kwa neema ya mvua iliyopo kwa sasa, zile athari za mafuriko zilizokuwepo siku za nyuma hazipo tena”

“Bwawa hili limeanza kuzaa matunda tuliyotarajia ikiwemo kudhibiti mafuriko, kwa sasa ujenzi wa Bwawa kwa ujumla uko 86%, Wakati Mh. Rais Samia anachukua madaraka ya nchi mradi huu ulikua ni asilimia 37"
 
Attachments

  • FulLAKOWIBwr_n-.jpg
    FulLAKOWIBwr_n-.jpg
    57.4 KB · Views: 7
  • FulMhIEWIAYxGdQ.jpg
    FulMhIEWIAYxGdQ.jpg
    46.3 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-04-26 at 16.03.08.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-26 at 16.03.08.jpeg
    57.5 KB · Views: 6
Pamoja na yote mi huwa nashangaa kila leo mapori yanafyekwa na kugeuza makazi na umeme unasambazwa kila leo kwenye nyumba mpya lakini mabwawa au vyanzo vya umeme vinaongezeka kwa kusua sua
 
MAJI BWAWA LA NYERERE (JNHPP) YAFIKIA MITA ZA UJAZO BILIONI 6

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema wanaridhishwa na kasi ya ujazaji maji Bwawa la Kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere Hydro Power (JNHPP) ambapo kwa sasa ujazo wa maji umefika mita za ujazo Bilioni 6.

“Zimebaki mita kumi na tatu tu, kufikia kiwango cha maji yatakayoweza kuzungusha mitambo ya kufua umeme”.

Waziri Makamba amesema kiwango hiko ni kizuri na kimezidi matarajio yaliyokuwepo awali wakati wa uzinduzi wa ujazaji maji uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Maendeleo mazuri ingawa kazi bado ipo, kwa mujibu wa takwimu, kiwango cha maji yaliongia wiki mbili zilizopita, ni mengi kuliko maji yaliyoleta mafuriko 2019/2020, hii maana yake kwa neema ya mvua iliyopo kwa sasa, zile athari za mafuriko zilizokuwepo siku za nyuma hazipo tena”

“Bwawa hili limeanza kuzaa matunda tuliyotarajia ikiwemo kudhibiti mafuriko, kwa sasa ujenzi wa Bwawa kwa ujumla uko 86%, Wakati Mh. Rais Samia anachukua madaraka ya nchi mradi huu ulikua ni asilimia 37"
Mnazijua mita za ujazo bilioni 6 ama mnaongea tu vitu vya kimpompompo
 
Hapo hata maji ya ziwa victoeia hayafikii hizo mita cubic
 
Kazi nzuri,watu wanasubiri matokeo,hapo ndipo watakuelewa,kwasasa bado inaonekana ni blah blah,ila piga kazi,tunakukubali...
 
Nadhani ni Lita sio mita, mita Bilioni 6 ni kilomita milioni 6, mbali sana. Unaenda mbinguni, unapitiliza hadi jehanamu na unarudi tena mbinguni na kisha kurudi Duniani na kisha kwenda sayari ya mars ndio zinaisha kilomita milioni 6.
 
Ni ujazo wa mita billioni 6, au ujazo wa mili lita billioni 6??
 
Back
Top Bottom