Sasa langu linahusu makampuni ya maji, nitayataja kwa majina hapa, lengo wafikishiwe wadau nao wachunguze. Hili sijui ni kwa sisi tu wenye pua kali, ila Brand za maji za Uhai, Afya, Hill na GSM kwakweli zimekuwa kero kwa kuwa na maji yanayotoa harufu.
Unakuta umenunua maji mapya kabisa (nukuu vizuri, mapya kabisa) yale ambayo hayajawekwa kwenye friji yaani ya moto ila ukifungua tu ukasogeza mdomoni unywe unahisi zile harufu tunapataga za maji machafu.
Tofauti tu ni kwamba sio kali kwa kuwa maji yamepitia Industrial process ila bado yanabaki yana harufu na inaashiria kabisa kuwa kuna tatizo kuanzia source mpaka kwenye purification line.
Ni brand ya Dew Drop tu ndio ina maji mazuri yenye flavor na bila harufu, Watu kadhaa wamekutana na hilo ila wengi Bado hasa wanaotumia haya maji yakiwa baridi yaani kutoka kwenye friji (effect yake kidogo inakuwa imepungua nadhani kutokana na cooling). Ndugu jamii Forums naomba hata ww Fanya experiment yako, nunua maji ya Afya 1.5 Litres ya moto.
Fungua kisha nusa kabla ya kuyanywa. Utagundua ninachosema, Jaribu pia hata na Hill, Uhai na hata GSM pia. Maji haya nakutana nayo hapa hapa Dar es Salaam maana ndio mkoa yanapozalishwa na kunyweka kwa wingi.
Sasa sijajua kwa mikoani. Japo nahisi kwa mikoa yanapofika kesi itakuwa ni hiyo hiyo maana sifikiri kwamba mabadiliko ya kijiografia yana mchango wa kuleta matokeo tofauti katika hili suala. So ni kwenye maduka ya hapa mjini Dar es Salaam karibu Kila Kona