Kuna mahali kanisa linakwama kwa kupunguza mafundisho ya imani kwa watoto, nashindwa kuelewa inakuwaje unajiita Mkatoliki na bado hauelewi ukuu wa Mama Bikira Maria katika historia ya Ukombozi, na jukumu alilokabidhiwa na Yesu Kristo pale msalabani na baada ya kufufuka kabla hajapaa.
Unashindwa hata kuelewa kwanini Mama Bikira Maria ndie Sanduku la agano lililoptea pale mlimani, likaja kuonekana kwa ishara mawinguni baada ya kupalizwa?
Bado huyo unamuita ni mwanadamu wa kawaida? Ungesema wewe si Mkatoliki kidogo ningekuelewa, japo kuwa Mkristo tu kunakufanya ufahamu vitu kama hivi.