Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,036
- 9,331
Yale maji ya Kilimanjaro ambayo hapo awali yalijizolea sifa kwa ubora, sasa hivi inasikitisha sana kwa jinsi walivyoamua kuachana na njia zilizoyafanya yakawa na ubora wa juu kuliko washindani wao wengi.
Hapo awali maji haya ya kilimanjaro yalikuwa yakiwekwa katika maboksi kwa ajili ya usafirishaji kutoka sehemu moja hadi nyingine. Maboksi haya yalisaidia sana kuzuia mionzi ya jua isipige kwenye chupa zake ambazo kikawaida maji yanyopigwa sana na mionzi ya jua hupoteza ladha yake kutokana na harufu mbaya ya plastic katika maji.
Kitu kingine ni kwamba Wataalamu wa Afya pia, wanasema maji yaliyowekwa kwenye plastic, yakipigwa na jua husababisha kiwango fulani cha upako wa kiplastic kuyeyukia kwenye maji na hivyo kuhatarisha afya zao, baada ya matumizi ya muda mrefu wa maji ya aina hiyo. Miongoni mwa madhara ya maji ya plastic yanayopigwa na joto la jua ni Upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume (Unaweza kugoogle, Plastic bottled water and Male Impotence).
Ni matumaini yangu kwamba kampuni ya kilimanjaro itaangalia uwezekano wa Kurudia packaging yao ya Zamani, kuliko kujishusha kutoka hatua nzuri kwenda kwenye hatua duni.
halafu pia packaging yao hii mpya wanayoifanya kwa kuweka chupa zao kwenye mifuko ya Plastic, itachangia sana uharibifu wa mazingira, kwa sababu mifuko hii siyo reusable. kwa maana hii watakuwa hawaitendei haki nembo yetu ya mlima kilimanjaro ambayo theluji yake inakaribia kuyeyuka kutokana na tabia joto kuwa kali zaidi. na miongoni mwa tabia joto hizi ni kutokana na uchomaji wa maplastic
Haya ni maoni yangu mtu aliyekuwa mteja mkubwa sana wa maji ya kunywa ya kilimanjaro. Naomba yeyote anayeweza kuwasiliana na kampuni hii afikishe maoni yangu haya!