Maji ya Kilimanjaro katika mtindo wa packaging mpya

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Posts
7,036
Reaction score
9,331
Yale maji ya Kilimanjaro ambayo hapo awali yalijizolea sifa kwa ubora, sasa hivi inasikitisha sana kwa jinsi walivyoamua kuachana na njia zilizoyafanya yakawa na ubora wa juu kuliko washindani wao wengi.

Hapo awali maji haya ya kilimanjaro yalikuwa yakiwekwa katika maboksi kwa ajili ya usafirishaji kutoka sehemu moja hadi nyingine. Maboksi haya yalisaidia sana kuzuia mionzi ya jua isipige kwenye chupa zake ambazo kikawaida maji yanyopigwa sana na mionzi ya jua hupoteza ladha yake kutokana na harufu mbaya ya plastic katika maji.

Kitu kingine ni kwamba Wataalamu wa Afya pia, wanasema maji yaliyowekwa kwenye plastic, yakipigwa na jua husababisha kiwango fulani cha upako wa kiplastic kuyeyukia kwenye maji na hivyo kuhatarisha afya zao, baada ya matumizi ya muda mrefu wa maji ya aina hiyo. Miongoni mwa madhara ya maji ya plastic yanayopigwa na joto la jua ni Upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume (Unaweza kugoogle, Plastic bottled water and Male Impotence).

Ni matumaini yangu kwamba kampuni ya kilimanjaro itaangalia uwezekano wa Kurudia packaging yao ya Zamani, kuliko kujishusha kutoka hatua nzuri kwenda kwenye hatua duni.

halafu pia packaging yao hii mpya wanayoifanya kwa kuweka chupa zao kwenye mifuko ya Plastic, itachangia sana uharibifu wa mazingira, kwa sababu mifuko hii siyo reusable. kwa maana hii watakuwa hawaitendei haki nembo yetu ya mlima kilimanjaro ambayo theluji yake inakaribia kuyeyuka kutokana na tabia joto kuwa kali zaidi. na miongoni mwa tabia joto hizi ni kutokana na uchomaji wa maplastic

Haya ni maoni yangu mtu aliyekuwa mteja mkubwa sana wa maji ya kunywa ya kilimanjaro. Naomba yeyote anayeweza kuwasiliana na kampuni hii afikishe maoni yangu haya!
 
Kama watadharau ushauri huu,wahesabu maumivu muda si mrefu. Sijaelewa mantiki ya kubadili mfumo wao wa awali,hata kama ni sababu za kulinda miti/mapori kwa sababu wanatumia maboxisi yanayotokana na mbao ,ni bora wakaangalia namna nyingi kuliko kutumia maplasti wanayotumia kwa sasa.

Ukiacha hilo hapa Kati 2013 - 2014 kumekuwa na uchakachuaji au uzalishaji mbovu,maji yao yalipoteza ile quality ya zamani na tumai watatembelea uzi huu kwa faida yao.

Sijui Dasani wamepotelea wape ,hawa jamaa nao walikuwa na maji mazuri kiasi.
 
Wadau,mwenye namba ya simu ya kampuni ya Kilimajaro drinking water aiweke hapa ili tuwaulize kwa nini wameamua kuyashusha hadhi maji yao yaliyopendwa.
 
hata maji yenyewe sio yale yazamani kuna wajanja wanauza maji yao kwa jina hili kama ilivyo kwa uhai ya kariakoo na magomeni mataa
 
hili la kupack maji ya Kilimanjaro kwa kutumia poly paper wamelazimishwa na coca cola company kwani maji ya Kilimanjaro yapo under trade name ya coca cola
 
Kama mtakumbuka kampuni hii iliacha kutumia chupa zilizokuwa nzuri na kuanza matumizi ya chupa za sasa ambazo kwa mtazamo wangu ni poor. Tutegemee waanze kupack Maji kwenye nylon kwa kisingizio cha kuongeza ubora. Kama biashara imewashinda wawaachie uhai, Dasani au wadau wengine
 
hili la kupack maji ya Kilimanjaro kwa kutumia poly paper wamelazimishwa na coca cola company kwani maji ya Kilimanjaro yapo under trade name ya coca cola

Mkuu wameingia lini wakiwa chini ya cocacola na hiyo packaging nayo imeanza kufungwa lini mkuu hivi ni kweli wamelazimishwa baada ya kuwa chini ya coke au walishakuwa chini ya coke muda mref wakati hii packaging ndio kwanza imeletwa mtaani hivi punde tu mkuu naomba unijuze tafadhali.
 
Back
Top Bottom