Maji ya kisima kutoa mafuta

Maji ya kisima kutoa mafuta

TUTYIANNA

Member
Joined
Jan 23, 2021
Posts
7
Reaction score
92
Habari za mchana!

Naomba kujuzwa na wenye uelewa zaidi!

Kaka yangu ana eneo huko Pwani ambapo amechimba kisima pia kwaajili ya matumizi yake ya nyumbani hapo! Sasa kumekuwa na hali ya maji hayo yakichotwa then yakalala kwenye ndoo au chombo chochote yanatoa layer ya mafuta!

Je ni hali ya kawaida tu? Au itakuwa crude oil? Tuna shauku kubwa ya kujua, tafadhali mwenye uelewa atusaidie kutuelimisha!

Natanguliza shukrani
 
Kisima kilichimbwa mita 65 kwenda chini!

Msaada wenu tafadhali
 
Ngoja nikae maana nimeshuhudia kwenye bonde langu pia kuna kisima kilichimbwa cha ku pump ila maji yana layer ya mafuta na pia hata kwenye udongo around, mvua ikinyesha kuna mafuta mafuta pia.
 
Kawaida sana hiyo, kwa tulioshi vijijini ni kitu cha kawaida kwa maji ya visima vile tunavyofukua temporary.

Unforgettable
 
Picha tafadhari. Mimi sijaelewa vzr😁
 
Inatokana na decay ya organic contents zilizopo sehemu husika! Nenda kwa watu wa maabara wakupimie ili ujue exactly ni elements gani na kama hakuna madhara kiafya.
 
Duh asanteni wakuu maana nimefatilia zaidi nimeambiwa crude oil ni nyeusi tii! Na kisima cha mita65 ni kifupi kutoaa mafuta!
 
Pitisha mwenge wa moto hapo kwenye layer ya juu uone kinachotokea.
 
Chemba ya choo hiyo kuweni makini
Pwani maeneo ya kibaha hadi bagamoyo yana mafuta na kuna mradi uanendelea wakutafiti yamepitiwa na mradi hivyo sio ajabu kuanzia mlandizi vigwaza saeni
 
Back
Top Bottom