Maji ya mvua ni salama kwa kunywa?

Water guard haitakusaidia chochote kwani asilimia kubwa ya maji hayo hayana vimelea lakini yanaweza kuwa na dusts. Asilimia kubwa ya matatizo ya Rain water ni toxic chemicals, coat ya Carbon, Impurities za kutu zilizotoka kwenye mabati n.k. Sidhani kama kuchemsha maji au WaterGuard itasaidia kwenye Acidic Rain au Toxic rains. Nop
 
Maji ya kuchemsha hayana ladha. Sithubu kabisa kuchemsha kwasababu ukichemsha unaua vile vijidudu, alafu vikifa si vinakuwa marehemu?!! Vikioza sasa!!! Bora kuvinywa vizima na utamu wake.
Hahaha umenichekesha mkuu
 
Dah! Mimi niliyakinga kwenye mvua ya juzi. Nimejaribu kuyanywa hayapiti kooni. Sijui hawa wakina Bakresa wametuwekea nini kwenye maji yao... Ngoja tu tuendelee kuwaunga mkono...
 
Nimeikuta nikaona si mbaya tukishare

Kwa ufupi
Kwa asili yake maji ya mvua kabla hayajafika katika anga letu huwa ni safi na salama kwa kunywa. Hata hivyo, maji hayo lazima yapite katika anga na ndipo yafike ardhini kama mvua.

Maji ya mvua ni salama kwa kunywa?
 
Maji ya Mvua, Maji ya kwenye mito, Maji yanayotiririka kwenye milima ( water falls) ... Ni dawa kubwa sana.

Pendelea kuoga na kunywa maji Haya.

Ni mazuri pia kwa kukuweka kuwa karibu na Mungu.

Kama wewe ni muislam au mkristo, pendelea kutumia maji haya kwa sala, toba , kutawaza n.k

Ni salama sana. Hayana madhara.

Maji ya kuchemsha hayana dawa!
 
Inategemea mazingira ya maji hayo. Kwa mfano maji ya mvua inayonyesha maeneo kama mijini ambako kuna uchafuzi mkubwa wa mazingira si salama. Pili, yanaweza yakawa maji ya mvua ambayo ni salama lakini ukayatunza katika chombo (Tank) ambayo ni chafu. Maji hayo yatakuwa si salama tena. Usalama wa chakula cha aina yoyote ikiwemo maji inategemea mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na wewe binasi unavyohandle hicho chakula.
 
Kinga maji ya mvua kwenye chombo kisafi, hakikisha bati halina kutu, yachemshe hapo unaweza kuyatumia kwa kunywa. Hakikisha hutumii maji ya mvua ya kwanza ya msimu hayo sio salama kwa kiasi kikubwa.

Duc In Altum.
 

Chumvi inasaidia nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…