Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MAJI YA ZIWA VICTORIA YAFIKA MGONGORO - JIMBO LA IGUNGA
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga (IGUWASA) imefanikiwa kufikisha huduma ya maji safi ya Ziwa Victoria kwenye Kijiji cha Mgongoro, Jimbo la Igunga. Huduma ya Maji imefika kijiji cha Mgongoro kufuatia IGUWASA kulaza bomba la maji safi mpaka kwenye matenki ya maji yanayohudumia Kijiji cha Mgongoro yaliyopo kijiji cha Mwalala, kata ya Nguvumoja.
Mradi unatarajia kuhudumia vitongoji viwili vya Mwamayoka na Mwamsunga, ambavyo vina jumla ya wakazi 4,480.
#KaziNaMaendeleo
#KaziIendelee