bellan2020
New Member
- Sep 13, 2022
- 2
- 1
Ufugaji wa Samaki aina ya sato kwa mikoa ya Shinyanaga na Tabora ni ukombozi mkubwa sana kutokana na mradi wa maji toka ZIWA victoria,mradi huu unaweza kuwa Msaada mkubwa sana hasa kwa vijana ukizingatia changamoto za ajira nchini zinavyoshika kasi.
Vijana wa Shinyanaga na Tabora tutumie maji haya kuanzisha ufugaji wa Samaki kwani ni moja ya kujikwamua kiuchumi,
Pia tutumie fursa ya Mikopo ya Halmashauri kama njia mojawapo ya kupata mitaji kwaajili ya shughuli hii.
Viongozi wa majimbo wakiwemo wabunge wanaopitiwa na mradi huu wajitolee katika kuwasemea na kuwasaidia vijana wa maeneo haya kwani Viongozi hawa wanao ushawishi mkubwa sana wakutafuta wataalamu wa Samaki na vijana wakapatiwa elimu hiyo kwa uweledi zaidi, Faida za shughuli hii itasaidia vijana kupata ajira hivyo kupata pesa na mwisho wa siku kupunguza umaskini uliopo kwasasa, pia shughuli hii itasaidia kupunguza makundi ya kihalifu katika jamii kwani vijana wengi watakuwa na kazi muda mwingi, ufugaji wa Samaki pia utaongeza mapato ya serikali za mikoa husika kwa kutakuwa na kodi mbalimbali ambazo wafugaji watalipa kwa njia moja au nyingine
Napendekeza serikali ifanye haya Ili kusaidia hii shughuli ifanyike vizuri,,
Mosi,itoe elimu na faida juu ya faida na umuhimu wa ufugaji wa Samaki kwa jamii yote INAYOPITIWA na mradi huu wa maji toka ziwa victoria.
Pili,Serikali ipeleke wataalamu wa Samaki maeneo hayo Ili wananchi wapate uweledi zaidi juu ya ufugaji wenye tija.
Tatu,Serikali itengeneze Miundombinu mizuri ya barabara Ili kurahisisha usafirishaji wa vifaranga kutoka vituo vya kuzalishia kwenda kwenye mabwawa au matangi eneo la mradi.
Nne,Kuwepo na viwanda vya uhakika kwaajili ya Samaki wataokuwa wanazalishwa na vijana wa Shinyanaga na Tabora hivyo utoshelevu utafikiwa na wananchi watapata hamasa zaidi.
Tano,Kuwepo kuna mashamba darasa ya Ufugaji wa Samaki katika ngazi ya Kata na vijiji hii itatia hamasa zaidi.
Haya yote yatachochea sana ufugaji huu wa kutumia maji asilia ya sato,hivyo kibaiolojia tutakuwa tumepunguza yale matatizo au changamoto ambayo sato angekutana nayo endapo maji mengine yangetumika pengine.
Mwisho napenda kuwaomba vijana wenzangu tuungane pamoja bila ubinafsi wowote tutafute pesa hasa halmashauri tutumie nguvu zetu panapowezekana Ili kupunguza gharama za uendeshaji pia tuwatafute wataalamu watupatie elimu na mahitaji yote ya ufugaji wa Samaki.
VIJANA tunaweza.
Mafanikio ni sasa .

Upvote
0