Maji yanafanyaje hadi yanazima moto? Maji yanaweza kuwaka?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habari wana JF.

Maji yanafanyaje hadi yanazima moto? Na kwa nini vitu vibichi huwa "haviwaki"? Pia inawezekana maji yakashika moto na kuwaka kama ilivyo kwa mafuta, ponbe nk? Kiufupi naomba kupata elimu juu ya moto na maji.

Natanguliza shukrani.
 
Habari wana JF. Maji yanafanyaje hadi yanazima moto? Na kwa nini vitu vibichi huwa "haviwaki"? Pia inawezekana maji yakashika moto na kuwaka kama ilivyo kwa mafuta, ponbe nk? Kiufupi naomba kupata elimu juu ya moto na maji. Natanguliza shukrani.
Haya mambo yalitufanye tusome Arts, sasa umri huu unaturudisha tena kule kule?

Ngoja nipate lunch kwanza nitarudi.
 
Habari wana JF. Maji yanafanyaje hadi yanazima moto? Na kwa nini vitu vibichi huwa "haviwaki"? Pia inawezekana maji yakashika moto na kuwaka kama ilivyo kwa mafuta, ponbe nk? Kiufupi naomba kupata elimu juu ya moto na maji. Natanguliza shukrani.

Embu tuangalie maji H2O, haya Ili moto uwake unahitaji hewa( O2) na kichocheo( organic materials). Ili moto uzime mfano mbao reaction inayotokea ni mchanganyiko

Moto una tafsiri yake kisayansi, kwa kifupi moto ni hali inayotokea ikiwa vitu vitatu vitakutana kwa wakati na mahali pamoja;
1. Oxygen atleast (16%)
2. Heat atleast 65 degrees centigrade na
3. Fuel (si kwa maana ya mafuta bali kitu chochote ambacho ni chakula cha moto) mf. Karatasi, mbao, nguo nk nk.

Pia kuna classes za moto ziko 6 na kila class ina namna ya kuuzima.

Kuna class za moto ambazo maji yanaweza zima na kuna class usithubutu kutumia maji.

Pia kujibu swali la kwa nini maji hayawaki ni kuwa ukirejea hapo juu kwenye tafsiri utaona ili moto utokee unahitaji heat zaidi ya 65 degrees ss maji temperature iko chini lakini hata yakiwa ya moto bado oxygen amount kwny maji ni kidogo kiasi cha kutosupport moto.

Moto tu pekee ni somo pana sana ukiachilia mbali namna ya kudeal nao, wataalam zaidi wataeleza mengine nimechoka kuandika wakuu.
 
Habari wana JF. Maji yanafanyaje hadi yanazima moto? Na kwa nini vitu vibichi huwa "haviwaki"? Pia inawezekana maji yakashika moto na kuwaka kama ilivyo kwa mafuta, ponbe nk? Kiufupi naomba kupata elimu juu ya moto na maji. Natanguliza shukrani.
Maji yanapooza moto kwa maana yanashusha joto kiasi cha kufanya moto usiwake kwa kufanya hivyo maji yanakuwa yametengeneza kinga kati ya kinachowaka na oxygen hivyo kupelekea moto kuzima kwa sababu kile kinachowaka moto kinakuwa kimepoozwa chini ya alama ya kulipuka. (Ignition point)
 
Maji hayawaki kwa sababu yanajumuisha atomu za hidrojeni na oksijeni ambazo tayari zipo katika muundo wao wa molekyuli ambao hauwezi kusababisha mwitikio wa kemikali wa kuchoma. Mchakato wa kuchoma unahitaji kuwa na kemikali zenye uwezo wa kuingia kwenye mchakato wa mwako, na kwa bahati mbaya, muundo wa molekyuli ya maji hauwezi kutoa mwitikio wa namna hiyo.
 
Ukimwaga maji kwenye moto, maji hufyonza joto kutoka kwenye eneo la moto. Kuna sababu kadhaa zinazoelezea kwa nini hii hufanya kazi:

Kufyonza Joto: Maji yanapoingia kwenye eneo la moto, yanayeyuka na kuyabadilisha kuwa mvuke. Mchakato huu wa kuyeyuka na kubadilika kuwa mvuke unahitaji joto. Maji yanaponyonya joto kutoka kwenye eneo la moto ili kufanikisha mchakato huu, hivyo kupunguza joto la eneo hilo na kusaidia kuzima moto.

Kuondoa Oksijeni: Maji inapobadilika kuwa mvuke, inaweza kuchukua oksijeni kutoka kwenye eneo la moto. Moto unahitaji oksijeni ili kuendelea kuwaka, hivyo kuondoa oksijeni kunaweza kusaidia kuzima moto au kusababisha mwako kuwa dhaifu.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa kumwaga maji kwenye moto kunaweza kuwa na athari zake kulingana na aina ya moto na vifaa vinavyochomeka. Kwa mfano, maji ikimwagwa kwenye mafuta moto au metali zinazoyeyuka inaweza kusababisha mlipuko au hatari zaidi. Katika hali nyingine, matumizi ya vifaa vya kuzima moto kama vile vumbi la kuzima moto au blanketi ya moto yanaweza kuwa na ufanisi zaidi.
 
Neil deGrasse Tyson hili swali angelitolea ufafanuzi makini..
Swali linaonekana simple ila si kama hivyo
 
Habari wana JF. Maji yanafanyaje hadi yanazima moto? Na kwa nini vitu vibichi huwa "haviwaki"? Pia inawezekana maji yakashika moto na kuwaka kama ilivyo kwa mafuta, ponbe nk? Kiufupi naomba kupata elimu juu ya moto na maji. Natanguliza shukrani.

Inaonekana ulikimbia chemistry kidato Cha pili.
 
Moto una tafsiri yake kisayansi, kwa kifupi moto ni hali inayotokea ikiwa vitu vitatu vitakutana kwa wakati na mahali pamoja;
1. Oxygen atleast (16%)
2. Heat atleast 65 degrees centigrade na
3. Fuel (si kwa maana ya mafuta bali kitu chochote ambacho ni chakula cha moto) mf. Karatasi, mbao, nguo nk nk.

Pia kuna classes za moto ziko 6 na kila class ina namna ya kuuzima.

Kuna class za moto ambazo maji yanaweza zima na kuna class usithubutu kutumia maji.

Pia kujibu swali la kwa nini maji hayawaki ni kuwa ukirejea hapo juu kwenye tafsiri utaona ili moto utokee unahitaji heat zaidi ya 65 degrees ss maji temperature iko chini lakini hata yakiwa ya moto bado oxygen amount kwny maji ni kidogo kiasi cha kutosupport moto.

Moto tu pekee ni somo pana sana ukiachilia mbali namna ya kudeal nao, wataalam zaidi wataeleza mengine nimechoka kuandika wakuu.
Shukrani. Nimepata mwanga.
 
Back
Top Bottom