Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
CHADEMA kimetoa majibu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kufuatia malalamiko ya mwanachama wake, Lembrus K. Mchome, aliyedai kuwa kikao cha Baraza Kuu Taifa cha Januari 22, 2025 kilikuwa batili kwa kukiuka Katiba ya chama.
Katika majibu yao, CHADEMA wameeleza kuwa barua ya Mchome ilikuwa ni rufaa kwa Msajili baada ya kutoridhika na majibu ya Katibu Mkuu, na si ombi la uchunguzi. Wamesisitiza kuwa Msajili hana mamlaka ya kisheria kusimamia uchaguzi wa ndani wa vyama wala kupokea rufaa za wanachama, bali jukumu lake ni kuangalia uchaguzi.
Hata hivyo, CHADEMA imesema iko tayari kuwasilisha taarifa iwapo Msajili ataeleza ni kwa mujibu wa kifungu gani cha sheria anahitaji taarifa hizo, na kwa madhumuni gani ya kisheria. Wamesisitiza kuwa malalamiko ya wanachama yanapaswa kushughulikiwa ndani ya mfumo wa chama.
=====
YAH: MALALAMIKO KUHUSU UKIUKWAJI WA KATIBA YA CHAMA CHENU
1. Tumepokea barua yako yenye Kumb.Na. HA.322/362/16/121 yenye kichwa hicho hapo juu. Katika barua yako ulitutaarifu kuwa mnamo tarehe 18 Machi 2025 ulipokea barua kutoka kwa mwanachama wetu Bwana Lembrus K. Mchome "akieleza kuwa, Kikao cha Baraza Kuu Taifa mlichofanya tarehe 22 Januari 2025 kilikuwa kikao batili kwa sababu hakikutimiza masharti ya Katiba yenu ili kuwa kikao halali." Aidha, kuwa "katika kikao hicho ndani ya ukumbiwalikuwepo wanachama ambao siyo wajumbe na baadhi ya watu hao walipiga kura kinyume na masharti ya Katiba yenu."
2. Kutokana na hayo malalamiko yako Ofisi yako imetuandikia, eti kwa mujibu wa Kifungu cha 5B cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura Namba 258 inaitaka CHADEMA Kuwasilisha maelezo kuhusu malalamiko hayo ya Bwana Lembrus K. Mchome ili "Msajili wa Vyama vya Siasa afahamuanachoeleza Bwana Lembrus K. Mchome ni kweli au hapana na achukue hatua stahiki endapo ni kweli.
3. Ukatutaka Kuwasilisha maelezo yetu katika ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa siyo zaidi ya tarehe 31 Machi 2024(sic) saa tisa na nusualasiri.
4. Katika barua yako kwetu hukuambatanisha barua ya Bwana Lembrus Mchome kwakobali ile aliyomwandikia Katibu Mkuu mnamo tarehe 18 Februari 2025. Lakini sisitunayo hiyo barua ya tarehe 15 Machi 2025 ya Bwana Lembrus Mchome kwako na ambayo alikuandikiaakikata rufaa kwako na alisema:
"Nakuandikia barua hii kukata rufaa kwa kutoridhika na majibu niliyopokea kwa Katibu Mkuu"
Aidha Akaendelea kudai:
Kwa mujibu wa kifungu cha 4(5) (b) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Ofisi yako ina wajibu wa kusimamia chaguzi za ndani ya (sic) ya Vyama vya Siasa.
5. Tunachokijua kwa mujibu wa barua ya Bwana Lembrus K. Mchome ni kuwa amekata rufaa kwako na si kuwa alikutakaufanye uchunguzi bali ameleta rufaa kwako.
6. Tunapenda kusema kuwa kwa uelewa wetu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Kifungu hicho cha 5B, ambacho unadaikinakupa madaraka ya kupewa unachokitaka, ni kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haina mamlaka ya kusimamia chaguzi za vyama vya siasa na si mamlaka ya rufaa kwa mwanachama ambaye hajaridhika na maamuzi ya Chama.
Aidha, sheria ya Vyama vya Siasa haiipi ofisi yako madaraka ya kusimamia uchaguzi bali kuangalia uchaguzi. Hivyo kwa kuwa Ofisi yako si Mamlaka ya Rufaa Chadema inasema kuwa takwa lako kwetu ni kinyume cha Katiba ya Chadema na kinyume kabisa na Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
7. Bila kubadilisha tuliyoyasema hapo, Chadema itakuwa tayari kabisa kukupa taarifa unazozitaka kama utatueleza kwa kina na wazi kabisa kuwa kwa taarifa hizo zitakuwezesha kutekeleza kifungu kipi cha Sheria ya Vyama vya Siasa kinachoipa Ofisi yako madaraka ya kupokea na kuamua rufaa za wanachama wa vyama vya siasa kwa upande mmoja au taarifa hizo zinaiwezesha Ofisi yako kutekeleza jukumu lipi la kisheria juu ya taarifa za vikao vya kawaida vya chama cha siasa.
8. Tunatumai kuwa Ofisi yako itatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kushughulika suala hili kwa kuheshimu Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na vile vile kujua kuwa mwanachama yeyote yule wa Chadema anatakiwa kutumia vyombo vya ndani vya chama kupata suluhu la malalamiko yake.
Pia, Soma

- Mchome amuomba Msajili kutengua maamuzi ya Baraza Kuu la CHADEMA kwa kukiuka Katiba
- Msajili wa Vyama vya Siasa aipa wiki moja CHADEMA ijibu barua ya Mchome
- Barua ya CHADEMA ikimjibu Lembrus Mchome kuhusu malalamiko ya kupitishwa kwa viongozi kinyume na katiba ya chama
- Pre GE2025 - DSM - CHADEMA imeazimia kutofuata maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa. No reforms No election kuchanja mbuga