Majibu ya David Kafulila kwa Zitto Zuberi Kabwe kuhusu uchumi wa kati

Hoja za kafulila ni ukweli mtupu, kama mzee wa msoga alibugi lazima isemwe, hayo sio matusi ewe nyumbu.
Sasa kajibu wapi hoja za zito?
Kwani zito alikataa kuwa ccm haikukodisha ndege mbovu kwa mapesa kibao?
 
Sawa tunakubali kupitia makaratasi ya wazungu nchi yetu iko uchumi wa kati na hiyo ni one angle (economic growth model) ya kuangalia maendeleo ya uchumi ila hao hao wazungu wake Kafulila waje sasa wafanye utafiti wa angle ya pili inaitwa human development index inayoangalia maisha halisi ya watu , aina ya nyumba wanazoishi watu, idadi ya watu walalao katika chumba kimoja , virago wanavyolalia , upatikanaji na ujazo wa maji ya kunywa, nguo wavaazo watu, aina na kiwango cha chakula kwa kila raia nk!

Huyu Kafulila hana njaa asikurupuke alete wazungu waje sasa kutafiti na kuona familia ngapi kwasasa bongo zinamudu japo mlo mmoja kwa siku na kuvaa viatu badala ya yeboyebo?! familia ngapi zinamudu kulipia japo vipimo tu mmojawapo anapoumwa? ni familia ngapi zinamudu kununua uniforms za shule za watoto? ni familia ngapi zinamudu kulipa nauli na kusafiri kutembelea ndugu , kuhudhuria harusi na kuhudhuria mazishi? ni familia ngapi bongo kwasasa zinaweza kuweka akiba ya pesa benki ? ni chache tu mojawapo ni familia yake yeye!!

Jibu kuu ni kuwa uchumi huu wa kati utaonekana kwa zile familia za wafanyakazi wa formal sector tu ambao ni less than 10%, ikimaanisha mamilioni ya raia tuliobakia wote tuko hoi tumegeuka maskini hohehahe sababu sote tuko na self employments kwenye informal sector isiyo na mzunguko wa pesa uliokatwa na sera za sasa za matumizi ya pesa za umma!!

Kwasasa zaidi ya watu millioni 50 bongo wameangukia kuwa familia maskini sababu hawana tena reliable income na hawako kwenye formal sector ambayo ni only 8% according to the website ya ofisi ya takwimu, zaidi ya 90% ya raia katika utawala huu wa Magu wako pembezoni kwenye small scale kilimo uvuvi na biashara na wanategemea kuishi kwa mzunguko wa pesa ambao umekata kabisa kwasasa sababu serikali inachukua kodi kubwa na kulipa wageni wanaojenga miundombinu kama waarabu na wachina na ambao hupeleka kwao hizo pesa!! Mzunguko wa pesa pia umekata sababu pesa zingine nyingi zikinunua moja kwa moja vitu mf pesa yote iliyolipia ndege zetu ilitoka kwenye mzunguko huu huu na imeacha maumivu ya kutisha kwenye uchumi wa walalahoi!!shimo ililoacha halijazibwa!!

Kwa upande mwingine pia kutokana na lawama za wafadhili kwa kudorora hali ya usalama kwa wapigania demokrasia nchini basi ukichanganya na athari za COVID19 ufadhili umekata sana kwa serikali na kukata kabisa kwa NGO hivyo kupunguza mno pesa zilizokuwepo katika mzunguko hasa wakati wa Mkwere wazungu walimwaga pesa nyingi mno ya ufadhili ambayo waliifurahia pia kuona iliishia kwenye matumbo ya watu na si kuendeleza nchi!! kukata kwa misaada
ya wafadhili kumeleta hali ngumu mno kwasasa bongo pesa hakuna, njaa ni kali mno kwasasa kwa mamilioni ya watu!! watu wana hasira si kitoto!!

Ingekuwa nchi hii haina magari ya washawasha , matumizi ya mabomu ya machozi, na matumizi ya nguvu na FFU wanaopiga watu kwa sifa, ingekuwa nchi hii ina utawala wa sheria na kuruhusu freedom of opinion, expression and assembly, ingekuwa nchi hii iko katika bara jingine na sio Afrika bara la giza , ingekuwa nchi hii ina mamilioni ya watu walio na civic education ya kutosha , ingekuwa nchi hii ina watu walioshiba vizuri chakula na kuweza kutulia na kuwaza mambo yao na si wale wanaohangaika kila kukicha eti kutafuta japo mlo mmoja tu kwa siku , ingekuwa nchi hii haina raia waoga , ingekuwa nchi hii ina kina ZZK mia tu basi muda huu kwa jinsi watu wanavyoteseka kusingekalika kwa maandamano yasiyoisha ya kupinga hali ngumu na kuitaka serikali iondoke madarakani!!sie tulie huku Geita mitaani tunaona watu wengi wanashindia uji na karanga!!

Kafulila ana mahali pa kupata mlo unaotokana na kodi za wanyonge ni vigumu kwake kujua ni kwa kiwango gani mamilioni ya raia wanateseka kwa njaa na magonjwa na kukosa hata nguo za kutokea , Kafulila anapaswa kujua mtaani hakuna sherehe na uchumi wa kati hauna maana yoyote kwasasa kwa mamilioni ya watanzania wanaoshindia mlo mmoja tena si balanced! Kafulila ajue sasa we have a fake economy in Magu era, pole mno zaidi kwa wabongo maskini waishio mijini tuliozoea cash sababu serikali inatoa pesa kwenye mzunguko kupitia kodi kisha inapeleka kwa makandarasi wanaozitoa nje pesa hizo!! katika miaka mitano ijayo ya Magu kila kitambi kitakwisha na kila goti litapigwa!!

Kwa mujibu wa Nape nilimsikia mwenyewe akiongea bungeni huku swahiba yake Mr Februari yuko pembeni akichekelea ni kuwa Mkulu hatimizi ilani ya sisiem waliyoitengeneza wao na waliyomtuma ilani ya sisiem ya sasa inayotaka maisha ya raia kuboreshwa , watu wawe na afya, chakula , nguo na furaha! leo hii kila mtu amejaa utapeli ili kujinusuru na hali ngumu!!

Kwasasa serikali imeweka ilani kapuni haijali tena maisha ya watu walioiweka madarakani inaangalia kujenga miundombinu tu, ila ukweli familia nyingi bongo zimeingia kwenye umaskini wa kutisha baada ya kufeli biashara zao kutokana na kulipa kodi kubwa na wateja hamna sababu serikali inaondoa pesa kwenye mzunguko kulipa foreign contractors and brokers!

Kutokana na ukali wa askari wa bongo na uoga wa asili na dharau za watanzania watakubali kuteseka kwa miaka mingine mitano ya Mkulu na amani itadumu raia wakimsubiri Mkulu amalize miaka yake mitano ya mwisho wamtukane na kumzomea popote atakapoenda iwapo miradi ya kimkakati haitakamilika!!

Mimi ni shabiki kindakindaki wa Mkulu na namshauri ili uchumi huo wa kati utufikie mitaani basi katika ngwe ya pili ya lala salama Magu needs to be mkali times two, apunguze wapinzani bungeni times two, aondoe mikutano ya siasa times two, awabane kina DJ Makengeza na ZZK times two (wawe na kesi za uchochezi times two), apunguze na kulibana baraza la mawaziri times two, atumbue wazembe times two sababu kawatisha raia kuigopa serikali, kawabana raia kwenye maisha sasa ni muhimu kusimamia kibabe miradi mikubwa ya kimkakati adeal na mawaziri perpendicular ahakikishe miradi yote mikubwa imekamilika kabla ya wakati basi raia wema wa bongo watasahau shida za miaka yote na Mkulu atachukua CREDITS zote na kila atakapopita raia watamwimbia nyimbo na mapambio!! Mkulu atakuwa shujaa and the best President of Tanzania of all times na lazima tumuandike kwenye vitabu vya shule kama mfano wa uongozi bora kwa nchi masikini.
 
Watu wamesahau kua david Kafulila ndiye alikua mtu wa kulipua mabomu yote ya vikao vya bunge la 10 yeye na pamoja na Slaa ndiye waliomfanya Zitto kufika hapo alipo kwa utafiti wa hoja zao na kumpatia Zitto. Ukiangalia kwasasa Zitto anajitahidi sana kufikia viwango vyake vya mwaka 2010-2015 lakini anashindwa sababu hana vichwa kama hivi tena
Huyo jamaa hatari sana
 
UCHUMI WA KATI NA REKODI SABA ZA JPM KIMATAIFA

Na David KAFULILA

Julai1, 2020 ni tarehe itakayobaki kwenye kumbukumbu kama siku ya kwanza ya kuanza kwa utekelezaji wa Bajeti ya tano na ya mwisho ya kumalizia miaka5 ya kwanza ya awamu ya tano.

Siku ambayo Benki ya dunia ilitambua Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa kati, ikiwa ni miaka5 kabla ya kufikia mwaka 2025.

Katika kujadili mafanikio haya ningependa kukumbusha rekodi SABA (7) za JPM kimataifa kama sehemu tu kutafsiri mafanikio haya kwa kumbukumbu za kizazi hiki na kijacho;

# Kwanza, nikuweka kumbukumbu kwamba wote waliokuwa wakijiuliza JPM ANAJENGA nchi ya namna au analipeleka wapi Taifa hili kama ilivyo kwenye topic moja jukwaa maarufu la JamiiForums.

Julai mosi, 2020 Benki ya Dunia wamejibu!
Wamejibu kwamba JPM alikuwa anatuleta uchumi wa kati kabla ya mwaka 2025!

# Pili, rekodi iliyotolewa na IMF kupitia aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo, Bi Christine Legarde alipohojiwa na Jarida maarufu la Quartz, mwaka 2017 akiwa Addis nchini Ethiopia.

Alipoulizwa ni nchi zipi Afrika zinaelekea Vietnam kwa mapinduzi ya viwanda, alizitaja Tanzania , Ethiopia , Nigeria na Kenya.

Hili ilikuwa jibu kwa Watanzania waliokuwa wakihoji kama kweli Serikali ya JPM inajenga uchumi wa viwanda. Kwamba kinachoendelea Tanzania kuhusu ujenzi wa viwanda kinatambulika duniani!

# Rekodi ya tatu ni ile iliyotolewa kwenye jukwaa la kimataifa kuhusu Uchumi ( World Economic Forum 2018), ambapo Tanzania ilitajwa kuwa Taifa kinara Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uchumi jumuifu
kwa maana ya uchumi unaobeba watu wengi ( inclusive economy).

Rekodi hii ilikuwa inajibu kama kweli Serikali ya awamu ya 5 ni Serikali ya wanyonge kweli au la!

# Rekodi ya nne, ni Serikali ya Tanzania kutajwa kuwa ya 28 kati ya nchi 186 duniani zilizofanyiwa tathimini kwa umadhubuti katika usimamizi wa matumizi fedha za umma.

Baadhi ya nchi zilizochwa mbali na nafasi zao kwenye mabano ni Kenya(70), Uganda(100), Malawi (106), Msumbiji (118), Ghana(61), Botswana (37).

Rekodi hii inathibitisha kuwa hata dunia inatambua kuwa JPM ANAJENGA Serikali yenye nidhamu ya matumizi hata kuwa na rekodi kubwa sio tu Afrika bali duniani.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya World Economic Forum, Excutive Opinion Survey 2019).

# Rekodi ya tano, ni Tanzania kutajwa kama Taifa kinara katika nchi 37 Afrika zilizofanyiwa utafiti katika vita dhidi ya ufisadi.

Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya The Africa global opinion survey 2019.

Tumetoka mbali jamani! mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Zama za kukodi ndege mbovu kwa dola milioni 43, inafanya kazi miezi 6 lakini miezi 37 ipo gereji ilikuwa mateso kwa Taifa hili la Mungu...( rejea ripoti ya CAG Aprili2020).

Leo chini ya JPM Serikali inanunua ndege mpya bombardier kwa dola milioni32, kiasi ambacho ni chini ya tulichotumia kukodi ndege mbovu iliyoishi gereji robo tatu ya muda wa mkataba.

Huu ni mfano mdogo tu kuonesha kwamba kama Taifa kuna miongo kadhaa tulipoteza na sasa Taifa linachukua heshima na nafasi yake !

# Rekodi ya sita ni imani ya wananchi kuwa Serikali yao inapambana na ufisadi, ambapo asilimia 72 ya watanzania walijibu kuwa Serikali ya Tanzania kweli inapambana na ufisadi ukilinganisha na asilimia 13 mwaka 2015( ripoti ya Africa Global opinion survey 2019).

Hii ni moja ya rekodi ya mapinduzi makubwa sana duniani.

Kuna mtaalamu mmoja alinichekesha kusema kwamba kuruhusu ufisadi pengine ilikuwa 'Expansionary policy'! Kwamba ufisadi uliruhusiwa kutanua matumizi kujenga uchumi!

Kwakweli uchumi unajengwa kwa mtindo huo ilikuwa uchumi wa' mishenitauni'.

# Rekodi ya Saba ni Tanzania kufanyiwa tathimini ya kimataifa kuhusu umadhubuti wa kiuchumi na kiubuka kinara Afrika mashariki kiasi cha kuzua taharuki nchini Kenya ( rejea Gazeti la nchini Kenya - The BusinessDaily, March4,2017).

Hii ni kwa mujibu wa tathimini ya Taasisi ya Kimataifa- The Moodys yenye makao makuu nchini Marekani.

Taasisi hiyo ambayo inaongoza duniani kwa kufanya tathimini hizi( Credit rating) ilifanya tathimini hii ya kwanza kufanywa Tanzania tangu tupate uhuru na ikaipa Tanzania daraja la B1 ikiwa juu ya nchi zote za Afrika mashariki zenye daraja B2.

Hizi ni kumbukumbu za dunia na zitabaki hivyo kama utambulisho wa JPM kimataifa achilia mbali kumbukumbu ya diplomasia kubwa aliyoitumia kukabili ugonjwa wa corona na kuziacha nchi zote duniani zikijiuliza iliwezekanaje corona iliyoyumbisha dunia nzima lakini ikashindwa Tanzania ya JPM.

Ninachosisitiza hapa nikwamba wakati JPM akifanikisha rekodi kubwa kiasi hiki kitaifa na kimataifa, vema tukakumbuka kuwa alipokea Serikali mwaka 2015 ikiwa hoi kiasi haikuwa na uwezo wa kulipa mshahara na deni la Taifa kwa mwezi.

Alipokea Serikali ambayo ililazimu kukopa ili kulipa mshahara na hivyo kukopa soko la ndani kwa riba kubwa ya asilimia 17 kwa hati fungani za mwaka mmoja kulinganisha na sasa ambapo Serikali inakopa kwa riba ya asilimia 4.8.

Serikali yenye dhiki inakopa kwa riba yeyote ( desperate government)!.... Ndani ya miaka5 JPM amefanikisha rekodi kubwa nchini kwenye kila sekta inayohusu maendeleo ya watu!

Amefanikisha kujenga Serikali yenye msuli kiuchumi katika tafsiri zote kiuchumi nchini na duniani.

Tuliojua rekodi hizi hatukushangaa kusikia rekodi ya Benki ya dunia kwa Tanzania kutangazwa kufuzu kuingia uchumi wa kati miaka 5 kabla ya mwaka wa lengo ambao 2025.

MWISHO

View attachment 1499570
Mkuu unatafuta ukuu wa mkoa? Tetea mkate wako
 
✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️
 
Watu wamesahau kua david Kafulila ndiye alikua mtu wa kulipua mabomu yote ya vikao vya bunge la 10 yeye na pamoja na Slaa ndiye waliomfanya Zitto kufika hapo alipo kwa utafiti wa hoja zao na kumpatia Zitto. Ukiangalia kwasasa Zitto anajitahidi sana kufikia viwango vyake vya mwaka 2010-2015 lakini anashindwa sababu hana vichwa kama hivi tena
😂😂😂
 
Back
Top Bottom