The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
Kwanza, tuwashukuru hawa jamaa wanaojiita G55 (kundi asi lililokuwa ndani ya CHADEMA) kujitokeza leo na kutangaza rasmi na kwa hiari yao wenyewe kuwa wanajiondoa CHADEMA. Ni vyema sasa kuwa wamekiri kushindwa kwa nia yao ovu wenyewe kwa midomo yao...
Pamoja na sababu zingine wanazozitaja za kujiondoa kwao CHADEMA, mimi nitajibu hoja yao moja tu....
Kwamba CHADEMA haina au haisemi itatumia mikakati au njia gani kuitekeleza agenda ya NO REFORMS, NO ELECTION hususani ktk "kuzuia uchaguzi wa mwaka huu 2025 usifanyike iwapo hakutakuwa na electoral reforms..."
Nawajulisha G55 kuwa njia na mikakati ya CHADEMA kuhakikisha kuwa Tanzania inapata mifumo HURU, ya HAKI, SAWA na ya KUAMINIKA ya uchaguzi kwa kuhakikisha kuwa kunafanyika reforms za kikatiba, kisheria na kikanuni ili wote kwa usawa tuingie kwenye uchaguzi iko very open and clear. Nayo ni hii hapa👇🏻👇🏻;
MKAKATI #1: Kuwashirikisha kwa kuwaelimisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara na makongamano ya ndani ili:
➡Wananchi waweze kuelewa kuwa kinachofanyika Tanzania kwa sasa sio chaguzi bali ni chafuzi. Ushahidi au case study ni chaguzi za mwaka 2019, 2020 na 2024..
➡Waelewe kuwa viongozi waliopo madarakani sasa hawakuwekwa na Kura zao bali waliiba kura, hawakushinda na walijitangaza tu kwa kutumia Jeshi la polisi, TISS na watumishi wa umma kama walimu, wakurugenzi wa halmshauri za wilaya, miji nk, watendaji wa kata na vijiji. Ushahidi au case study ni chaguzi za 2019, 2020 na 2024...
➡Waelewe kuwa, sababu ya kutotangazwa kwa viongozi wao wanaowachagua kwenye sanduku la kura ktk chaguzi hizo zote na badala yake wanatangazwa wa CCM ambao huwa hawashindi, ni ubovu wa mfumo wa sheria za uchaguzi unaokipendelea chama kimoja..
➡Waelewe kuwa, tangu ktk chaguzi za 2019, 2020 na 2024 kura zao wanazokwendaga kupiga asubuhi na mapema wakipoteza nguvu na muda wao hazina thamani tena maana sio zinazoamua nani awe kiongozi bali uamuzi wa nani awe kiongozi unakuwa tayari ulishafanywa mapema kabla hata ya kura kupigwa kwenye vituo vya kupigia na viongozi wa CCM kwa kuwatumia mapolisi, TISS na watumishi wa umma kama walimu, watendaji wa vijiji nk
➡Waelewe kuwa CCM na serikali yao hutumia udhaifu wa sheria za uchaguzi na Tume ya Uchaguzi inayotumia wateule wa Rais wa CCM (ambaye naye ni mgombea) kusimamia uchaguzi kuengua wagombea wa vyama vya upinzani ili CCM ipite bila kupingwa...
➡Waelewe kuwa mchakato wote wa uchaguzi hudhibitiwa (controlled) na Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais na mgombea pia. Mwenyekiti wa CCM ndiye anaiteua Tume ya Uchaguzi ya Taifa, anateua wasimamizi wote wa uchaguzi wakiwemo wakurugenzi wa halmshauri za wilaya, miji nk, watendaji wa kata na vijiji, walimu, manesi nk. Na yeye kwa kutumia mazingira ya namna hii yasiyo haki hutoa amri na maelekezo ya kupendelea chama chake na wagombea wa chama chake kwa kuengua wote wa vyama vingine...
➡Waelewe na kuamua, katika mazingira ya uchaguzi wa namna hii yasiyo HURU wala HAKI wala kuwa na UWAZI wowote wala KUAMINIKA wanakwenda kupiga kura ili iweje...?
➡ Waelewe na kuamua, kuwa, waende tu kupoteza nguvu na muda wao kupiga kura kwenye uchaguzi ambao CCM walishajitangazia ushindi tayari au wadai mabadiliko ya sheria za uchaguzi kwanza....?
➡Waelewe na kuamua kuwa, waende tu kupoteza nguvu na muda wao kupiga kura kwenye uchaguzi ambao mifumo yake haitambui thamani ya kura wanazopiga na hazihesabiwi ili kupata viongozi wawatakao au wadai mabadiliko kwanza ya mifumo ya sheria za uchaguzi...?
##NDO KUSEMA, wananchi tukielewa haya (na tayari tunaelewa) ni wazi kuwa hatutaweza kushiriki kwenye ujinga huu unaoitwa "uchaguzi" wakati sio bali ni "uchafuzi" tu. Hivyo uchaguzi hautafanyika maana hakuna atakayeenda kwenye vituo vya kuoigia kura kupiga kura..!!
Mkakati 2 Ku - engage makundi mbalimbali kama madhehebu ya dini zote za Kikristo, Waislamu, wabudha nk...
MKAKATI #3: Kuzii - engage taasisi na mashirika yote ya kidini zote nchini kama TEC, CCT, CPCT, BAKWATA nk ili wafungue macho na kuona shida ya mfumo wote mbovu wa uchaguzi ili nao wapige kelele kutaka kufanyika kwa electoral reforms....
MKAKATI #4: Kuzii - engage jumuiya za kiraia za kitaifa na kimataifa ili zione ubovu na hatari ya mfumo wa uchaguzi wa nchi yetu na athari zake. Mfano wa jumuiya hizo ni THRDC, TAMWA, UN, AU, SADCC, ICJ, Amnesty International, European Union, Commonwealth etc
MKAKATI #5: Kui - engage Jumuiya ya Kimataifa pamoja na nchi wahisani moja moja zinazoisadia Tanzania misaada mbalimbali ya kibajeti na maeneo mengine ya kiuchumi na kijamii...
Lengo ni kuhakikisha kuwa serikali ya Tanzania inapata mashinikizo makubwa na mazito kutoka ndani na nje ya nchi (international pressure) ili kufanya mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi ili tuwe na chaguzi huru, za haki, wazi, za kuaminika na za kidrmokrasia...
Hii itatuhakikishia kupata viongozi wanaowajibika kwa nchi na wananchi na hivyo kuharakisha maendeleo ya wananchi na kuondoa au kupunguza tatizo la rushwa na ufisadi nchini ambalo ndicho kikwazo kikuu cha maendeleo ya wananchi...
##Mikakati hii tayari imeshaonesha mafanikio makubwa ya kampeni ya NO REFORMS NO ELECTION kwani karibu nchi nzima sasa inaimba wimbo wa NO REFORMS, NO ELECTION..!!
##Hawa watu (G55) kwa jinsi walivyo wajinga vichwani mwao, hata hawajiulizi ni kwanini serikali na CCM wamem - retain Tundu Lissu kiongozi wa harakati za NO REFORMS NO ELECTION gerezani bila makosa. Hawajui kuwa huo ndio mwitikio wenyewe wa kampeni hii, kwamba, wanajaribu kuzima moto wa gesi kwa maji...!!
##Swali la kujiuliza ni kuwa, ina maana hawa G55 ni wajinga na wapumbavu wa kiwango hiki kiasi cha kutoelewa mambo haya rahisi kabisa...?
##It's better that they've conceded defeat and decided to give up. Tunawatakia kila la kheri huko watakakokuwa iwe kurudi shambani kulima nyanya au kuendeleza siasa zao huko CHAUMA....!
Moderator tafadhali iache hii mada ijadiliwe kwa kujitegemea. Isiunganishwe na uzi mwingine wowote kwa sababu maudhui yake ni unique