Jamani hii kweli ni historia kwa kipindi hiki ambacho taifa linakumbwa na misukosuko mikubwa.
Taifa lipo pabaya linakumbwa na hali kubwa ya umasikini na ufisadi. mzee kashindwa kabisa kujibu maswali ya watanzania walio wengi, ambao wanahoji juu ya hali yao ya umaskini itaisha lini, hali inayokithiri ya ufisadi itatokomezwa lini?
Maana mtu anaulizwa juu ya ufisadi tena sio dagaa ni ule ufisadi papa, yeye anajibu generaly eti kesi za rushwa zimeongezeka mahakamani. kwa nini asituambie lowasa, chenge, rostam na wengine watapelekwa lini mahakamani? ili warudishe fedha zetu. Kwa nini asituambie wale wababaishaji bandarini aliojigamba anawafahamu kwa majina watafukuzwa lini na hatimaye washitakiwe? na wale pia wauza madawa ya kulevya ambao alipelekewa majina yao ni wakina nani? watakamatwa lini?
Anaulizwa hali ya chama anasema mambo ni shwali wakati ukweli kila mwenye macho haambiwi tazama, anaona tu kuwa hali ya chama ni taaabani. chama kinaposhikwa na kuendeshwa na wenye pesa anasema ni shwari? chama kinakuwa si mali ya wanachama watu wachache wanataka kumnyanganya kadi mwanachama mwenzao hali ni shwari? jamani tuache ya historia tuangalie taifa letu linaelekea wapi? kuweka historia hakuna maana kama hali ya wanjonge itaendelea kuwa duni.
Mimi nafikiri mzee kaona hali ngumu na hii ni mikakati ya kushafisha njia 2010. Maana hata namna ambavyo simu zilikuwa zinapokelewa inaleta mashaka kwani simu zilikuwa haziingiliani na mazungumzo. halafu hivi huyu jamaa siku hizi tuseme amekuwa jiniasi sana kukariri data kiasi kile. au maswali haya yaliandaliwa majibu hivyo alikuwa na maswali kabla. ( wajinga ndio waliwao)
Halafu swali ambalo ni specific kwa mfano swali la kigoma kuna haja gani kujibu mpaka asikoulizwa ruvuma nk. au ni jinsi ya kupoteza muda na kufanya aonekane anajibu vizuri sana. hapana kama mimi ningelikuwa msahihishaji basi nafikiri unajua angepata ngapi ya mia. ( swali na maksi mbili unajibu kurasa nane unafikiri maksi zitaongezeka). Hapa ni kwa kiswahili tuachane na vituko vya siku ile anahojiwa na kabinti ka CNN.
Jamani tanzania hii umaskini umezidi kuna maswali ya wakina mama ambao wako kijijini hospitali ni umbali wa km 30, hawana redio wala umeme video wanaangalia kwa walanguzi wanaowatembelea kipindi cha mavuno tu. tena wanaangalia kwa malipo ya mazao( namaanisha kisado cha mahindi au mpunga). Hawa ni watanzania wenzetu ambao rais wao amewatenga. Anasema anaongea na watanzania watu hawa hawajui hata kama kuna raisi anaongea maskini. Leo nimesikitika kwani nimepokea barua kwa posta eti wananiuliza hivi kikwete amesema ataleta lini hospitali? Wanamaswali mengi mno. je watayafikishaje?
Mafanikio ya ziara moja wapo ni ya kuongea na tajiri eti alete chandarua kila kaya tanzania? Jamani hivi ninyi mnakubaliana na jibu simple kama hili? chandarua? Aibu!!! hivi tujiulize kuna haja ya kuwa ombaomba kiasi hichi. hii ni laana au ni kukosa ......, hivi tuchukue pesa inayotumika kwenye uchaguzi tu ya kununulia kanga zenye picha na maandishi ambayo nadhani kwa makusudi yanatengenezwa ili zikivaliwa picha na maandishi chagua sisi yanakuwa kwenye makalio. haziwezi kutupatia chandarua kwa kila mtanzania. sio katika kaya tu bali ni kwa kila mtz. Tuachane na hizo je mabilioni yanayoibiwa benki kuu je? Rada? Ndege ya rais? Madini? Yanayowatesa watanzania wenzetu mpaka wanapoteza maisha. Yote haya ni mabilioni ya fedha sasa kuomba chandarua! Tumefika sehemu mbaya. Watu wanaiba pesa zaidi ya ambazo tunaenda kuomba kwa kununulia chandarua tunasema tunawajua kwa majina. Halafu tunatabasamu sana tu. Tunaenda kuomba chandarua?
Tunasahahu wakina mama wanaokosa vitanda kwa ajili ya kujifungua mpaka walala chini, Hawa ni watanzania jamani kwa nini tusikirie matatizo haya jinsi ya kutatua. Tunakimbilia kuomba misaada ya kutudhalilisha.
Jamani tutaomba mpaka lini wakati Mungu ametupa kila kitu madini, maziwa, bahari, wanyama, mapango, misitu na watu wa kutosha milioni kama 40 hivi. hivi hatujiulizi watu kama uingereza ambao waliendelea na kufikia kuitawala dunia kwa kutumia time management tu. tusome maendeleo ya nchi kama singapore, china, japani nk.
Kuna nchi zimefanikiwa kwa kuwa na rasmali watu tu. je hizi nchi zingefikiria kuomba hata chandarua zingefika zilipo?
next time tumuulize hivi alipojibu swali huko majuu kuwa hajui kwa nini tz ni maskini? alitaka msaada wa nini? maana kahaidi maisha bora. sasa tena hajui chanzo cha umaskini atunongoneze hatutamuuliza hewani ilikua gia ya kuomba nini?