Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Shida vitambi vya madafu na malimao. Hovyo kabisa yule kocha
Kuna siku Ndairagije alizungumza vizuri sana kuhusu uchaguzi wake wa Kaseja badala ya Aishi Manula kwenye mechi dhidi ya Burundi
Alisema alimwita Manula lakini akamwambia anamaumivu, alipata injury kwenye mechi ya ligi kwahiyo anaomba wamuache
Watu hawakuelewa mazingira hayo wakawa wanalaumu lakini akasema yeye kama Kocha asingeweza kumlazimisha awepo National Team wakati kashamwambia anaumwa
Hayo ndio majibu ya kitaalamu na kiweledi hasa kwa mwalimu wa kiwango cha kufundisha timu ya Taifa. Tena Ndairagije alifunguka hiyo story baada ya watangazaji kumkomalia na hilo swali lakini mwenyewe hakuwahi kufungua mdomo kulizungunzia hilo kabda. Hiyo ndio professionalism
Juma Mgunda yeye mwenyewe watu wakisema wachimbe CV yake ni mashaka matupu