Majibu ya Juma Mgunda kuhusu kipa Aishi Manula 'very unprofessional'

Majibu ya Juma Mgunda kuhusu kipa Aishi Manula 'very unprofessional'

Jana nami nilishangaa sana, ajabu maneno yale yanatamkwa na kocha msaidizi,
Tuna safari ndefu sana kufika wenzetu walipo
 
Hivi manula na yule kipa namba mbili wa yanga yupi anastahili kuitwa timu ya taifa afadhali wangemchukua hata Benno Kakolanya
 
Ilitosha mwalimu huyo kusema tu hatujamwita kikosi cha taifa kwa vile kiwango chake kiko chini kwa sasa.

Hii ya kusema hatuendi kuposa ina uhusiano gani na Aishi Manula kuteuliwa kikosi cha timu ya taifa?Au kuna chuki binafsi iko nyuma ya kauli hii?
Binafsi alinishangaza, hizi ni chuki. Maelezo mengi yasiyo na maana yoyote.
 
Heheheheh

Ila manula pale hakuna kitu

Ana vituko Sana akiwa golini

Mi sijaona kipa anaefaa

Wote mapazia tu
 
Dah huyo kocha wamemwokota wapi mbona unprofessional kabsa
 
Nimeshangaa sanaaa, Kuona Kocha Msaidizi Wa Timu ya Taifa Anatoa Kaulii zisizo na Maadili tena Kwa Nchi Kama TANZANIA ambayo Inapambana Sanaa Kukuza Mpiraa Wake!

Kulikuwa Hakuna Sababu za Msingi za Kumuacha Golikipa Namba Moja Wa Simba AISHI MANULA..!! Hata Kama Sababu Zilikuwepo Za Kifundi, Kocha Alitakiwa Kuzieleza na Sio Kutoa Maneno Ya Shomboo na Ya Kejeli Kwa Aishi Manula Kama amekuja Kumkomoa! Alitakiwa Kuelezea Sababu za Kiufundi zilizofanya kumuacha AISHI MANULA kama Swali lilivyokuwa Limeulizwa! Au angeweza kusema Hawezi kujibu hilo swalii, au angeleezea kiwango cha sasa cha AISHI MANULA kulinganisha na wale walio Itwa.

Nanukuu Kocha Juma Mgunda Anasema “HATUCHAGUI SURA YAKE,HATUJI KUPOSA” Kauli Hii Sitaki Hata Kuanza Kuangalia CV ya Juma Mgunda Moja Kwa Moja Na conclude kuwa Ni UNPROFESSIONAL COACH.

Anaendelea Kusema “KAMA AISHI MANULA ALIVYOKUWA ANACHAGULIWA NYUMA,KUNA MAKIPA WENGINE WALIKUWA HAWACHAGULIWI” Anaendelea Kuoneshaa Anaamua Kufanya kwa Kukomoana! Hii ni Very Very Unprofessional!

Hatujafika hivyo viwango vya kudharau wachezaji wetuuu! Sikumbuki jina lakini kuna mchezaji walikuwa wanamdharau sanaaa lakini Mwisho wa Siku aliisaidia timu Kuvuka kule Sudan na aliitwa baada ya Kuifunga Yangaa hii ilikuwa sio sawa!

Najaribu kufikilia psychological Effect anayoipata sasa AISHI MANULA kwa Kauli kama Hii tena Ya Kocha Wa Timi Ya Taifa.

Mchawi wa soka la Tanzania Ni Watanzania Wenyewe kama akina JUMA MGUNDA! TFF na wadau wa Soka Kuweni Makini na watu kama Hawa

Over.
Wewe ni mpumbavu manula ni gorikipa wa kiwango cha chini kabisa hafai kuwa gorikipa wa timu ya taifa, labda kakolanya siyo huyo besela lenu Manula
 
Huu ni ujinga kufikiri hivi.Wewe unakubaliana vipi na kauli ya huyu kocha kumsema maneno Aishi wakati yeye binafsi siye aliyeomba kuichezea timu ya taifa?
Swali ameulizwa na mtu mwingine,alishindwa nini kujibu kwa staha.
Hata huyo aliyepo sasa kwani si mwana Simba?
Au Juma K.Juma kawa mwana yanga siku hizi?
Mpigeni makofi au ng'oeni viti vya mahali mlipo msikubali hata kidogo
 
Neno Golikipa lenyewe huwezi kuliandika kwa ufasaha utawezaje kugundua ubora wa golikipa ?

Ile statement ya Mgunda inapaswa kutolewa na mapoyoyo tu.

Yote haya ni kwa sababu ya vitambi vya madafu.
Wewe ni mpumbavu manula ni gorikipa wa kiwango cha chini kabisa hafai kuwa gorikipa wa timu ya taifa, labda kakolanya siyo huyo besela lenu Manula
 
shida si majibu ya kocha uwaga najiuliza awa waandishi watanzania wanamatatizo gani maana awanaga maswali yamaana zaidi ya ushabikitu mbona awajawai kuuliza kaseja kuto itwa miaka yote
 
Watakapofungwa tu,tunaleta kocha kutoka nje ya nchi tuone kama Manula hatarudi golini....end justifies the means
 
Saa nyingine ni bahati ina amua na ukichukulia viwango vyao ao walio itwa na Aishi havijapishana sana, Mbona Kakolanya hapangwi marakwamara pale Simba wakati uwezo wake na Manura haujapishana? Saa nyingine mkilingana uwezo Bahati/Nyota ya mtu ina amua nani aitwe.
Mkuu hapa hatujadili sababu za kuachwa manula hapa mjadala ni majibu ya kocha ndio tatizo kwa mujibu wa mleta mada
 
Anapaswa kuwa professional badala ya kutoa majungu tu. Soon kundi kubwa la mashabiki litakuwa against na kundi zima la ufundi.

Siku yoyote wakifungwa tu kwa blunders za magolikipa tayari watu watawageuka.

Kama hawana matumizi na Aishi Manula waseme siyo kumpiga vijembe vya kipumbavu.

They must act professionally
Kuna siku Ndairagije alizungumza vizuri sana kuhusu uchaguzi wake wa Kaseja badala ya Aishi Manula kwenye mechi dhidi ya Burundi

Alisema alimwita Manula lakini akamwambia anamaumivu, alipata injury kwenye mechi ya ligi kwahiyo anaomba wamuache

Watu hawakuelewa mazingira hayo wakawa wanalaumu lakini akasema yeye kama Kocha asingeweza kumlazimisha awepo National Team wakati kashamwambia anaumwa

Hayo ndio majibu ya kitaalamu na kiweledi hasa kwa mwalimu wa kiwango cha kufundisha timu ya Taifa. Tena Ndairagije alifunguka hiyo story baada ya watangazaji kumkomalia na hilo swali lakini mwenyewe hakuwahi kufungua mdomo kulizungunzia hilo kabda. Hiyo ndio professionalism

Juma Mgunda yeye mwenyewe watu wakisema wachimbe CV yake ni mashaka matupu
 
shida si majibu ya kocha uwaga najiuliza awa waandishi watanzania wanamatatizo gani maana awanaga maswali yamaana zaidi ya ushabikitu mbona awajawai kuuliza kaseja kuto itwa miaka yote
Mkuu let's be serious kidogo. Kwa hiyo unaamin Kaseja wa sasa ni bora kuliko Manula?! Metacha Mnata kipi namba mbili wa Yanga ni bora kuliko Manula?!

Nitaamini kuna sababu nyingi na sio hii ya kiwango kushuka. Ila kauli ya huyo kocha msaidizi haina viashiria kuwa Manula ni majeruhi.
 
Back
Top Bottom