Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Kama hukuona tatizo kwenye speechi yake basi kuna tatizo somewhere.... katika karne hii ya 21 huwezi kutegemea mambo kufanyika kwa kudra za mwenyezi mungu, mvua si kitu reliable, na tatizo la umeme ni la siku nyingi. Tulitegemea raisi atuambia kuwa nitawaleta wataalumu wa kuzalisha mitambo ya nyuklia kwa ajili ya nishati ya umeme...

Mkuu I totally agree. Ndio maana napinga kabisa kusema JK ni mwanasiasa mahiri kwasababu; angekua mahiri angetoa option hii na nyingine zilizokwishatajwa hata kama hakuwa na data on hand za wapi, na kiasi cha Uranium kinachozalishwa. Kama ange-discuss different options ingetoa picha tofauti i.e. hili tatizo analichukulia serious, and at least amefanya research kidogo on some things. Kinachonishangaza zaidi si ni huyu raisi alileta timu kutoka Brazil icheze na TZ (sijajua madhumuni hasa yalikuwa nini hadi leo) lakini kama anaona hamna wataalamu wa kutatua tatizo la umeme Tanzania, si ange-make effort kama ile aliyoiweka kwenye timu ya Brazil. Ninachokumbuka kwenye mahojiano alipotajiwa kuhusu Mnyika akasema "Mimi nasema mwenye soln/idea alete tutapitia ... Sasa sijui yeye anasubiri kuletewa tu. Mbona yeye hajisumbui? He has the best opportunity to learn from the other countries but so far it looks like he is not learning anything from those frequent trips he makes.
 
Ndugu zangu,

Kuna mengine yamenipita hapa kati. Leo nimesikiliza mahojiano ya mwandishi wa BBC na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tatizo la upatikanaji wa umeme Tanzania.

Nimefuatilia pia maoni ya Watanzania mtandaoni juu ya majibu ya Kikwete. Tafsiri yangu; uongozi wa nchi ni kitu kigumu sana. Wengi wamemshambulia Kikwete kwa majibu yake kiasi wengine wamediriki kuandika; kuwa hatuna Rais.

Tunafanya makosa sana kutoa hukumu zenye kusukumwa na hisia hasi. Nimesikiliza mara mbili majibu ya Rais. Sikuona mahala pa kumshutumu Rais isipokuwa nimesikitishwa na maswali ya mwandishi wa BBC ambayo kwa Kikwete ilikuwa kama penalti alizokuwa akipigiwa mikononi na yeye kuzidaka huku akitabasamu.

Tusisahau, kuwa Kikwete ni mwanasiasa mahiri. Mwandishi anayekutana na Kikwete ni vema akajiandaa vilivyo juu ya namna ya kumbana Kikwete ndani ya majibu yake. Afanye hivyo ili kupata maswali mapya na hivyo basi habari mpya kutokana na majibu ya Rais.

Niseme tu, mahojiano yale ya Kikwete na BBC hayakutoa maswali mapya wala kuja na habari mpya. Na huo si udhaifu wa Kikwete bali mwandishi wa BBC aliyemhoji Kikwete.

Si tumemwona? Kikwete aliweza kucheza anavyotaka kwenye mahojiano yale. Na umahiri wake ulijidhihirisha pale alipogeuza sura ya mahojiano yale na Kikwete kuchukua nafasi ya mwandishi kwa kumbana mwandishi na husuan juu ya maarifa ya mwandishi katika eneo husika;

” Wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - “unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo” - tungeweza kufanya hivyo.” Kikwete anamwambia mwandishi wa BBC.

Katika mahojiano yale Kikwete alikwenda na takwimu zake mfukoni. Kama moja ya mbinu katika sanaa ya mawasiliano ili kufikisha ujumbe, mara tatu ndani ya mahojiano yale Kikwete alizungumzia MW 600 zilizozalishwa tangu uhuru na MW 145 zilizozalishwa tangu 2009, na MW 160 zitakazozalishwa ifikapo Desemba mwaka huu. Jumla zitakuwa MW 305 tangu 2009. Na hapo ndipo kwenye hoja ya msingi ya Kikwete. Ana haki kuwashangaa wasioona jitihada zake.

Na Kikwete hakosi majibu ukimwuliza juu ya umeme wa jua, upepo na mvuke. Ana hoja anaposema kuwa umeme huo pia unahitaji mipango na kuwa huwezi kupata umeme wa jua kesho kwa vile jua linawaka.

Kama msikilizaji ningependa mwandishi ambane Kikwete kwenye maeneo ya ufisadi kwenye mikataba ikiwamo yenye kuhusiana na nishati ya umeme. Hakika, kama tungedhibiti ufisadi kwenye mikataba, basi, ni imani ya wengi kuwa tungejenga uwezo wa kuzalisha MW nyingi zaidi za umeme na kwa kasi kabisa, kulifanya tatizo la umeme kuwa ni historia. Tungeweza pia kupunguza gharama za mtumiaji wa umeme.

Tuna tatizo pia la baadhi ya wanasiasa kujiingiza katika kuwekeza kwenye eneo la nishati ya umeme. Wachague kati ya uongozi na uwekezaji. Kiongozi huwezi kuwa na hisa kwenye kampuni binafsi ya kuzalisha umeme na wakati huo huo ukalinda maslahi ya umma badala ya kampuni yako.

Vinginevyo, kwa waliokuwa na utayari wa kuelewa, mahojiano yale ya BBC na Kikwete yamempa nafasi Kikwete ya kujenga hoja ya msingi juu ya nini alichofanikiwa kufanya tangu aingie madarakani katika jitihada za kutatua tatizo la umeme nchini.

Nawasilisha.

Maggid,

Sweden, Jumanne, Julai 26,2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
Tafsiri yako siyo sahih...imejaa unafiki wakati hatuna umeme plz majid be serous.
 
Tanzanians don't need certain Vikwete's media showdown.
Neither do they need these "tafsiri's".

Tanzanians need the f.....g electricity!!!!
 
ivi nchozote ambazo hazina mgao zinatengeneza mvua? hata zilizo kwenye majangwa nazo pia hazina mgao kwasababu hazina "ukame" Maajabu ya ****** Wakati wa megawat ivi mgw 145 walizozalisha tangu uhuru mbona hazikuwa na mgao mkali kama huu izi mgw 600 alizozalisha kikwete kauza wapi maana hatuzioni au ndo ziko kwenya karatasi za kutupa takwimu ambazo haziendani na hali halisi tunayoiona nchini kwetu? Afu hoja ya kuwa mkali wakati wa mahojiano hakusaidii kama anakuwa mpole wakati wa kusign mikataba mibovu,
 
Jamani wanataka kutufanya sisi watoto wadogo, toka lini teknolojia ya umeme wa jua inahitjai muda wote aliyotuambia raisi. Japo ni small scale user wa solar lakini mimi nimekuwa mdau wa nishati ya solar kwa takribani miaka mitatu sasa. Nimenua mitambo yangu yote ndani ya siku moja na siku ya pili nikafanya installation na kuanza kufaidi nishati within two days. Kwahiyo kinachohitajika ni utayari na pesa, mitambo imejaa tele nchini na hata nje ya nchi. Hakuna haja ya kupiga blablaa za kisiasa.
 
Je kama mleta hoja ameboronga kwanini asielimishwe? lazima tubadilike, nidhamu ya uoga si pahala pake hapa!
 
Katika mahojiano yale Kikwete alikwenda na takwimu zake mfukoni. Kama moja ya mbinu katika sanaa ya mawasiliano ili kufikisha ujumbe, mara tatu ndani ya mahojiano yale Kikwete alizungumzia MW 600 zilizozalishwa tangu uhuru na MW 145 zilizozalishwa tangu 2009, na MW 160 zitakazozalishwa ifikapo Desemba mwaka huu. Jumla zitakuwa MW 305 tangu 2009. Na hapo ndipo kwenye hoja ya msingi ya Kikwete. Ana haki kuwashangaa wasioona jitihada zake.
Mjengwa,
Mkuu wangu ikiwa hufahamu asili ya kitu ni bora kaa kimya kabisa..Na yawezekana huelewi matatizo ya umeme nchini yanatokana na kitu gani. Labda nikurahisishie hoja hii kwa mfano wa maisha yako mwenyewe. Unaponunua music system huwa ina Amplifier na ukubwa wa amplifier hauna maana kuna ongezeko la umeme ndani ya nyumba (Energy - Power) hivyo ndio kusema current na voltage vinaweza kuongezeka lakini hukuongeza nguvu ya umeme ndani ya nyumba yako. Na unaponunua power amp kubwa ni kwa sababu unataka ku boost sauti zaidi na sio kwamba umeongeza umeme zaidi.. neno power amp halihusiani na kuongezeka kwa energy power..

Sasa nirudi kwa JK, yeye kazi yake kama rais ni kule kwenye vyanzo vya kuzalisha umeme...iwe Songos, kiwira, Hydroelectric dams, wind na kadhalika, ambako ndiko kunakogomba ili kuwezesha uwekezaji nchini kuhimili wingi wa uwekezaji... vitu hivi vinakwenda sambamba, unaponunua amp kubwa bila shaka umetazama kwanza nguvu ya umeme unayoingia nyumbani mwako au sio.

Kwa hiyo, kuongeza hizo genarators ni sawa na kuweka amp kubwa zaidi kwa sababu unaotaka sauti ya music iwafikie mbali zaidi hali kinachogomba hapa ni nguvu ya umeme kukabiliana na amp ulonunua na muuliza swali anakuuliza makusudi kwa nini muziki wako unakata kata kila mara.. wewe unatoa defence yako kwa kuelezea ukubwa wa amplifier..Na ukirudishwa ktk swala la kuwa ni umeme mdogo unadai kuwa wewe sio Tanesco!..

Mkuu kama rais anatakiwa kutazama vyanzo vya umeme na sio majenerata acha hili lishughulikiwe na Tanesco...Nyerere aliweka MW600 huzalishwa ktk grid ya Taifa kwa sababu ndiyo kiwango kilichotakiwa kwenda sambamba na investment za wakati ule, leo hii unapoongeza hizi jenereta ktk grid ya taifa kwa MW 100 sijui 200 ni uchovu wa kutofikiria majukumu yako. Hapa wenzetu hizo jenerata zinatumiwa na mashirika binafsi yaani kampuni kama Barricks pekee walitakiwa kuwa na MW hizo..

Sasa kama rais ataona kazi kubwa kaifanya kuleta jenerata sijui hao wananchi kwa ujumla wa jenerata za petrol na Diesel walizoingiza nchi zinafika MW ngapi!.. ina maana maana nao tuhesabu walichoweza kufanya zaidi kwa Taifa hili, kitu ambacho Nyerere na waliofuata hawakuweza kuwa na watts hizo..
 
Huyu jamaa kweli zuzu.....yaan anamtetea Rais leo hii mbona hakujitolea kumshahuri mapema.
Jamani humu jamvini kuongezwe jukwaa la vilaza kwani kufanya hivyo tutakuwa tumewatendea haki kuliko kila siku kupoteza muda kujibu hoja zao za kizuzu.Hapa jukwaan kwetu tunahitaji hoja zenye mashiko tu.
 
Ndugu zangu, Kuna mengine yamenipita hapa kati. Leo nimesikiliza mahojiano ya mwandishi wa BBC na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tatizo la upatikanaji wa umeme Tanzania. Nimefuatilia pia maoni ya Watanzania mtandaoni juu ya majibu ya Kikwete. Tafsiri yangu; uongozi wa nchi ni kitu kigumu sana. Wengi wamemshambulia Kikwete kwa majibu yake kiasi wengine wamediriki kuandika; kuwa hatuna Rais. Tunafanya makosa sana kutoa hukumu zenye kusukumwa na hisia hasi. Nimesikiliza mara mbili majibu ya Rais. Sikuona mahala pa kumshutumu Rais isipokuwa nimesikitishwa na maswali ya mwandishi wa BBC ambayo kwa Kikwete ilikuwa kama penalti alizokuwa akipigiwa mikononi na yeye kuzidaka huku akitabasamu. Tusisahau, kuwa Kikwete ni mwanasiasa mahiri. Mwandishi anayekutana na Kikwete ni vema akajiandaa vilivyo juu ya namna ya kumbana Kikwete ndani ya majibu yake. Afanye hivyo ili kupata maswali mapya na hivyo basi habari mpya kutokana na majibu ya Rais. Niseme tu, mahojiano yale ya Kikwete na BBC hayakutoa maswali mapya wala kuja na habari mpya. Na huo si udhaifu wa Kikwete bali mwandishi wa BBC aliyemhoji Kikwete. Si tumemwona? Kikwete aliweza kucheza anavyotaka kwenye mahojiano yale. Na umahiri wake ulijidhihirisha pale alipogeuza sura ya mahojiano yale na Kikwete kuchukua nafasi ya mwandishi kwa kumbana mwandishi na husuan juu ya maarifa ya mwandishi katika eneo husika; ” Wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - “unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo” - tungeweza kufanya hivyo.” Kikwete anamwambia mwandishi wa BBC. Katika mahojiano yale Kikwete alikwenda na takwimu zake mfukoni. Kama moja ya mbinu katika sanaa ya mawasiliano ili kufikisha ujumbe, mara tatu ndani ya mahojiano yale Kikwete alizungumzia MW 600 zilizozalishwa tangu uhuru na MW 145 zilizozalishwa tangu 2009, na MW 160 zitakazozalishwa ifikapo Desemba mwaka huu. Jumla zitakuwa MW 305 tangu 2009. Na hapo ndipo kwenye hoja ya msingi ya Kikwete. Ana haki kuwashangaa wasioona jitihada zake. Na Kikwete hakosi majibu ukimwuliza juu ya umeme wa jua, upepo na mvuke. Ana hoja anaposema kuwa umeme huo pia unahitaji mipango na kuwa huwezi kupata umeme wa jua kesho kwa vile jua linawaka. Kama msikilizaji ningependa mwandishi ambane Kikwete kwenye maeneo ya ufisadi kwenye mikataba ikiwamo yenye kuhusiana na nishati ya umeme. Hakika, kama tungedhibiti ufisadi kwenye mikataba, basi, ni imani ya wengi kuwa tungejenga uwezo wa kuzalisha MW nyingi zaidi za umeme na kwa kasi kabisa, kulifanya tatizo la umeme kuwa ni historia. Tungeweza pia kupunguza gharama za mtumiaji wa umeme. Tuna tatizo pia la baadhi ya wanasiasa kujiingiza katika kuwekeza kwenye eneo la nishati ya umeme. Wachague kati ya uongozi na uwekezaji. Kiongozi huwezi kuwa na hisa kwenye kampuni binafsi ya kuzalisha umeme na wakati huo huo ukalinda maslahi ya umma badala ya kampuni yako. Vinginevyo, kwa waliokuwa na utayari wa kuelewa, mahojiano yale ya BBC na Kikwete yamempa nafasi Kikwete ya kujenga hoja ya msingi juu ya nini alichofanikiwa kufanya tangu aingie madarakani katika jitihada za kutatua tatizo la umeme nchini. Nawasilisha. Maggid, Sweden, Jumanne, Julai 26,2011MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
Watu wanataka umeme, eti wengine wanatafsiri rais kasema hivi!! Upuuzi na ushe... I gani huu!!??
 
He will never do that, in fact Maggid is a writer but a very tricky one with his hidden agenda, better Issa Michuzi who is straight foward! To be honest Maggid is typical writer of Michuzi type, the only difference is that he is not brave enough to reveal himself.
 
Moods Nilindeni, Mjengwa wewe ni Hawala wa Mkwe.le
 
Ndugu zangu,

Kuna mengine yamenipita hapa kati. Leo nimesikiliza mahojiano ya mwandishi wa BBC na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tatizo la upatikanaji wa umeme Tanzania.

Nimefuatilia pia maoni ya Watanzania mtandaoni juu ya majibu ya Kikwete. Tafsiri yangu; uongozi wa nchi ni kitu kigumu sana. Wengi wamemshambulia Kikwete kwa majibu yake kiasi wengine wamediriki kuandika; kuwa hatuna Rais.

Tunafanya makosa sana kutoa hukumu zenye kusukumwa na hisia hasi. Nimesikiliza mara mbili majibu ya Rais. Sikuona mahala pa kumshutumu Rais isipokuwa nimesikitishwa na maswali ya mwandishi wa BBC ambayo kwa Kikwete ilikuwa kama penalti alizokuwa akipigiwa mikononi na yeye kuzidaka huku akitabasamu.

Tusisahau, kuwa Kikwete ni mwanasiasa mahiri. Mwandishi anayekutana na Kikwete ni vema akajiandaa vilivyo juu ya namna ya kumbana Kikwete ndani ya majibu yake. Afanye hivyo ili kupata maswali mapya na hivyo basi habari mpya kutokana na majibu ya Rais.

Niseme tu, mahojiano yale ya Kikwete na BBC hayakutoa maswali mapya wala kuja na habari mpya. Na huo si udhaifu wa Kikwete bali mwandishi wa BBC aliyemhoji Kikwete.

Si tumemwona? Kikwete aliweza kucheza anavyotaka kwenye mahojiano yale. Na umahiri wake ulijidhihirisha pale alipogeuza sura ya mahojiano yale na Kikwete kuchukua nafasi ya mwandishi kwa kumbana mwandishi na husuan juu ya maarifa ya mwandishi katika eneo husika;

” Wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - “unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo” - tungeweza kufanya hivyo.” Kikwete anamwambia mwandishi wa BBC.

Katika mahojiano yale Kikwete alikwenda na takwimu zake mfukoni. Kama moja ya mbinu katika sanaa ya mawasiliano ili kufikisha ujumbe, mara tatu ndani ya mahojiano yale Kikwete alizungumzia
MW 600 zilizozalishwa tangu uhuru na MW 145 zilizozalishwa tangu 2009, na MW 160 zitakazozalishwa ifikapo Desemba mwaka huu. Jumla zitakuwa MW 305 tangu 2009. Na hapo ndipo kwenye hoja ya msingi ya Kikwete. Ana haki kuwashangaa wasioona jitihada zake.

Na Kikwete hakosi majibu ukimwuliza juu ya umeme wa jua, upepo na mvuke. Ana hoja anaposema kuwa umeme huo pia unahitaji mipango na kuwa huwezi kupata umeme wa jua kesho kwa vile jua linawaka.

Kama msikilizaji ningependa mwandishi ambane Kikwete kwenye maeneo ya ufisadi kwenye mikataba ikiwamo yenye kuhusiana na nishati ya umeme. Hakika, kama tungedhibiti ufisadi kwenye mikataba, basi, ni imani ya wengi kuwa tungejenga uwezo wa kuzalisha MW nyingi zaidi za umeme na kwa kasi kabisa, kulifanya tatizo la umeme kuwa ni historia. Tungeweza pia kupunguza gharama za mtumiaji wa umeme.

Tuna tatizo pia la baadhi ya wanasiasa kujiingiza katika kuwekeza kwenye eneo la nishati ya umeme. Wachague kati ya uongozi na uwekezaji. Kiongozi huwezi kuwa na hisa kwenye kampuni binafsi ya kuzalisha umeme na wakati huo huo ukalinda maslahi ya umma badala ya kampuni yako.

Vinginevyo, kwa waliokuwa na utayari wa kuelewa, mahojiano yale ya BBC na Kikwete yamempa nafasi Kikwete ya kujenga hoja ya msingi juu ya nini alichofanikiwa kufanya tangu aingie madarakani katika jitihada za kutatua tatizo la umeme nchini.

Nawasilisha.

Maggid,

Sweden, Jumanne, Julai 26,2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo

600 MW, 145 MW, 160 MW are just figures but there is a different in the old days and nowadays, during my tender age i didnt experience such a problem so if there is improvement on production of Mw from independence and current production why this crisis now????

ITS BETTER BEING THE LAST IN THE CLASS WITH AN AVERAGE OF 81 THAN BEING THE FIRST WITH AVERAGE OF 21.
 
Hizo MW 160 zilizo mbioni nadhani zitakuwa ni zile Wataalamu wa Kichina watafua na kugavi kutoka "tabasamu lake la kufwa mutu" kutumia cutting-edge nanotechnology.
 
Maggid,

Kuna vitu vingine katika maisha vinahitaji akili ya mwendawazimu kuvitetea. Rais anapotoa majibu ya kiholela kama " serikali haiwezi kuleta mvua" kwenye tatizo linalogusa mstakabali wa taifa, ni lazima tukemee hicho kitendo. Kwanza kabisa, Kikwete ni part ya hili tatizo! Yeye ndiye aliyekuwa waziri wa nishati walipoleta ile kampuni ya Malyasia pale Tegeta. Ikumbukwe ya kuwa , mkataba mbovu kati ya serikali na hii Kampuni ya Tegeta( nimeisahau jina) imechangia sana katika kuifilisi Tanesco.

Kikwete amejivuna ya kuwa wameweza kuongeza MW 305 tangu 2009 ni kichekesho cha hali ya juu, na kwa kiasi fulani ameonyesha jinsi alivyoweka bar chini. Nyerere aliweza kutengeneza grid ya taifa kipindi hicho wakati pato la taifa likiwa chini sana na hakuwa na watalaamu wengi.
 
Toka uhuru MW 600, awamu ya JK MW 305. Hizi ni takwimu tamu sana. Ni sawa na mwanafunzi anayempelekea baba yake ripoti ya matokeo inayoonyesha mwanae alikuwa wa tatu darasani. Baba anaanza kusherehekea bila kujua darasan kuna wanafunzi watatu na hivyo mwanae ni wa mwisho darasani. Tunataka umeme na sio mgao wa umeme. Akumbuke toka uhuru, hatujawahi kuwa na mgao mkali kiasi hiki kwa sababu ya ukame au sababu nyingine yeyote.

Ndugu mtoa tafsiri, namshukuru Mungu kwa thread yako maana pamoja na exposure kubwa ya mambo ya kitaifa na kimataifa,bado wewe ni mnafiki. Usingekuwa na exposure uliyonayo, leo hii wewe ungekuwa mchawi! Yaani wewe Kanjanja leo una balls za kumkosoa mwandishi mwandamizi wa BBC kwa 'tafsiri' yenye chongo kama hii? Wewe, Rweyemamu na wenzenu mnaotuuza utumwani, historia itawahukumu!
 
Katika mahojiano yale Kikwete alikwenda na takwimu zake mfukoni. Kama moja ya mbinu katika sanaa ya mawasiliano ili kufikisha ujumbe, mara tatu ndani ya mahojiano yale Kikwete alizungumzia MW 600 zilizozalishwa tangu uhuru na MW 145 zilizozalishwa tangu 2009, na MW 160 zitakazozalishwa ifikapo Desemba mwaka huu. Jumla zitakuwa MW 305 tangu 2009. Na hapo ndipo kwenye hoja ya msingi ya Kikwete. Ana haki kuwashangaa wasioona jitihada zake.

Kwa mtu ambaye alishawahi kushika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati, kuhadaa watu na hizo takwimu za "MW" kabla na baada ya kuwa rais is plainly deceptive if not straight out fraudulent. Hiyo ni kama slum dunk ya LeBron James against Pazi Basketball Club or whatever. Pato la Taifa na idadi ya watu Tanzania ya leo siyo sawa na enzi za Nyerere, achilia mbali maendeleo makubwa kwenye teknolojia mbadala za nishati yaliyotokea tokea enzi za Nyerere hadi hii leo. Nadhani sooth ameweka wazi hapo juu kwamba kuzungumza in relative terms is simply meaningless without explaining the relevant contexts.
 
Back
Top Bottom