niliweka link watu wakapate huduma ya vitabu vyetu, ikawa nongwa..hahaha, hata hivyo nawaheshimu, hii ni website yao wanastahili kuendesha wapendavyo na kuweka sheria wazipendazo kwasababu ni mali yao. ila nashukuru walinipa ban ya siku mbili tu, zimeshaisha sasaivi nipo ulingoni.
kujibu swali lako, kama mmeshatimiza miaka miwili, watu wanaowazunguka wanawaona kama mume na mke, either of you hakuna ambaye alishawahi kufunga ndoa ambayo haijavunjika, na mpo kwenye watu wenye vigezo vya kuoana....basi hapo itabidi presumption of marriage iingilie kati wakati wa kugawana mali. presumption of marriage ni dhana ya ndoa...yaani hapo hamna ndoa ila ili kugawana mali mnadhania tu kama mmeoana, mtagawana mali kulingana na mchango wa kila mtu, kila mtu achukue hamsini zake. hauwezi kuondoka na mali ambazo mlichuma pamoja na mwenzio katika mazingira ya namna hii.
isipokuwa (ambayo sasa sio facts za kesi yako), kama umehamia kwa hawara wakati una ndoa inayoendelea, hamjaishi miaka walau miwili, na mmeishi kwa kificho tu watu wanaowazunguka hawako kwenye mazingira ya kuamini kama mmeoana au la, hapo hata kama mmechuma mali pamoja presumption of marriage haipo. (hii ni saa saba usiku, kama sijakujibu vizuri niulize tena kesho yawezekana ni usingizi).