MAJIBU YA MASWALI MBALIMBALI YALIYOTEKA MJADALA WA CHANJO YA CORONA KULETWA NCHINI
Toka Serikali kupitia kwa Kamati maalum aliyoiunda Rais Samia Suluhu Hassan itangaze uamuzi wa kuruhusu chanjo kuja na toka chanjo iingie nchini, kumezuka mjadala mkubwa sana kwa Watanzania, kila mtu akisema lake kuhusu uamuzi wa chanjo kuletwa nchini. Wengine wakipongeza uamuzi huo kwamba ni wa kuokoa Watanzania hasa kipindi hiki cha wimbi la 3 la Corona, wengine wakiponda na kuweka hofu kwa chanjo hiyo kwa minajili mbalimbali ikiwemo kuwa imegandisha damu baadhi ya maeneo, wengine inasababisha kifo, wengine ni mpango wa Mataifa ya nje kutumaliza Waafrika (Watanzania), mara sio salama na mengine mengi.
Nimepitia mitandaoni na kufuatilia mjadala huu kuhusu uamuzi wa Serikali kuruhusu chanjo kuja nchini na haya ni maswali ya Watanzania yanayozunguka sana kwenye mjadala huu wa chanjo ya Corona. Nimeona nianze kuyajibu maswali ambayo pasi na shaka nimejiridhisha majibu yake kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya habari duniani na kupitia kwa Wataalamu mbalimbali.
1. Je, Serikali ya Rais Samia imesaliti mawazo ya awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli kukataa chanjo?
Jibu: kwanza ni uongo mkubwa kabisa kusema Serikali ya Rais Samia imeisaliti au imemsaliti Rais Magufuli kwenye chanjo. Hakuna sehemu yoyote ambayo Rais Magufuli mwenyewe akiwa hai au Serikali yake ilikataa chanjo ya Corona. Msisitizo wa Rais Magufuli na Serikali yake ilikuwa ni kuitaka Wizara ya afya ijiridhishe na hizo chanjo kabla ya kuzikimbilia. Msimamo huu aliutoa Rais Magufuli mwenyewe akiwa Chato mkoani Geita wakati anafungua shamba la miti, Januari 27 mwaka huu.
Kwahiyo, Rais Samia hajasaliti Serikali ya mtangulizi wake ya Hayati Rais Magufuli ambayo yeye alikuwa sehemu bali Serikali yake imefuata ushauri wake kwa kujiridhisha na hizi chanjo kupitia kuunda Kamati Maalum ya Wataalamu kujiridhisha ya kushughulikia ishu ya Corona. Kamati hiyo yenye Wataalamu tupu wa afya irijiridhisha ndipo bila kukimbilia ikajiridhisha na kuamua kuruhusu chanjo kwasababu ni salama na inafaa kutumika kupambana na ugonjwa huu hatari wa Corona unaosumbua dunia nzima. Kwahiyo ushauri wa Hayati Magufuli wa kujiridhisha na chanjo hii kabla ya kuileta umezingatiwa na ndio maana tumechelewa sana kuleta chanjo hii kwa muda mrefu tukijiridhisha chini ya Wataalamu wa afya.
2. Je, chanjo iliyoletwa Tanzania ya Johnson & Johnson imepigwa marufuku kutumika na kwamba ni mbaya?
Jibu, si kweli, chanjo hii haijapigwa marufuku. Kama mnavyofahamu wakati wa majanga makubwa kama haya wanaweza kutokea watu wasio na nia njema (matapeli) na kutaka kutumia upenyo huu kujinufaisha na kutengeneza chanjo feki. Mwezi wa 4, matapeli walitumia chapa ya chanjo hii kuingiza chanjo zao feki mtaani ambazo ndiyo hizo zilikamatwa na kugundulika kugandisha mpaka damu maeneo mbalimbali duniani. Shehena ya hizo chanjo ikakamatwa na ndipo wazalishaji wakazuia kidogo hii chanjo ili kujiridhisha mpaka baadae Aprili 23 walipoamua kuendelea na uzalishaji na usambazaji wake.
Kwahiyo, si kweli kwamba chanjo hii imepigwa marufuku. Marekani mpaka sasa watu wake zaidi ya milioni 8 wamechanja chanjo hii ya Johnson & Johnson na Mataifa mengine zaidi ya 50 kote ulimwenguni wanaendelea kutumia na kuchanja hii chanjo.
Kizuri zaidi kwenye chanjo hii ya Johnson & Johnson ni chanjo moja tu (one shot). Ukichanja leo imetoka hiyo huna haja ya kurudia. Zile chanjo nyingine kama Pfizer, Astrazeneca, Moderna na zingine itakutaka kurudia kuchanja kukamilisha dozi lakini hii ukichanja umemaliza dozi na huhitaji tena kurudia kwahiyo kwa mazingira ya Kitanzania na Kiafrika hii chanjo inatufaa sana sababu unatujua tena Wabongo na mazingira yetu kusema ziwe dozi nyingi tunaweza kukwama uchache wa chanjo, ufuatiliaji na mengine.
3. Je, chanjo hizi ni mpango wa Mataifa ya nje kuua Waafrika (Watanzania)
Jibu, kwanza ukimkuta mtu anayefikiri hivi basi atakuwa na mawazo ya mgando sana na mtu mjinga. Sisi Waafrika tunapaswa kuwa wa mwisho kutamka maneno ya hovyo kama haya. Hivi Mzungu au hayo Mataifa ya nje yakitaka kutumaliza sisi Waafrika wangesubili eti mpaka ije Corona walete chanjo ndo watumalize? Sisi toka tunazaliwa kila tunachokitumia ni vya kwao. Dawa tunazomeza, mitambo ya kufanya upasuaji mpaka wa magonjwa ya kutisha kama ya kwenye moyo, ubongo na kila kitu vya kwao. Vyombo vya usafiri vyote kuanzia baiskeri, pikipiki, meli, ndege, magari vyao. Yani kila kitu chao. Sasa wangetaka kutumaliza wangesubili mpaka chanjo ya Corona? Si wangetumalizia huko tu na kwingine kabla hata ya kuja kwenye chanjo hii ya leo.
Kwahiyo mawazo kwamba chanjo hii ni mpango wa kuwamaliza Waafrika ni mawazo yanayoweza kutoka kwa mtu mjinga na mpuuzi sana. Chanjo sio jambo geni Afrika au hapa duniani na hapa nchini. Toka tunazaliwa tunachanjwa machanjo ya polio, surua, pepopunda na mengine na mpaka leo watu tunaishi, tunazaana mpaka hapo Mungu tu kwa kudra zake anapokutwaa. Kwahiyo ishu sio chanjo ya Corona sababu machanjo yamekuwepo Tanzania na Afrika miaka kwa miaka na bado hujakufa mtu wala kukosa kizazi au hizo imani potofu zilizopo zaidi tu ya Afrika kuendelea kuongoza kuzaana duniani.
4. Je, chanjo hizi za Corona zina madhara?
Jibu, kwanza lazima tufahamu hakuna dawa yoyote duniani ambayo haina madhara. Kila dawa ina madhara lakini kinachopimwa ni madhara yawe kidogo sana dhidi ya faida. Yani faida ziwe nyingi kuliko madhara kwahiyo kila dawa (chanjo) ina madhara yake.
Hata Paracetamol ambazo zinasemwa ni kiboko ya maumivu zina madhara yake kwa mtumiaji, quinine zina madhara mpaka panadol. Yani kimsingi kila dawa ina madhara, kinachoangaliwa tu madhara yasiwe makubwa kiasi cha kumsababishia kifo au madhara makubwa mtumiaji.
Mwili unapopokea kitu kipya kimsingi lazima pawe na diverse response. Hata ukishindia mihogo au dona la kutosha utahisi mwili uchovu na tumbo hivi kuzingua sababu tu mwili umepokea kitu. Kwahiyo madhara madogo madogo yanayoripotiwa kwenye chanjo hizi za Corona ni ya kawaida na ni kama tu ambayo unaweza kupata hata ukimeza panadol, aspirin au caffeine. Kimsingi tunaangalia imesaidia wangapi dhidi ya wale kidogo waliopata madhara ya kawaida. Kama kawaida, kanuni ya dawa yoyote duniani ina madhara lakini ni tu yasiwe makubwa kuliko faida zake.
5. Je, chanjo hii imekuja kwa haraka?
Jibu, ndiyo imekuja kwa haraka kutokana na ugonjwa nao kuwa wa mlipuko na kuleta madhara ya kutisha dunia nzima hivyo kuilazima dunia kutafuta njia ya haraka kuokoa maisha ya watu. Hivi jiulize hata wewe, kipindi kile dunia inapoteza mpaka watu elfu 10 kwa siku, ukitaka dunia ifanyaje kuokoa watu? Yani usubili miaka 10 wakati huku watu wanaendelea kufa. Mimi na wengine tunaamini inawezekana madhara madogo yanayojitokeza yanahusiana na kuwahi kwa chanjo zenyewe lakini kwa kiasi kikubwa sana cha zaidi ya asilimia 98 chanjo hizi zimeokoa mamilioni ya watu duniani na kushusha pia kwa mamilioni visa na idadi ya maambukizi. Jiulize Taifa gani tena sasa hapa duniani linaripoti maelfu ya visa kwa siku? Au jiulize nchi gani tena baada ya chanjo hizi inaripoti tena vifo zaidi ya elfu 3 kwa siku? Hayo yote ni matokeo ya chanjo hizi.
Wanasayansi duniani walimobilize resources zao kwa pamoja na kutafuta suluhu ya kuponya watu kwa haraka ndipo hatua nyingine zaidi zifuate. Hata wewe ukiwa na njaa usisubili upate msosi mzito wa kushiba, ukiokota hata kitumbua anza nacho kukila kupambana kujiokoa huku ukipambania kikubwa. Na huo ndio ununda, ukileta ubishoo utakufa siku si zako. Kwahiyo dunia ilireact mapema kuokoa watu huku ikiendelea na jitihada za kupata suluhu ya kuduma ya janga hili. Tusingeweza kusubili mpaka miaka 10 ndo tupate complete vaccine wakati huku watu wanaendelea kuteketea.
Halafu sio chanjo ya Corona tu ndiyo imewahi, hata ugonjwa kama ebola na mengine yaliporipuka chanjo ilipatikana ndani ya miezi 6 tu. Hata mripuko wa kirusi cha SARS ulioikumba China miaka 18 iliyopita chanjo yake iliwahi sana, hata kirusi cha MERS kilichoripuka Saudia Arabia mwaka 2012 chanjo yake pia iliwahi sana. Kwahiyo sio chanjo ya kwanza ya mapema na sio jambo geni unapopambana kujinasua na si chanjo ya mapema kuwahi kutokea hapa duniani pindi janga linaloteketeza watu linapotokea.
6. Je, ukipata chanjo unaweza kuambukizwa na Corona?
Jibu, ndiyo unaweza kuambukizwa na Corona kutoka kwa mtu ambaye hakupata chanjo. Kwahiyo unaweza kuwa umepata chanjo lakini kwasababu umekutana na mtu mwenye ugonjwa na hajachanja basi ukapata Corona na ndio maana msisitizo ni mkubwa sana kwamba watu wengi zaidi wachanje ili kuondoa uwezekano wa wewe ambaye hujachanja kumuambukiza mwenzako aliyechanjwa.
Kwahiyo ni muhimu sana Watanzania tuendelee kujitokeza kupata chanjo ili tuondoe uwezekano wa kuambukizana kwa wale wasiopata chanjo. Nakupa mfano, leo hii kwenye Mataifa ambayo maambukizi yalikuwa juu sana kama Marekani na nchi nyingi za Ulaya maambukizi yameshuka sababu tu watu wake wengi zaidi wanaendelea kupata chanjo na hivyo kuondoa uwezekano wa kuambukizana.
7. Je, Serikali inakwepa kuwajibika kama chanjo zikileta madhara kwa mwananchi?
Jibu, kwanza sio kweli kwamba Serikali inakwepa kuwajibika ikiwa chanjo italeta madhara. Utaratibu wa kwamba Serikali au mtoa huduma hatawajibika na chochote kama matibabu yakiwa na madhara ni utaratibu wa kawaida sana na unaotumika hapa nchini na kote duniani.
Hata ukiachana na chanjo, leo hii hata ukitaka kufanyiwa upasuaji (operation) iwe ya uzazi, uvimbe n.k unasaini au familia na wauguzi wako wanasaini fomu ya kukubali matokeo yoyote ya matibabu. Ikitokea mgonjwa amefariki huwezi kudai daktari akulipe kwasababu ya kifo cha mgonjwa wako kwahiyo huo ni utaratibu uliozoeleka na unaotumika kote duniani.
Makala hii imeandikwa na Bwanku M Bwanku anayepatikana kwa simu no: 0657475347 kwa msaada wa mitandao na maelezo ya Wataalamu mbalimbali wa afya wa Tanzania na duniani kwa ujumla.