Majibu ya nesi huyu yamenikanganya.

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Ni hivi juzi nilienda hospital kwa dhumuni la kujua afya yangu.
Ajabu nilivyochukuliwa damu tayari kwa kipimo nesi yule alichukua muda mrefu kunipatia majibu hali iliyopelekea kuingiwa na hofu labda majibu hayako mazuri na nesi anatafakari jinsi ya kunifikishia.
Baada ya muda mrefu akaniita na kunipatia majibu yangu kua ni negative virology. Nikafurahi lakini nilishindwa zuia dukuduku langu. Nikamuuliza ilikuaje alichukua muda mrefu mpaka nikapatwa wasiwasi akanijibu. Ilichukua muda mpaka kupata majibu ya jumla mana kuna kipindi kipimo kinasoma positive halafu ukirudia tena kinasoma negative.
Hapo ndio nilipatwa na utata.
Hebu wataalam nijuzeni ndio kawaida hii kipimo cha hiv kuleta majibu dizaini hii?
 
Naomba nipe details walitumia kipimo gani au kama ni mashine basi niAmbie ili nitolee maelezo kidogo hili
 
Naomba nipe details walitumia kipimo gani au kama ni mashine basi niAmbie ili nitolee maelezo kidogo hili
Alichukua damu kwa syringe sio kwa kutoboa kidole sikuuliza aina ya mashine alotumia. Je kuna baadhi ya mashine zinakawaida hiyo ya kuonesha positive na negative kwa sample hiyo hiyo?
 
Alichukua damu kwa syringe sio kwa kutoboa kidole sikuuliza aina ya mashine alotumia. Je kuna baadhi ya mashine zinakawaida hiyo ya kuonesha positive na negative kwa sample hiyo hiyo?
Sometime huwa inakua kwa baadhi ya machine system zinaweza toa majibu hayo kama ile damu haija meet sample criteria maana inawezekana wakati wa kuchukua damu au wakati wa kuiandaa kuipima inaweza kutoa majibu ambayo ni inditerminant hivo haikua na haja ya kuirudia sample hiyo bali ni kutoa sample mpya na kuipima tena na kama wanatumia ELISA basi pia preparation na incubation time inaweza sababisha sample ikasoma optical density(OD) ya 0.5 S/CO ambayo hii kwa machine inaitambua kama positive ila wakati wa ku interprete majibu hii inakua ni inditerminant means unatakiwa urudie tena kupima ndani ya miezi 3 sababu kwa machine za Hiv na optical density nyingi huanzia 0-1 S/CO ina maana any optical density ya 1 na zaidi ya 1 basi test hiyo ni positive na
0.5 hii inaweza kadiriwa kama nusu ya 1 basi hii pia ni markar ya positive na haitaripotiwa kama positive bali inditerminant (0.5 mpk 0.9) na >1.0 zinakua ni positive zote hizo
Hizi ranges ni kwa baadhi ya test kama HIV, HEPATITIS B na HEPATITIS C ambazo ni blood borne disease na maambukizi yake yanafanana
Ok karibu nadhani umeelewa
 
Duh tumia lishe zaidi
 

Negative virology ndio kitu gani?

Halafu kwani kujua afya yako maana yake ni kupima HIV?Kwanini ubongo wako umeji lock kwenye HIV na si kitu kingine kama vile kupima moyo,figo,ini nk?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…