Majibu ya Pastor Tony baada ya kubezwa, hayaridhishi

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Mchungaji Tony Kapola ajibu wanaomkosoa kuhusu muujiza wa kupuliza mtungi wa gesi

Baada ya kusambaa kwa video ikimuonyesha Mchungaji mke wa Mchungaji Tony Kapola akieleza muujiza wa kujaza gesi kwa kupuliza mtungi na kutumia zaidi ya siku 14 kumaliza gesi hiyo, kumeibuka mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wengine wamemkosoa na kumbeza, wakipinga ukweli wa muujiza huo. Hata hivyo, Kapola ametoa majibu yake kwa wale anaosema wanamdhihaki:

"Ukimaliza kunibeza, utaenda kwenye nyumba yako ya kupanga, mimi naenda kwenye nyumba yangu ya maana.
Ukimaliza kunibeza, utachukua Uber, mimi napanda mashine yangu.
Of course mimi siendeshi magari, naendesha mashine.
It doesn’t matter, mimi naishi the best life of my life." ---> Mchungaji Kapola

Maneno haya yamezua maoni mseto, baadhi wakimuunga mkono na wengine wakionekana kuendelea kutilia shaka simulizi lake la muujiza huo.

Niliwahisema miujiza ya nguvu za giza Yana mdaa yakiianza kukuaibisha dunia inakuchukiaa
 
haya yote yameletwa na mwanamke mmoja tu na tony anachojaribu kukifanya ni kumtetea mke wake na sio kuwaprove wrong wanaomkosoa.
 
Mbona anawa bagaza wasio amini.?
Asiyeamini muujiza huu anaweza kuamini muujiza mwingine.
Ilipaswa ajibu kwa miujiza sio kubagaza wenye imani haba.
Kujibu kwa mhemko ni kiashiria bado hajakomaa..
Ajifunze kwa akina Mwamposa,Geo Davie,Kuhani Mwacha.
Wamekuwa wakipigwa spana mpk na wachungaji wakubwa wenzao lkn husalia kimya ama baada ya muda mreefu kwenda ndo hujibu.
Yeye siku mbili tuk
Kajaaa kwelikweli.
Huenda anapenda kuzingumziwa yy na mkewe mitandaoni.
 
Mnatuvuruga mjue,sisi tunasubiri nabii za ma miamba na mavisiki mazito mazito kurudisha kadi kwa muumba,nyie mnaleta habari za magesi,na mnalalamika kama mmepeleka sadaka vile.
 
Amepanic sana, nimemsikiliza ila naona ni mtu ambae hana kifua cha kuhimili kejeli za wabongo anaishia kuwajibu kwa kejeli pia na kuwabeza, so sad
 
Lazima kashinikizwa na mkewe
 
Huyu jamaa sio mara ya kwanza kuropoka hivi. Kipindi cha siku si nyingi nyuma hapa,alituhumiwa kutoka nje ya ndoa nadhani Mange Kimambi alimtuhumu kutembea na Niffer.

Alipohojiwa kwakweli aibu niliona mimi. Alikuwa anaongea kama mvuta bange bila hekima. Anamwambia muandishi kuwa hao wanaosema mimi wameshuhudia kuwa nimefanya na mtu basi na wao nimewafanya hivyo hivyo itakuwa na wao nimewala na kuwafanya.

Anaongea kwa kupanic kabisa. Kimsingi jamaa hajui kuvunga wala kutuliza akili anaamini chochote anachosema kitachukuliwa kirahisi na hata kama kitakuwa cha hovyo basi waumini wake na jamii watamsamehe bila kumjudge.

Saa hii ameanza kuwa na kiburi sababu ya maokoto.
 
Tayari hela za michongo ya kanisa zimemfumba hekima huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…