Majibu ya rufaa yangu baada ya kufukuzwa kazi serikalini

Makox

Senior Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
125
Reaction score
163
Poleni na majukumu ndugu zangu Wanafamilia ya JamiiForums!

Nimerudi Tena kuleta mrejesho na kuomba kuendelea kuongezewa uwezo kwani naamini kuwa humu mpo baba zangu, mama zangu na wengine wengi.

NINAWAHESHIMU na KUWATHAMINI SANA kwa umuhimu wenu.

Mapema mwaka huu Baada ya kutengenezewa tuhuma na kunisababishia nifukuzwe kazi Nilileta taarifa iliyokuwa na kichwa "MKUU WA SHULE NA MZAZI WA MWANAFUNZI WALINITENGENEZEA ZENGWE MPAKA NIKAFUKUZWA KAZI"

Kwa kipindi kile nilikuwa nimekata rufaa ngazi ya TSC Makao makuu na nilikuwa ninasubiri ushughulikiwaji wa rufaa yangu iliyochukua muda mrefu kutokana na tume kusubiri uteuzi baada ya kumaliza muda wake.

NDUGU ZANGU WANAJAMII FORUM; Kwa ukurasa huu ninatumia fursa hii kuwataarifu matokeo ya rufaa yangu baada ya kupitiwa na kutolewa maamuzi.

Rufaa ilipitiwa na nilipewa taarifa iliyonitaka nirejeshwe kazini na tuhuma ianzishwe upya kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu.

Nilipewa majibu ya rufaa yangu japo kwa kuchelewa kidogo kutokana na changamoto za kimawasiliano.

Ndugu WANAJAMII FORUM; kwa sasa nilikwisharipoti kazini katika kituo changu Cha zamani na ninaendelea na Majukumu yangu ya kazi.

Katika ukurasa huu ninaomba sana ndugu zangu mniongezee uwezo kwenye mambo kadhaa muhimu sana;

1. Tuhuma imeanzishwa upya, kosa ninalotuhumiwa nalo ni "KUWA NA TABIA YA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWANAFUNZI YANAYOASHIRIA KUTAKA KUFANYA NAYE NGONO KINYUME NA KANUNI"

T.S.C Wilaya wameanzisha kesi upya kwa kosa lile lile nililokuwa nimetuhumiwa na kuhukumiwa mwaka Jana.

Nilipewa notisi na hati ya mashitaka iliyotaka nitoe utetezi ndani ya siku kumi na nne na Nilifanikiwa kuandika na kuwasilisha utetezi ndani ya muda niliopangiwa na kwa sasa ninasubiri mrejesho wao.
Ombi langu katika hili ni ushauri wa namna yoyote ile kutoka kwenu.

2. Barua yangu ya kurejeshwa kazini ilikuwa na nakala iliyotaka Mkurugenzi anirejeshe kwenye payroll ya malipo ya serikali, lakini ni miezi miwili sasa sijarudishwa kwenye payroll. Je nifuate taratibu zipi ili nirudishwe kwenye payroll?

3. Wafanyakazi wezangu katika kituo changu Cha kazi kwa sehemu kubwa ni wale wale waliotumika kutoa ushahidi wa uongo nikafukuzwa kazi, baada ya kurudi nawaona hawako sawa hasa kwa upande wa kunipa ushirikiano na misaada ya kikazi. Je nifanye Nini niendane nao?

NDUGU WANAJAMII FORUM ninawategemea sana katika kuniweka sawa kiakili na kimwili.

Ninatanguliza Shukran zangu za dhati, MUNGU AENDELEE KUWA NANYI NA KUWABARIKI🙏🙏​
 
Poleni na majukumu ndugu zangu Wanafamilia ya Jamiiforum!

Nimerudi Tena kuleta mrejesho na kuomba kuendelea kuongezewa uwezo kwani naamini kuwa humu mpo baba zangu, mama zangu na wengine wengi...​
Pole Sana mkuu na hongera kwa hiyo hatua

Ila ukiweza jiepushe na migogoro eneo la kazi maana eneo la kazi ndo sehemu unayotumia Muda wako mwingi katika kuutafuta mkate.
 
Poleni na majukumu ndugu zangu Wanafamilia ya Jamiiforum!

Nimerudi Tena kuleta mrejesho na kuomba kuendelea kuongezewa uwezo kwani naamini kuwa humu mpo baba zangu, mama zangu na wengine wengi...​
Kama hujakamatwa ukifanya mapenzi (kama hakuna ushahidi), kuhusu tu kwamba una 'tabia inayoashiria kutaka kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi' siyo issue.

Issue ni je kuna ushahidi wa kufanya mapenzi na mwanafunzi? X anaweza kuwa anamuwaza Y ambaye ni mtoto wa shule, kama yakibaki tu mawazo ya kichwani, ambayo hayana ushahidi unaojionyesha kwenye vitendo kwa sheria za Tanzania hakuna kitu hapo.
 
Polee na Changamoto za maishà mselaa wangu mwanadamu ujafa ujaumbika ,mbingu Yako n hapa hapa duniani na jihanamu Yako n hapa hapa mkuu Cha msingi n kupambania mpk tone la mwishoo...


VP uwezi kuomba uhamisho ukaenda fundisha sehemu nyingine maana hapo ulipo pameshakukataaaa kamandaa...
 
Poleni na majukumu ndugu zangu Wanafamilia ya Jamiiforum!

Nimerudi Tena kuleta mrejesho na kuomba kuendelea kuongezewa uwezo kwani naamini kuwa humu mpo baba zangu, mama zangu na wengine wengi...​
Mimi nahisi una upekee katika ufanyaji wako wa kazi na hii inawaogopesha sana. Litakwisha hilo. Uongo haudumu. Wewe Jiamini. Sali sana. Mungu atafungua njia.
 
Poleni na majukumu ndugu zangu Wanafamilia ya Jamiiforum!

Nimerudi Tena kuleta mrejesho na kuomba kuendelea kuongezewa uwezo kwani naamini kuwa humu mpo baba zangu, mama zangu na wengine wengi...​
Tafuta mwanasheria haraka, wamesema shauri lianze upya ili wakufukuze vizuri baada ya kugundua awali kuna makosa yaliyopo kwenye mwenendo wa shauri.
 
Usifikiri kuwa mashtaka kuanza upya ni upenyo wa wewe kuepuka adhabu.Kuna scenario kama yako ilitokea huku kwetu,tofauti ni nsture ya makosa. Huyu alituhumiwa kwa utoro,na ni kweli yeye hakuwepo kazini muda mrefu. Kesi iliporudishwa taratibu zikaanza upya na sheria zikafatwa na akafukuzwa.

Sasahivi waliokushitaki hawatafanya tena makosa yaliyosababisha rufaa iamue kuanza upya mashitaka.Ukiomba uhamisho hautakubaliwa mpaka shauri liamuliwe.Kitakachokuokoa ni utetezi wako
 
Pole sana kwa changamoto uliyonayo, kama unaamini katika nguvu za Mungu basi mtafute Mungu kwa bidii.

Kibinadamu hili suala linawe likamaliza energy yako kabisa, usiweze kufurahia hata kazi yenyewe. Tafuta mwanasheria awe anakupa mwongozo katika kila hatua. Hi itakusaidia kutokuchukulia vitu personal na kuingia katika migogoro au chuki zaidi na/au kushindwa kujitetea vizuri kwenye kesi.

Kwa mda huu kaa mbali tu ikiwezekana na watumishi wenzako huwezi jua nani ni adui wako kwa sasa.

Ukishinda hii kesi omba uhamisho, japo kama una imani wabaya wako watahama wao 😂

Usife moyo mkuu,
 
Sijawahi hata kumtongoza mtoto ninayetuhumiwa naye. Hata mara ya kwanza walitumia ushahidi wa kulazimisha Tena kwa nguvu mpaka za polisi
 
Tuliza akili wao ndiyo wana jukumu kubwa la kuthibitisha tuhuma pasipo kuacha shaka.cha msingi kwako ni kucheza na akili zao uzuri moja wote kitaaluma ni walimu hatua zao ni chache.wataaibika na hakikisha unabaki kazini,nitakushangaa ikitokea umefukuzwa kazi na hao walala hoi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…